Mchungaji Lwakatare Arudisha Yatima 250 Kwao

Haya sasa!
Kumjadili mtu na huku facts kwanza ni potofu.Ndugu kwani huyu Mchungaji kakukosea nini hadi utake kumchafua humu mtandaoni? Kama anayoyafanya ni rahisi hebu na wewe ujaribu halafu na sisi tuje hapa tukujadili.Kwamba anaendesha kanisa kwa misingi usiyoipenda, hiyo siyo juu yako kumhukumu.Yuko JUDGE MKUU wa kuhukumu kila mtu hiyo siku ikifika.

Kama yupo Jaji mkuu wa kumhukumu mbona tunawajadili mafisadi hapa na watu kibao. Why cant she be discussed hapa jamvini??. Au mwambia Mods aondoe celebrity forum. Najua nimewagusa wengi bt habari ndio hiyo! Ni watu gani wanapaswa kujadiliwa kama mkuu wa kaya anajadiliwa. Mbona waraka wa kikatoliki na mahakama ya kadhi vilijadiliwa?? Vp WOS, mbona unaniangusha Madam?
 
Duniani watu wanagawanya ktk makundi matatu (3) ktk dhana ya civilization.
Kundi 1 (uncivilized): Watu hawahukaa na kuwajadili watu
Kundi 2 (Civilizing...): Watu hawa huwa wanapendelea kujadili vitu
Kundi 3 (Civilized): Hawa huwa wanajadili ideas, issues ...

Wewe upo ktk kundi lipi?
Contextualize. Copy and paste does not always work!
 
Sina la kusema kuhusu hayo mengine.Nimeongeza rangi nyekundu kwenye maandishi yako.Attached is the document i request you to read.Humo utaona Founder wa Dovetel(Brand name ni SasaTel) ni nani(Peter Chitamu) na nini role(Malipo ya awali katika mradi huo) ya Mama Lwaakatare.

Huko nilishasoma kitambo kaka. Siwezi kukulazimisha usome nilichoandika kaka, lakini ukweli ni kwamba ana 40% ungeniwekea copy ya MEMARTS tukaona shares zilivyo hapo ningekuelewa! Lakini management na board members haitoshi kuonesha nani mmiliki. Joyce mhavile ni mkurugenzi wa radio one na ITV na si Reginald Mengi, na bado anaweza uenyekiti akamwachia mtu mwingine!
 
Nampa hongera sana huyu Mchungaji Lwakatare.
1) Kwanza ni mwanamke mchungaji, na kazi anayofanya kweli inaleta utukufu kwa Mungu.
2) Ni mjasiliamali, hivyo kaleta ajira nyingi tu kwa wanawake na kwa wanaume. Kaanzisha shule, radio station ile ya praise power, SASATEL na sasa anataka kuanzisha hiyo Foundation ya christian women. Vitu hivi vyote vinaleta maendeleo kwa taifa letu na ajira nyingi tu.
3) Hivi ni mbunge vile vile huyu mama, analitumika taifa lake pia.
Na tukumbuke, huyu mama ni binadamu, kama binadamu kila mtu ana mazuri na vile vile ana mapungufu yake. Aliye kamili ni Mungu peke yake.
Hivyo mimi nampa big up mama Lwakatare kwa kazi zake anavyofanya za kumtumikia Mungu na Taifa vile vile.

Mbona hukutaja asasi yake ya zamani ya Mission to the Needy aliyoitumia mwaka 1984 kupitishia pesa za wakimbizi wa Uganda, kuwadhurumu pesa zao, kula njama na mashushushu na hatimaye kuwaua hao beneficiaries baada ya siri kuvuja? Kweli huyu mama ni mwanamke jasiri!
 
Kama Tungefanya kama Mungu atakavyo basi tungekuwa mbali kuliko mchungji Dr lwakatare, Mungu anavitu vyakuwapa wanadamu,lakini watu wakuwapa wakowapi maana wengi wetu sio wema kwake, na Mungu ame mwahidi kila amtumikiae kuwa bopra zaidi kuliko watu wote waliopo duniani, hivyo basisihisi kamani dhambi mama huyo kubarikiwa.
Kutumia kiwanja chake ndiyo hasa Mungu hupenda, mungu hutumika na wale waliotiyari kutoa mali zao, kama unafikiri uongo to mali zako kwaajili ya MUngu kama hakukugusu na ukaona baraka zake.

