Mchungaji Lusekelo anawaponda Mitume na Manabii feki Channel 10

Mmh kama ni hivyo, basi watumishi Tanzania ni akina nani?maana hao ndo waliopo na wote ni wezi. Huko Mwanza yupo malisa anatikisa wanasema nabii wa uongo, huko arusha yupo geordavie wanasema wa uongo mwizi, sasa tunamtaka nani? Au mwashamu baba askofu?

Maana yake hatuna nabiii wa ukweli
 
Nakutaka kushuhudia miujiza,baadhi ya Wakristo wa sasa wanaona sehemu alipo Kristo ni pale ambapo amekuja mtu na magongo akaondoka bila magongo,anakuja mtu goi goi anaondoka yupo strong bila kutambua ni wasanii,hata Kenya hapo ilkuja story humu mwanamke alikuwa analipwa aka-act kama mlemavu ibada ikiisha analipwa(na bado mchungaji msanii hakumlipa akamdhulumia mbali,na alikuwa anazini nae) but watu hawafunguki akili,nilichogundua hawa wakujiita sijui maaskofu na manabii wanacheza na akili za watu wavivu kusoma Biblia,so akisoma mstari ktk Bible akaufafanua vizuri basi mtu asiesoma Bible anaona ni nabii kumbe yeye mwenyewe angetulia akaisoma Bible angepata kile kile alichofafanuliwa na pia angetuliza akili angepata zaidi ya kile coz kwanza angesoma neno zima na kutafakari neno lote kwa wakati mmoja tofauti na wachungaji wao huchukua mstari mmoja na kuufafanua nusu saa nzima na kuwahimiza "sema amen,sema amen" kumbe anawaibia.

Kwenye kazi ya Mungu kuna ngano na magugu na Yesu mwenyewe alisema acheni vyote viote pamoja lakini utaweza kutofautisha ngano na magugu wakati wa kuvuna.Shetani ameingia sana katika kuvuruga kazi ya injili ionekane kama utapeli kwa kupandikiza magugu katika shamba la ngano na hiyo inakufanya uone wokovu na watumishi wote wanaohubiri wokovu kama wasanii! Kwako au kwenu Kanisa sahihi ni Roman Catholic na labda Lutheran na haya mengine ni usanii! Nakuhakikishia umepotoka na ninakushauri ujikite katika kusoma Biblia ili Roho Mtakatifu akufundishe kweli yote na utaelewa mambo mengi usiyoyajua! Si vyema kukimbilia kukosoa ukiwa huna authority ya kufanya hivyo.Mambo ya Mungu siyo mambo ya Simba na Yanga au Manchester na Arsenal ambayo kila mtu anaweza kutoa opinion yake.
 
na mimi ngoja nikuulize. kazi ya nabii nini?

Nabii mara nyingi huongea nia na mpango wa Mungu kwa wakati uliopo, kutahadharisha au kuonya. Anaweza kuongea kwa kundi au mtu mmoja. Katika agano jipya manabii wanatakiwa kusema wawili au watatu kwa habari kudhibitika lakini wakristo lazima wapambanue roho kwa neno kama ni ya Mungu au shetani au binadamu tu. Kama nabii ataongelea jambo lako binafsi litakuwa jambo unalojua sirini mwako au ambalo Mungu alikuonyesha hukuliamini sasa anakudhibitishia. Kwa mfano "Mungu ananionyesha unapigwa risasi lakini ukimrudia utapona" wakati huo wewe umejiunga kundi la ujambazi basi ni rahisi sana kuelewa hata usipojibu neno kwake.
 
Dah huyu jamaa noma, anasema anashangaa watu kujiita mitume wakati hawana hata sifa moja. Mfano anasema Nabii huwa Hana makazi ya kudumu sasa inakuaje Nabii anakuwa na makao Makuu??

Sasa anasema wenzake hawafai?
 
kwani tanzania tuna mitume makubwa

Waefeso 4:10 Basi,
huyo aliyeshuka hapa duniani, ndiye aliyepaa juu ya mbingu zote
apate kuujaza ulimwengu. 11 Ndiye aliyewapa watu zawadi:
wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe
wainjilisti , wengine wachungaji na walimu. 12 Alifanya
hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya
huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo, 13 na hivyo sote
tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu
waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.
 
