Mchungaji: JK futa chaguzi zote ilizotawaliwa na rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji: JK futa chaguzi zote ilizotawaliwa na rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtwana, Oct 24, 2012.

 1. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanganyika limemshauri Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete kutoa tamko la kufuta chaguzi zote zizogubikwa na rushwa ndani ya chama hicho ili kurejesha heshima kwa chama na serikali iliyopo madarakani.

  Tamko hilo limetolewa na Mchungaji wa kanisa hilo, William Mwamalanga, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kufuatia kauli ya Rais Kikwete kwamba vitendo vya rushwa vinavyojitoleza katika chaguzi za CCM vitakitumbukiza chama hicho kwenye shimo.

  Mwamalanga alisema rushwa ndani ya CCM imekifanya chama hicho kukosa mwelekeo hivyo kinachotakiwa ni kwa Rais Kikwete kuchukua hatua ya kufuta matokeo yote ya viongozi waliochaguliwa kwa rushwa ili kurejesha heshima na imani kwa wananchi kwa chama hicho.

  “Rushwa ndani ya CCM imekuwa zaidi ya malaria, imekuwa zaidi ya ukimwi, kwa msingi huo kauli ya Rais kukemea rushwa haitoshi,maana tatizo hili ndani ya CCM limebaki kama ngoma isiyokuwa na wachezaji,” alisema Mwamalanga.

  Alisema CCM ndiyo chama tawala, hivyo Watanzania walitegema kuona kinakuwa chama cha mfano kupambana na rushwa badala yake kimekuwa kiongozi wa rushwa hali ambayo inazorotesha upatikanaji wa maendeleo nchini.

  Mwamalanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kurugenzi ya Kueneza Amani kwa Jamii na dini zote nchini kama tatizo la rushwa litaachwa liendelee kushamiri ndani ya chama hicho kikongwe, itakuwa vigumu kukemea vyama vingine vya siasa iwapo vitachukua madaraka ya nchi.

  Alisema CCM ambayo ilitokana na Tanu ilijiwekea misingi mizuri ya kukataa rushwa, lakini hivi sasa kimekuwa chama kinachoongoza kwa rushwa.

  Kuhusu tatizo la kuchomwa kwa makanisa, alisema serikali inapaswa kuchunguza kwa umakini suala hilo kubaini chanzo na kwamba makanisa yote yaliyochomwa yajengwe kwa gharama za serikali.

  Rais Kikwete akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), alitoa onyo kwamba vitendo vya rushwa vinavyojitokeza katika chaguzi za ndani za CCM visipodhibitiwa, vitakitumbukiza chama hicho kwenye shimo.

  Malalamiko ya rushwa ndani ya chaguzi za CCM yametolewa na baadhi ya wagombea wa uenyekiti wa mikoa. Waliolalamika ni Clement Mabina (Mwanza), John Guninita (Dar es Salaam), Thomas Ngawaiya (Kilimanjaro), Makongoro Nyerere (Mara) na William Kusila (Dodoma).


  Kwa muono wangu hana ubavu wa kufanya hivyo mana.................................
   
 2. r

  raymg JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu Mchungaji naye bhana, lini JK akafanya kaz hiyo! Yeye n kulalamika tu bs
   
 3. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama kuna mtu anayeweza kututumia huu wimbo mpya wa Mrisho Mpoto wa CHOCHEA KUNI MBICHI, atuwekee tafadhali. Sehemu inayonifurahisha zaidi ni ile anaposema, UKIONA MTU MZIMA ANAMWELEZA MTU MZIMA MWENZIE MAMBO YA KITOTO, UJUE KUNA TATIZO. Nadhani ni Ujumbe mahususi kwa JK, pamoja na yote ya kuupaka wanja Udini nao sasa Uhamsho na akina Sheikh Ponda wameamua sasa kumpaka Pilipili halafu yeye ndiye anayezinga kwenye Kombolela!
   
 4. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  thubutuuuu!
   
 5. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,476
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA

  Hakuna ushauri wowote utakaoutoa kwa ccm kwa lengo la kukiimarisha chama hicho wakausikiliza na kuuzingatia. kwa sababu kinahitaji kufa.