Tatizo wengi wetu tunaishi nafikra zilizofungwa ndani ya mabox, tutkifikiri Mtu akiwa mtumishi wa Mungu basi awe maskini au mtu wa ibaada tu, tunasahau kuwa mtu huyu ambaye Mungu ndiye baba yake hasa anawezakumpa kituchochote ilimraditu anaweza kukimudu na kukitendea haki, elewa kuwa Wamutafutao Mungu ndio humuona.

Sina lengo la kumsaidi kutangaza utakatifu wake Dr, kwini MUNGU anamjua lakini sikubaliani na wazo lakuwa watu wa wanao mtafuta MUNGU wasimiliki mali kubwa kubwa kwa sababu tu weti ni watumishi ...halikubaliki.

Suala hapa si kwamba ukiwa mtumishi wa Mungu basi huwezi kuwa Mjasiriamali, NO! Simaanishi hivyo?

Tatizo Mh. Mch. Dr. anafichaficha mambo yake, ni vigumu kugundua (si kwamba haiwezekani) kwamba yeye ni mmiliki wa sasatel japo ukweli ndio huo? Je alishindwaje kujiunga na Tanzania Assemblies of God kipindi kila alipoomba wamruhusu ajiunge na Bunge na wakadai hawamtambui labda kama ndo anatuma application, mama wa watu akasepa!

Tamasha Women foundation kaandaa yeye japo anajiita mgeni maalum, totally blackmailing! Waheshimiwa kibao akiwemo Waziri Sophia Simba na Mbunge wa Busanda wamenunua ticketi maalum kwa Shs. laki 1 japo zinatangazwa kwa Sh elfu 10, 5 na kuendelea.

Hivi unakumbuka ule "MRADI" wake wa kusomesha watoto yatima walokuwa wanaishi pale Tabata Bima? Kwa sasa ngoma ilishtukiwa kwamba si yatima wala nini bt purely ujasiriamali!! Kuna Mangi mmoja alishutuka na kutaka kumlipua mama alipogundua mwanae yupo kwenye list ya yatima na analipiwa kila kitu na wafadhili, na huku mzazi nae ananchangia! You know what happened? Mama alimpoza Mangi kwa Mil. 15 ana amsomeshe mtoto bure bt jamaa akaamua amwamishe mwanae!

Habari ndio hiyo. IF YOU THINK YOU CAN HAVE FRESH MILK WHY KEEP A COW!
 
Nampa hongera sana huyu Mchungaji Lwakatare.
1) Kwanza ni mwanamke mchungaji, na kazi anayofanya kweli inaleta utukufu kwa Mungu.
2) Ni mjasiliamali, hivyo kaleta ajira nyingi tu kwa wanawake na kwa wanaume. Kaanzisha shule, radio station ile ya praise power, SASATEL na sasa anataka kuanzisha hiyo Foundation ya christian women. Vitu hivi vyote vinaleta maendeleo kwa taifa letu na ajira nyingi tu.
3) Hivi ni mbunge vile vile huyu mama, analitumika taifa lake pia.
Na tukumbuke, huyu mama ni binadamu, kama binadamu kila mtu ana mazuri na vile vile ana mapungufu yake. Aliye kamili ni Mungu peke yake.
Hivyo mimi nampa big up mama Lwakatare kwa kazi zake anavyofanya za kumtumikia Mungu na Taifa vile vile.

Hebu tuelezee ni kwa vipi kazi yake inaleta utukufu? Kuwatoza watu sadaka kwa kuwapangia viwango vya kutoa na special seats kwa tycoons in the church, kwamba kama huwezitoa laki1 then ukae backbench, au?

Hata Alex Massawe ni mjasiriamali na kaajili watanzania kibao karibu kila mkoa ana hotel, bt aliwahi kutajwa kwenye list ya majambazi!