Kwenye kazi ya Mungu kuna ngano na magugu na Yesu mwenyewe alisema acheni vyote viote pamoja lakini utaweza kutofautisha ngano na magugu wakati wa kuvuna.Shetani ameingia sana katika kuvuruga kazi ya injili ionekane kama utapeli kwa kupandikiza magugu katika shamba la ngano na hiyo inakufanya uone wokovu na watumishi wote wanaohubiri wokovu kama wasanii! Kwako au kwenu Kanisa sahihi ni Roman Catholic na labda Lutheran na haya mengine ni usanii! Nakuhakikishia umepotoka na ninakushauri ujikite katika kusoma Biblia ili Roho Mtakatifu akufundishe kweli yote na utaelewa mambo mengi usiyoyajua! Si vyema kukimbilia kukosoa ukiwa huna authority ya kufanya hivyo.Mambo ya Mungu siyo mambo ya Simba na Yanga au Manchester na Arsenal ambayo kila mtu anaweza kutoa opinion yake.

Duh mkuu wakatoliki mtateswa sana na mapepo maana kwa hizo ibada zenu za kukalili ambazo unaingia ibadani na mizigo yako kama magonjwa,mapepo na vifungo na unatoka nayo ni ngumu sana na ndo maana nyie kwenu pombe ni ruksa lakni kwetu sisi walokole ndugu huwezi ingia na mapepo yako ukaondoka nayo maana huyo pepo mwnyew atajuta lakn kwa nyie roman endeleeni tu na ibada zenu za kukalili
 
Dah huyu jamaa noma, anasema anashangaa watu kujiita mitume wakati hawana hata sifa moja. Mfano anasema Nabii huwa Hana makazi ya kudumu sasa inakuaje Nabii anakuwa na makao Makuu??

kwani hata yeye mbona feki?
 
Nabii mara nyingi huongea nia na mpango wa Mungu kwa wakati uliopo, kutahadharisha au kuonya. Anaweza kuongea kwa kundi au mtu mmoja. Katika agano jipya manabii wanatakiwa kusema wawili au watatu kwa habari kudhibitika lakini wakristo lazima wapambanue roho kwa neno kama ni ya Mungu au shetani au binadamu tu. Kama nabii ataongelea jambo lako binafsi litakuwa jambo unalojua sirini mwako au ambalo Mungu alikuonyesha hukuliamini sasa anakudhibitishia. Kwa mfano "Mungu ananionyesha unapigwa risasi lakini ukimrudia utapona" wakati huo wewe umejiunga kundi la ujambazi basi ni rahisi sana kuelewa hata usipojibu neno kwake.

.. ...mmmh!...aiseeeh!
 
Waefeso 4:10 Basi,
huyo aliyeshuka hapa duniani, ndiye aliyepaa juu ya mbingu zote
apate kuujaza ulimwengu. 11 Ndiye aliyewapa watu zawadi:
wengine aliwajalia wawe mitume, wengine manabii, wengine wawe
wainjilisti , wengine wachungaji na walimu. 12 Alifanya
hivyo apate kuwatayarisha watu wote wa Mungu kwa ajili ya kazi ya
huduma ya Kikristo ili kuujenga mwili wa Kristo, 13 na hivyo sote
tuufikie umoja wa imani na kumjua Mwana wa Mungu; tuwe watu
waliokomaa na kuufikia utimilifu wake Kristo mwenyewe.

Wagalatia nomaa!
 
Dah huyu jamaa noma, anasema anashangaa watu kujiita mitume wakati hawana hata sifa moja. Mfano anasema Nabii huwa Hana makazi ya kudumu sasa inakuaje Nabii anakuwa na makao Makuu??
Naunga mkono hayo mahubiri hata kama sijayasikia au kuyaona, huduma ya kinabii imeshakoma zamani kama uumbaji wa mbingu na nchi ulivyokoma, sasa hawa wanaojiita manabii sidhani kama ni manabii hao wa uongo au ni wa Mungu yupi?
 