  Cha kufanyi ni sisi watanzania wote Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa na CHADEMA (M4C).

  Hakika Tanzania mpya itazaliwa 2015.
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Kukataza rushwa ndani ya ccm kutasababisha kupotea kwa chama hiki ktk siasa.
  Ccm bila rushwa haiwezekani.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 7. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  M
  Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanzania limemshauri Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete kutoa tamko la kufuta chaguzi zote zizogubikwa na rushwa ndani ya chama hicho ili kurejesha heshima kwa chama na serikali iliyopo madarakani.

  Tamko hilo limetolewa na Mchungaji wa kanisa hilo, William Mwamalanga, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kufuatia kauli ya Rais Kikwete kwamba vitendo vya rushwa vinavyojitoleza katika chaguzi za CCM vitakitumbukiza chama hicho kwenye shimo.

  Mwamalanga alisema rushwa ndani ya CCM imekifanya chama hicho kukosa mwelekeo hivyo kinachotakiwa ni kwa Rais Kikwete kuchukua hatua ya kufuta matokeo yote ya viongozi waliochaguliwa kwa rushwa ili kurejesha heshima na imani kwa wananchi kwa chama hicho.

  “Rushwa ndani ya CCM imekuwa zaidi ya malaria, imekuwa zaidi ya ukimwi, kwa msingi huo kauli ya Rais kukemea rushwa haitoshi,maana tatizo hili ndani ya CCM limebaki kama ngoma isiyokuwa na wachezaji,” alisema Mwamalanga.

  Alisema CCM ndiyo chama tawala, hivyo Watanzania walitegema kuona kinakuwa chama cha mfano kupambana na rushwa badala yake kimekuwa kiongozi wa rushwa hali ambayo inazorotesha upatikanaji wa maendeleo nchini.

  Mwamalanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kurugenzi ya Kueneza Amani kwa Jamii na dini zote nchini kama tatizo la rushwa litaachwa liendelee kushamiri ndani ya chama hicho kikongwe, itakuwa vigumu kukemea vyama vingine vya siasa iwapo vitachukua madaraka ya nchi.

  Alisema CCM ambayo ilitokana na Tanu ilijiwekea misingi mizuri ya kukataa rushwa, lakini hivi sasa kimekuwa chama kinachoongoza kwa rushwa
   
 8. l

  lufungulo k JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 1,267
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  sikubali, sikubali, sikubali kuona kuwa chaguzi za CCM tu tena za mallalamiko ya walioshindwa ndo eti rushwa italipeleka pabaya Taifa hili, Mgawo wa viwanja maeneo mbalimbali ya nchi mfano Gezaulole viongozi wa wananchi siasa na kidini mmekaa kimya mpaka leo viwanja vinagawiwa [vilivyotangazwa vimeisha] hilo aaah Mzee Mwamakula unaona sawa. narudia asiye kupenda hata ukimpa rushwa hakuchagui . nenda kwenye ofisi zote unazozijua ww zenye malisho bora uone waliokalia nafasi hizo wanatoka ktk familia zipi hilo aaaah halilipeleki taifa kubaya. nipe khanga, kofia na t-shirt ntapokea kama sikupendi sikupi kura yangu jamani tujielezee kiualisia na hali halisi ya Utanzania wetu porojo tuache.
   
 9. kawakama

  kawakama JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,303
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  KKKT=Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
  KKKT=Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanganyika
  ???????????????????????
  !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  JK mwenyewe ni matokeo ya rushwa! unategemea afanye nini??
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Mchungaji vipi rushwa kwenye uchaguzi wa Bavicha ulitoa kauli gani.
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  kikwete ameagiza vijana wa magamba wapokee pesa [za rushwa] ila wasiwapigie kura hao wanaowapatia rushwa.


  ukimwi na rushwa avitaisha maana wengine wanatowaga rushwa ya kunaniliuliwa.
   
 13. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,928
  Likes Received: 1,859
  Trophy Points: 280

  hapo tukisema baadhi ya viongozi wa dini hii ni pro-chadema tunaonekana wachumia tumbo na tumetumwa
  sasa mchungaji anapodiriki kusema kua hayo makanisa yaliyochomwa yajengwe kwa gharama za serikali sasa hiyo serikali ndio iliyoyachoma??
  Then mbona wanaonekana tu kutoa matamko ya uangalizi kwa chama fulani huku vyama vingne vinapohitaji kutolewa matamko kama haya hatuskii yakitamkwa??
  Chadema=chaga+ dini fulani na inafahamika vyema tuh...
   