Unataka tufumbe macho kisa ajira kwa watanzania?

Nashuru unakubali kwamba ana mapungufu pia and so being a Celebrity ndio maana tunamjadili!
 
"Sio wote wamwitao bwana bwana wataurithi uzima wa milele. "
"Kila mtu atalipwa kutokana na matendo yake."
"Huwezi kutumikia mabwana wawili, mungu na fedha"
 
[QUOTE=MjasiriamaliShupavu;537210]
Tatizo Mh. Mch. Dr. anafichaficha mambo yake, ni vigumu kugundua (si kwamba haiwezekani)

Mkuu ninamfahamu sana Mama Lwakatare pengine kuliko wote mnaoandika hapa! I can agree with you in many things including dishonesty conduct.

Ila hili la 'kufichaficha' mambo halijakaa sawa, hukutakiwa kuweka hapa.Maana sisi wote tunatakiwa tuwe open, ukianza na mama Lwakatare tutarudi katika jamii yetu ni kwa kiasi gani tuko wawazi kwenye mambo yetu?? maana isiwe tu kwa huyu?

Pili huwa napigana ana na ukweli wa dini zetu Tanzania na uamuzi wa kuzifuata! yaliyo ndani ya makanisa mengine ni hayo hayo mkuu!! labda hujui mengine yanatisha hutaamini.

Te best way unapotaka kumuanika mtu, tafuta ukweli, thibitisha reserach,mkuu kama hupo DSM nenda sikumoja kanisani kwake uone kama kweli kuna wa viti vya mbele na nyuma.

Tukishaanza kuhisihisi ndiyo tutakuwa watu wa kuhisihisi, mawazo yetu yatakuw siku zote ya hisiahisia, no facts, just living in rumors cloud.Hii inadumaza hata uwezo wa kufikiri.Katika wote mlioandika humu hamna facts! Then what makes you different from Shigongo? au hamuoni jamii yetu ni ya aina hii ya kupenda umbea na ndio maana Shigongo tajiri?

Is this our cultures to be open au inaanzia kwa huyu mama?
 
Tuache uzamani wapendwa....zamani ilikuwa mtu akiokoka basi kila mwenye kusema atasema kaamua kuwa masikini huyo...mara kakosa mwelekeo....mara amefilisika...n.k
leo watu kwa neema ya Mungu mwenyewe wameielewa Biblia kuwa mtu akiokoka anakuwa mfalme....sio wa kumouongoza mtu bali wa maisha yake mwenyewe....ndo sababu leo unaona mtu kaokoka na ana maisha mazuri sana...Mama Lwakatare ni mfano mzuri wa watu waliookoka....waliookoka ni watoto wa Mungu,vitu vyote huku duniani na mbinguni ni vya Mungu....sasa kwa nini watoto wake wasirithishwe vitu hivyo????....mimi ni mmoja wao kwa kweli life goes as am planning...Ukitaka kujua utamu wa ngoma ingia ucheze...
 
Point tupu! ni wajibu wetu sote kulea yatima yeye kafanya mpaka hapo alipofika wengine tumsaidie.
huyu mama hupitisha bakuli Marekani kwa jina la Yatima na wajane.yeye alipewa fungu na anapata pesa kwa jina la yatima. ni vyema awatumie.usifikiri alikuwa akijitolea hapana.
 

Mbona hukutaja asasi yake ya zamani ya Mission to the Needy aliyoitumia mwaka 1984 kupitishia pesa za wakimbizi wa Uganda, kuwadhurumu pesa zao, kula njama na mashushushu na hatimaye kuwaua hao beneficiaries baada ya siri kuvuja? Kweli huyu mama ni mwanamke jasiri!

wengi hawamjui huyu mama ni sawa na utukufu anaopewa bwana MENGI.lakini siku Rostam alipoeleza upande wa pili wa shilingi.Mengi hakurudi kujibu akaamua kuwatuma wafanyakazi wake.

