Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama aliomba radhi Jeshi la Polisi, asema alihadaiwa kuhusu Muuza Chips aliyekutwa amefariki dunia

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,608
141,429
Mchungaji Kimaro ameliomba radhi jeshi la polisi baada ya kutoa taarifa zisizo sahihi kufuatia kifo cha muimba kwaya wa Kanisa hilo.

Kimaro amesema muimba kwaya huyo aitwaye Yusuph aliyekuwa anauza chips pale makumbusho alimdanganya kuwa alitekwa lakini polisi wamebaini kuwa Yusuph hakuwai kutekwa.

Yusuph alikutwa akiwa amekufa siku moja kabla ya Krismas na iliaminika kuwa watekaji ndio walirudi kumuua baada ya kumteka na kumuachia.

Mchungaji Kimaro amesema Yusuph alikuwa ni kijana wake aliyekuwa anamlea kiroho na imebainika kuwa kifo chake kimetokana na msongo wa mawazo baada ya kuwa na madeni makubwa yanayozidi tsh milioni saba.

Mchungaji Kimaro amewataka vijana kuacha tabia ya kuwadanganya wachungaji pindi wanapokuwa na changamoto mbalimbali kwani mshahara wa dhambi ni mauti.

Mchungaji ameliomba radhi Kanisa kwa kutoa maeleza yasiyo sahihi mbele ya madhabahu kuhusiana na kutekwa nyara kwa mwimba kwaya ya Uamsho rip Yusuph.

Maendeleo hayana vyama!

===
Ilivyokuwa

Wakati mwili wa Yusuf Deus (26) ukitarajiwa kusafirishwa leo kwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya maziko, Jeshi la Polisi limesema bado linaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.

Kauli hiyo ya polisi imekuja ikiwa tayari familia na Mchungaji wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama, Eliona Kimaro wakielezea sintofahamu ya tukio hilo.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kujua tukio hilo huku akibainisha kuwa uchunguzi bado unaendelea.

“Tunaendelea na uchunguzi wa tukio hili na pindi utakapokamilika tutakuwa na la kusema kwa vyombo vya habari,” alisema Mambosasa.

Yusuf alikutwa amepoteza maisha Jumatatu alfajiri katika eneo analofanyia biashara ya kuuza chips karibu na makao makuu ya Tigo Kijitonyama jijini hapa.

Mwili wa marehemu unasafirishwa leo kwenda wilaya ya Kishapu Kijiji cha Mipa, tofauti na walivyokuwa wametarajia.

“Tulishindwa kuondoka jana (juzi) kwa sababu ya ratiba hii ya ibada iliyopangwa kufanyika kesho (leo) katika kanisa alilokuwa akiabudu (KKKT Usharika wa Kijitonyama) ambayo imepangwa kufanyika kuanzia saa 7 mchana,” alisema Kija.

Kuhusu majibu ya uchunguzi alisema bado hayajatoka huku akibainisha kuwa hayawazuii kufanya maziko huku akisema endapo yataonyesha alitendewa kama familia itafuatilia kwa ukaribu.

“Tutafuatilia ili kujua nani aliyefanya ili hatua zaidi zichukuliwe juu yake,” alisema.

Yusuf akiacha mke na watoto wawili atakumbukwa kama muumini aliyekuwa akijitoa kwa kanisa, mcheshi, anayependa watu wanaomzunguka bila kubagua.

Kupitia video ambayo ilielezea tukio la kifo chake iliyotumwa kwenye mitandao ya jamii, Mchungaji Kimaro alionekana akieleza tukio hilo kuwa kabla ya kifo chake, kijana huyo aliyekuwa mwimbaji wa kwaya kanisani kwake aliwahi kutekwa na watu wasiojulikana tangu Desemba 2 hadi 8 mwaka huu.

Mchungaji Kimaro alieleza kwenye video hiyo kuwa walimtafuta Yussuf baada ya kutekwa na walipomkosa waliripoti polisi.

“Alikuwa amechukua Sh1.7 milioni kwenda kulipa mayai na bidhaa nyingine. Walikuja watu wakamteka na kumtupia kwenye gari na kuondoka naye.”

Alisema walimpeleka porini ambako pia hakujui na walikuwa wakibishana ama wamuue na wengine wakipinga.

Hata hivyo, mmoja wa watekaji hao alipinga wazo la kumuua akisema aliyewatuma hajawalipa na kuamua kuchukua zile Sh1.7 milioni walizomkuta nazo kisha wakamrudisha na kumtupa maeneo ya Sayansi baada ya wiki.

Baada ya kuokotwa, kijana huyo alirejea nyumbani na walikutana na alimwelezea mchungaji yaliyomkuta na alimsaidia kuendelea na shughuli zake.

Mchungaji alisema Desemba 20 alimkabidhi Sh1.5 milioni ili arejee kwenye biashara yake ya chipsi. Lakini baada ya siku kadhaa kijana huyo akakutwa amejinyonga kwenye banda lake.
 
Mchungaji akasema Dogo alikuwa anauza chips mpaka za 2M kwa siku! mimi nilianza hisi kuna walakini na shuhuda hile...inaonekana Dogo alikuwa na biashara nyingine,ukizingatia na idadi ya wapiga debe jirani na banda lake la Chips Kuku.some thing went wrong,kama vile Kwenye Movie ya Friday.Smokey alikoswa koswa Kupigwa Risasi na Big Worm baada ya kudedicate Business Terms tofauti na walizokubaliana na Big Worm kabla
 
Mi nilihisi hata mchungaji anaongea uwongo ili kuvuta watu kanisani.

Mi kilichonishangaza mwonekano wa kupata 2M per day na jinsi alivyo mwenye kupata hizo hela....alikuwa choka mbaya....lkn pia nilishangaa sana mtu utekwe wiki moja, halafu urudishwe kisha utembee mtaani saa 4 za usiku kifua mbele peke ako.....eti unafata luku....nyokoooo 2M ukashindwa kuwa na hata buku 5 kwenye simu? Ilinishangaza sana kutembea bila tahadhari....nikamshangaa na mchungaji na wazee wa kanisa.
 
mchungaji akasema Dogo alikuwa anauza chips mpaka za 2M kwa siku! mimi nilianza hisi kuna walakini na shuhuda hile...inaonekana Dogo alikuwa na biashara nyingine,ukizingatia na idadi ya wapiga debe jirani na banda lake la Chips Kuku.some thing went wrong,kama vile Kwenye Movie ya Friday.Smokey alikoswa koswa Kupigwa Risasi na Big Worm baada ya kudedicate Business Terms tofauti na walizokubaliana na Big Worm kabla
Shikamoo broo.
 
Back
Top Bottom