Huo unaouendesha ni ubishi wa vijiweni usiokuwa na reference. Nimekupa waefeso 4:10 na ni agano jipya, huduma tano zinatajwa pamoja, kwa hiyo kama manabii hawapo basi hata wakati wa wachungaji umepita pia. Naona kwako zimebaki karama za kipadirisho. Toka nimesoma sijawahi kuona mahali panaposema Yesu alitoa karama za upadre na ufather, ukadinali, upapa! Kama unajua vilipoandikwa katika biblia nionyeshe, nitaanza kuviamini . Hizi mnazipokea kama mapokeo ya kanisa bila kujiuliza, lakini vilivyoandikwa mnavipinga.
 
Kuthibitisha wehu wa huyu ndugu nimemuona baa iitwayo "Soccer City" Sinza akielezea namna ya eti "kumgonga housegirl kwa kutumia alama ya f**k kwa kutumia mkono. Hovyo kabisa nimemfukuza baada ya kuona watu wanamzunguka wakitaka arudie kipengele cha" kumlamba " housegirl" likawa linarudiarudia tu kama zuzu
 
Thibitisha wizi wake au ndo wivu wa kukimbiwa na waumini wenu?
kweli umepotea ndugu yangu unazungumzia wivu wa kukimbiwa thehebu????????????????????badala uone wivu wa wenzako kuingia mbinguni???hawa wachungaj wanawapeleka direct kwa lucifer....................muamini mungu tu utaokoka sio wachungaji
 
Haya ni maneno aliyoyasema Mungu baada ya kuweka unabii mdomoni mwa Yeremia:

"Nabii huenda kule ambako Mungu anamtuma"

KWamba nabii hawi na HQ hiyo mimi sijui labda Lusekelo mwenyewe binafsi kaambiwa na Roho wa Mungu.

Yeremia1:4-10

Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.
7 Lakini
Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.
8 Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana.
9 Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;
10 angalia, nimekuweka leo juu ya
mataifa na juu ya falme,ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.

Mataifa na Falme si lazima ziwe nchi za mbali.

Mataifa= watu wasiomjua Mungu.
Falme=i Mamlaka mbali mbali zilizo kinyume na Mungu
Ndugu najua inania njema ya kuelimisha watu khs manabii lakini naomba unisaidie swali hili...UNAWEZA KUNITAJIA JAPO NABII MMOJA AU MTUME KUTOKA KWENYE BIBLIA AMBAYE ALIKUWA NI TAJIRI?
PILI...MANABII NA MITUME WENGI WA KWENYE BIBLIA WALIHUBIRI WAKIKEMEA SANA DHAMBI LAKINI KWANIN MANABII NA MITUME WENGI WA LEO HAWAKEMEI DHAMBI BALI MKAZO WAO HUWA JUU YA MAFANIKIO YA KIMWILI
 
Ibrahim ambaye ni Baba wa Imani hakuwa tu Tajiri alikuwa na serikali kabisa.
Kulikuwa na Lundo la watu chini yake waliogawanywa kufuatana na kazi zao.
Hakuwa na Magari au ndege lakini alikuwa Tajiri.

Daniel alikuwa na cheo kikubwa sana serikalini huko Babeli na alikuwa mshauri mkuu wa Mfalme.
Hakuwa LOFA.

Kuhusu wanacho hubiri hiyo ni kati yao na Mungu.
Mitume huambiwa cha kusema na Mungu mwenyewe.
Mungu huwatuma mitume kwa wakati nau huwapa ujumbe kuhusu wakati ule.
Zamani zile mitume waliwaambia watu watabarikiwa mijiniMashambani na katika uzao wa wanyama wao.
Pia zitabarikiwa kazi za mikono yao.
Leo ukiambiwa Utabarikiwa kazini kwako na katika Biashara yako tofauti yake ni nini?
Kifupi mitume hupewa ujumbe wa wakati ule waliotumwa.

Back
Top Bottom