Mama Rwakatare amekaa Marekani miaka nane akatengeneza NGO ya kusaidia Yatima na Wajane kupitia UKIMWI.HIZI PESA ni mali ya YATIMA NA WAJANE.

wako wengi wametumia njia ya UKIMWI mnakumbuka bilioni 49 zilizopotea kienyeji CRDB kwa jina la Mzee WETU MENGI?hadi sasa hakuna taarifa wala ripoti juu ya upotevu wa BILLION 49. karibu nusu ya pesa za watu wote wa Epa.

watu wanalia na KAGOBA iliyochukua BILIONI 40 huku wakisahau kuna BILIONI 49 hazijafanyiwa uchunguzi wowote hadi sasa.
 
Hapo ndio natoa sulute kwa wabongo, mtu ameanzisha thread haina data kamili lakini wachangiaji wa kwanza lazima wawe negative bila hata kufikiria. Siwezi shangaa mpingaji saa nyingine hajatoa hata ajira ya house girl home achilia mbali kuwa na watu zaidi ya kumi unawalipa mshahara.

Huyo mama ni mtu wa kupigiwa mfano, kuanzisha biashara na ikasimama bongo kwa zaidi ya miaka 10 unahitaji salute. Kama kurudisha yatima home inawezekana ikawa kwa good reason, manake wafanyakazi wanazalisha na wanarudishwa home itakuwa NGO inayohitaji pesa kutoka kwa wafadhili ambao hivi sasa wanamatatizo ya kiuchumi kwao na hawawezi kutusaidia kama walivyofanya kipindi kilichopita.

Labda mjadala ungehusu namna ya kuwasaidia yatima kama watarudi au Mch. aendelee kukaa nao kwa utaratibu upi, manake wabongo utamaduni wa kusaidia yatima bado ni tatizo, manake mtu anakuwa yatima kwa kufiwa na baba na mama, sasa mjomba, shangazi, jamaa, jirani, wanaukoo, kabira moja, dini, babu au bibi si wapo jamani.

Kupiga soga kila kukicha hakuwezi kulipa bili, mwisho wa siku lazima chakula, maji umeme n.k vilipwe.

Salute Mama Lwakatare kama umeshindwa, wengine waendelee pale ulipofikia. Hii haizuii mapungufu katika utekelezaji.


TATIZO NI PALE UNAPOLETEWA PESA TOKA NJE NA WAFADHILI KUWA UNAWASAIDIA YATIMA.

Ukishazipata unaanza kuwasaidia kwa miaka kadhaa wakisha kuamini na hawakufanyii tena AUDIT unaanza kuwatelekeza na kunufaika kwa kutumia migongo yao.
 
wengi hawamjui huyu mama ni sawa na utukufu anaopewa bwana MENGI.lakini siku Rostam alipoeleza upande wa pili wa shilingi.Mengi hakurudi kujibu akaamua kuwatuma wafanyakazi wake.

Mama Rwakatare amekaa Marekani miaka nane akatengeneza NGO ya kusaidia Yatima na Wajane kupitia UKIMWI.HIZI PESA ni mali ya YATIMA NA WAJANE.

wako wengi wametumia njia ya UKIMWI mnakumbuka bilioni 49 zilizopotea kienyeji CRDB kwa jina la Mzee WETU MENGI?hadi sasa hakuna taarifa wala ripoti juu ya upotevu wa BILLION 49. karibu nusu ya pesa za watu wote wa Epa.

watu wanalia na KAGOBA iliyochukua BILIONI 40 huku wakisahau kuna BILIONI 49 hazijafanyiwa uchunguzi wowote hadi sasa.



