Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Nnjaa Mbaya....yani hatawewe umepewa Kijisent cha Kumsafisha Bashite.....Sasa naona Mambo ya Uwakiki yamekufa Rasm
 
ndio ujiulize, kwanini Yesu akuacha kanisa kwa Malaika, akaamua kuliacha kanisa kwa binadamu..

Majibu mepesi ni kwakuwa binadamu anaanguka na kusimama, ili utukufu wake uweze kutukuka...

uwezi kumuelewa Askofu Gwajima kwa hata maandiko yanasema "tazama haya yalifichwa kwa watu wazima lakin wakafunuliwa watto wadogo"...

alafu hakuna mahala, Gwajima alishawahi kujiita yeye ni Nabiii....

mimi ni mkatoliki, ila kama umefichwa hekima ya kimungu kaa kimya
 
Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "kiumbe".

Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Mchungaji Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, jee namna ambayo Mchungaji Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa, ndivyo Bwana Yesu alivyofundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto mgeuzie na la kuume. Adui mpende. Samehe saba mara sabini. Vipi kuhusu Baba Mchungaji Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo? .

Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.

Jumatatu Njema.
Paskali
Your Good
 
divishen zero haina cheti hawa ndo watumishi hewa ukiskia
Living ni cheti pia, huyo unayemwita mtumishi hewa sasa anamhenyesha boss wako Daud Albert mpaka anakesha kwa waganga wa kienyeji, Bakwata, na sasa kampa pesa pasco na Steven Nyerere wamtetee, angekuwa mchungaji hewa mngehangaika kupoteza mda?
 
Hivi hadi gwajima anatamka maneno hayo ulimfuatilia tokea mwanzo?? Ndio shida ya kudandia treni kwa mbele!! Wala usingekuja na upuuzi huo!! Ubashite huu ni shidaaaa
Akili ni nywele kila mtu ana zake,ww hujamuelewa lakini wengi wanye wepesi ktk kuelewa wamemwelewa vizuri ndiyo maana wanajadili kwa kiina juu ya ligi hii ya boss wako Daud vs Gwajma
 
kuna muda mwingine huwa nawashangaa sana watu wanaokosoaga watumish wa Mungu. let me tell you Pascal Mayalla, hawa watumish wa Mungu sio kazi yetu kuwahukumu manake kazi waifanyayo sio yetu ni ya Mungu. na yy ndie awezaye kusoma nafsi na kuhukumu.

istoshe hivi unakumbuka neno ambalo Bwana wetu Yesu Kristo alimwambia Petro siku Petro alipomwambia kwamba je kwani yampasa kufa? YESU ALIMJIBU 'PITA NYUMA YANGU WEEE SHETANI'
neno ambalo hata leo hii hakuna mtumish wa Mungu aliyewah kuthubutu kumwambia mtu. hivi unadhani Yesu angekuwa leo hii atumie neno hili ungesemaje?
 
kuna muda mwingine huwa nawashangaa sana watu wanaokosoaga watumish wa Mungu. let me tell you Pascal Mayalla, hawa watumish wa Mungu sio kazi yetu kuwahukumu manake kazi waifanyayo sio yetu ni ya Mungu. na yy ndie awezaye kusoma nafsi na kuhukumu.

istoshe hivi unakumbuka neno ambalo Bwana wetu Yesu Kristo alimwambia Petro siku Petro alipomwambia kwamba je kwani yampasa kufa? YESU ALIMJIBU 'PITA NYUMA YANGU WEEE SHETANI'
neno ambalo hata leo hii hakuna mtumish wa Mungu aliyewah kuthubutu kumwambia mtu. hivi unadhani Yesu angekuwa leo hii atumie neno hili ungesemaje?
Kuwa mtumishi wa Mungu si kigezo cha kuruhusu tabia ya kubambikiwa Kesi, hiyo tabia ya kubambikia mtu kesi lazima ilaaniwe vilivyo pasipo kuangalia maandiko yeyote, ww unamsaidia Pasco mayala lakini mwenzako kapewa pesa amtetee makonda huoni kama na ww unatenda dhambi? Msitumie maandiko matakatifu kuharalisha uonevu, ukandamizaji, Udikteta, kubambikia watu kesi.
 
Nakubaliana nae kuwa yeye ni zaidi ya rais ikiwa tu ni mtumishi wa kweli anaemtumikia mungu lakini kama ni ngru mbili ujue hamfikii rais hata kidogo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom