Mchungaji Lusekelo: Libya na Iraq zinajuta kuwasaliti viongozi wao Gaddafi na Sadam Hussein, watanzania msifanye makosa mtajuta!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,867
141,804
Mchungaji Anthony Lusekelo amewataka Watanzania kutoiga iga mambo kwani demokrasia ina maana pana.

Mzee wa Upako amesema hata Marekani demokrasia wanayoihubiri hawaiishi kwa mfano Hilarry Clinton ndiye aliyeshinda kwa wingi wa kura lakini aliyeteuliwa kuwa Rais ni Donald Trump.

Kadhalika Uingereza Waziri Mkuu anapigiwa kura lakini mfalme ndiye anayempitisha.

Lusekelo amewataka Watanzania wajifunze Libya na Iraq waliotupa " mbachao" kwa msala upitao na sasa wanajuta.

Chanzo: Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
 
Muulize huyo mtu wako

Anajua mfumo wa kura za Marekani ukoje?

Muulize pia ni Uingereza gani Waziri mkuu anapitishwa na Mfalme?

Mwisho muulize tutajuta nini??? Kwa hiyo yeye anamfananisha Magufuli na Saddam Hussein??? Anazijua sifa za Saddam Hussein??? Je anamfananisha Magufuli na Gaddafi? Anazijua sifa za Gaddafi??? Ametumia vigezo gani kumfananisha Magufuli na hawa? Au amekaririshwa tu??
 
ZWAZWA jingine hilo nalo limeamua kusikika. MAZWAZWA haya yalikuwa kimya kabisa kuhusu maovu mbali mbali ya KICHAA ikiwemo bomoa bomoa, 2.7 trillions iliyokwapuliwa hazina, kutekwa kuteswa na hata kupotezwa kwa wasiojulikana, shambulizi la lissu, maiti kwenye viroba ufukweni, ubambikiaji kesi, sheria eti asishtakiwe kwa maovu yake na madudu mengine chungu nzima.
 
Back
Top Bottom