Taarifa hizi ninazo tangu last year ...wakati zikiwa fununu miongoni mwa watendaji wake ....sikuamini kama angetekeleza...hasa ukizingatia wamarekani wanaofadhili kituo hichi walikuwa wametembelea kituo hiki wakati wa moja ya ziara zilizoratibiwa na ubalozi wao......nilitegemea kituo ndio kingeendelea kunawiri,labda kama wafadhili wake watakuwa wamepewa negative informations...

lakini kwa upande mwingine tujuwe yatima ni wetu sote...pamoja na utajiri wa huyu mama na kuamini kuwa ana uwezo wa kutunza hata yatima 2,000 waliokuwa pale kwa pesa yake mwenyewe...tuna jukumu la kuchangia.Na kwa kituo cha mama kilishajulikana ...kosa kubwa alilofanya ni kutotokea hadharani kusema kuwa gharama za uendeshaji zinamzidi kimo...ili kuwakaribisha makampuni,taasisi, na watu binafsi kuchangia ....ikumbukwe kuwa hata jakaya ..rais ....anafahamu kituo kile na watu wengi walikuwa wanakitembelea., ni wazi lazima mama aje hadharani kutoa tamko ...la kuelemewa kwake na kutoa mwito wa misaada zaidi ...si lazima wazungu hata sisi tunaweza kusaidia kidogo tulichonacho!!

Iwapo itaonekana kuwa kuna haja ya kukifunga kituo moja kwa moja ...namshauri asifanye ghafla...bali uwe kama mkakati wa miaka mitano..utakaolenga kwa kuanzia kuacha kuchukua watoto wapya.....na kulenga zaidi kuwasaidia wale waliopo kituoni walio primary wamalize ....walio sekondari wamalize ..na badaye watabaki wachache watachanganywa na watoto wa shule zake nyingine.Ni dhahiri ni pigo kwa mtoto ukimzowesha life style mpya halafu ukamkatisha ghafla.....tena wengi wao hawana hata hizo familia za kurudishwa kwao!
 
Thred ya kwanza ilikuwa kutafuta mawazo na utafiti ili kupata usahihi na akauliza MWENYE KUJUA ZAIDI AMFAHAMISHE, sasa mbona tunaleta mengine, ...wengi mmepoteza hoja, yeye aliuliza kama habari ni kweli, tuanze kwa kujibu hilo halafu tuchangie positively sio kulaumu tu.
Mkuu Modereta, si kweli kwamba alikuwa anatafuta ukweli wa habari. Yeye alileta taarifa humu na akataka habari zaidi. Kama hujaona vizuri, hebu pitia tena hapa:
Mwanahabari said:
Naomba kama kuna mtu ana habari zaidi aweze kunisaidia, maana huyu mchungaji there is something fishy going on, na kuchezea maisha ya yatima is something serious, so i am interested kama kweli ni mtu wa kusaidia watu au ana badilisha miradi tu at the expense of the disadvantaged people.
 
where is god? no one knows.lakini nina uhakika kanisani kwa mama Lwakatare "there is no god in there"Imani ni mabo ambayo yanaweza yakamfanya Professor wa taaluma yoyote akawa mpumbavu zaidi ya mtu mwenye mtindio wa ubongo.usidanganyike na aina ya watu wanaosali kwa mama Lwakatare au elimu zao.imani ni habari nyingine kabisa.
huyu mama sio mwema katika matendo yake na mienendo yake(subiri nikusanye ushahidi nitauwasilisha)
afterall JeSUS CHRIST told us"kama unataka kunifuata mimi,basi nenda kauze mali zako kisha uwagawie masikini,then follow me" tunatakiwa tujikane kwanza kabla hatujamkubali yeye.hivyo ndivyo maandiko yanavyosema.
Sasa nenda kwa mama Lwakatare uone kinyume,anahubiri zaidi kuhusu mafanikio ya kidunia na kusahau kazi ya kanisa ni kuokoa roho za watu na kumuandaa mwanadamu kuupokea ufalme wa mbinguni,Hebu ngoja nimnukuu baadhi ya matamshi yake anayopenda kutoa"kama unataka kupandishwa cheo kazini,kama unataka upewew safari za ulaya kazini kwako,kama unataka mafanikio katika miradi yako,kama unataka...... basi njo mikocheni B assemblies of god"
Tunajua matangazo kama hayo utayakuta kwa waganga wa tiba za jadi na si kwenye nyumba ya ibada ambayo waumini wanatakiwa kundaliwa kuupokea ufalmw wa bwana.
HEAVEN IS OPEN TO THOSE WHO ARE DRIVEN BY THEIR BRAINS AND NOT THEIR FAITH
 