 14. S

  Savannah JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM na Serikali yake inaendeshwa kwa rushwa "of the highest order" siku zote. JK hawezi kuchukua hatua yeyote.
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Huyo mchungaji si akakate nyasi tu.........haya mambo hayana uchungaji
   
 16. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Rushwa siyo tu kwamba zipo kwenye chaguzi. Kuna rushwa sehemu nyingi mahakamani, polisi, hospitalini, ajira, ofisi za ardhi. Hapa Tanzania rushwa ni mtindo wa maisha kwa watu wa ngazi zote. Hivyo, kuiondoa ni mzigo.
   
 17. T

  Tabby JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,895
  Likes Received: 5,528
  Trophy Points: 280
  Raisi mwenyewe aliingia ikulu kwa kuchakachua. Obvious kuna incentive aliyowapa usalama wa taifa, tume ya uchaguzi na takukuru ili kufanikisha upotoshaji huo wa kweli na haki ya wananchi walio wengi kuongozwa na mtu wamtakaye. Hicho kitu si kingine zaidi ya rushwa. Kama raisi anatawala kwa rungu la rushwa na chama chake kinalijua hili, itakuwa ni ajabu aanze kuwakataza. Ubavu huo hana. Sasa hivi rushwa ni moja ya maadili ya ccm.

  Na kama ccm itaruhusiwa kuendelea na ujanjajanja na hila zake ili iendelee na utawala wake dharimu, Watz wa kawaida tumekwisha.

  Sitaki kusema mengi lakini TZ inahitaji mabadiliko makubwa ambayo ccm chini ya viongozi wake hawawezi kukubali yatokee. Dawa yake ni jeshi lichukue nchi, lisimamie katiba mpya na uchaguzi huru.
   
 18. M

  Mr jokes and serious Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu rais toz kweli ni dhaifu jamani duuu,adi inabore,alafu unakuta mtu msomi na akili zake timamu unakuta ana wapenda penda ccm,wakati bosi wao ana lalamika je wanaomfuata chini yake wafanye nini,ccm uozo tusitegemee mabadiliko kupitia hichi chama wameoza wote na hao uvccm wameoza,kulikomboa taifa dawa kubadili cha tawala full stop.
   
 19. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Mchungaji hajatambua tuu kinachoendelea?
  kwa ufupi ni haya:
  -Hao ni watu wachache wanaotaka kichafulia jina chama chetu.
  -JK hana shina ni wasaidizi wake tuu ndio wanamharibia.
  -CCM haina shida wenye shida ni wafuasi.Na usiulize kwanini wafuasi wenye waliofundwa kwa misingi ya chama ndio wanabaribi hayo.

  -CCM ni chama cha amani.(uisulize mibunduki ya wagombea na wapambe wao)
  -CCM ni chama cha wanyonge.
  -CCM ni chama kinacholinda wananchi.Usiulize ya mwangosi.
  ........endelea mengine...........
   
 20. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwanza, kwa nini huyu mchungaji yuko sana interested na kinachotokea ndani ya CCM? Anataka kutupa picha kuwa we need to save this sinking ship MV CCM. Awaache CCM wajifie wenyewe kwa kuwa ndio path ambayo wameichagua.

  Pili, ushauri huu kwa kweli ni irrelevant kwa JK. Maana akiamua kufuta hizi chaguzi kwa sababu anazotoa mchungaji hapa basi na yeye (JK) ajiuzulu. Au tuseme kuwa kwa kuanzia atumie wadhifa wake kuitisha upya chaguzi ziligubikwa na rushwa na yeye pia in turn ajipime kupitia michakato iliyomuingiza madarakani aone kama na yeye bado anastahili kutuongoza.

  Mwisho, mchungaji apime upepo ajue kwamba bila fedha hupati kitu CCM. Na kujiunga au kushabikia CCM ni hiari ya mtu na si lazima.
   
Loading...