jamani huyu lwakatare si mtu mzuri kitambo tu yaani, ni kwa vile watanzania hawapendi tu kufuatilia mambo yas watu, kule kwenye mashule yake kuna vituko kweli yaani, ukiyasikia unaweza hama nchi, huyu mama ni noma kwa mambo ya ishirikina, mara nyingi sana wanafunzi hukuta kuku amechinjwa bustanini maeneo yua shule, kuna rafiki yangu alikuwa anasoma huko aliishawahi kuniambia kuwa kila walipokuwa wanakaribia kufanya mitihani walikuwa wanaona vitu vya ajabu sana, kama vichwa vya kuku waliochinjwa na kuchimbiwa chini, damu kuzagaa ovyo maeneo ya viungo vya shule, na mambo mengine ya ajabu ajabu na ya kishirikina kama hayo.
mi hawa wachungaji siwaelewi kabisa yaani. wako kimasilahi sana hakuna cha kuhubiri wala kuinjilisha, zaidi ya yote wanataka utajiri tu hawana lolote, ndo maana hata mahubiri yao ni juu ya utajiri na kupigana vijembe na majungu.
hii ni hatari wandugu.
 
I think watu mna miss point, Orphans ndiyo wanatunzwa na Taifa Lote, lakini kuwarudisha tu kwao kisa unataka kuanzisha University, I am concerned with that notion. I have confirmed this story already na baadhi wanaorudi hawana ndugu huko kwao, dont think sihusiki na kulea yatima, ila ukiwatreat kama comodities tu kuendeleza miradi yako, dont do it in the first place (you cant downsize orphans!!)...these are fragile people especially the sick ones that need more care than others....


Labda namimi nichangie kidogo - nimesoma threads zote - naona tumetoka kwenye YATIMA na TUMEINGIA kwenye HUKUMU, KASHFA ETC. Ukweli ni kuwa WOTE tutasimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya matendo, maneno, mawazo yetu. Lakini KITENDO CHA KUANZA KUSAIDIA YATIMA, NA KUWAACHA TENA NI KITENDO CHA KIKATILI SANA
1) Unapoamua kufanya jambo - fanya planning, jipange vizuri ili ulifikishe mwisho - Mungu sio Mungu wa KIGEUGEU - AKIAMUA JAMBO ANAFANYA HADI MWISHO - so mtu wa Mungu inabidi uwe na tabia ya Mungu
2) YATIMA ni wanadamu - they have feelings too - KITENDO CHA KUWA UMIZA MIOYO YAO KIASI HIKI KINA MATOKEO MABAYA SANA KWA YOYOTE ANAYEFANYA HIVYO - MACHOZI YAO YATAMFIKIA ALIYEWAUMBA NA ITAKUWA LAANA

Haijalishi anayewafanyia yatima hivyo ni mchungaji, sheikh, mtu binafsi au la..... unapoamua KUMHURUMIA MTU - FANYA KWA MOYO - OTHERWSIE THAWABU YAKO MBELE ZA MUNGU INAPOTEA - NA YOTE ULIYOFANYA NI HASARA TU -

Mimi ninaye yatima mmoja namlea - namsomesha etc. laiti kila mtanzania anayejiweza angemchukua mmoja - akawa naye kama mwanae, akamlea, kumsomesha etc. basi kiasi tungepunguza - na wale wanaoweza wakachukua hata wawili -
SHIDA WATANZANIA WENGI WAKO BUSY KUJENGA MAJUMBA, KUNUNUA MAJUMBA YA KIFAHARI, KUISHI MAISHA YA ULEVI, ULAFI, - WAKIDHANIA MUNGU HAWAONI - TUNAPIGA VITA MAFISADI ILA MUNGU ANAPOTUANGALIA JINSI TUNAVYOWAACHA YATIMA WANAHANGAIKA - ANATUONA WOTE NI MAFISADI - LETS DO SOMETHING ABOUT IT - WE TAKE A STEP
 
YATIMA si ni kwamba mtu asiye na walezi au sivyo?Sasa anawarudisha kwao kukaa na nani? mbona sielewi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom