Mchungaji Gwajima Kuueleza Umma Kesho kuhusu Mkenya wa Ulimboka

Baada ya kufanya bidii za maksudi kutaka kujua sakata hili la shambulizi la Mwenyekiti Wa Jumuia ya Madaktari TZ, Dr. Steve Ulimboka pamoja Na madai yaliyotolewa Jana Na Kamanda Kova kwamba Kuna Mtu anaedaiwa kuhusika Na utekaji Na shambulizi Hilo aliyejitokeza kujisalimisha ndani ya Kanisa linaloongozwa Mch Josephat Gwajima, pamoja Na utata uliosambaa juu ya matamshi hayo, nimebahatika hatimae kuongea na Mchungaji huyo..

Yeye mwenyewe Kwanza amekiri kusikia taarifa hizo Na pia maelfu ya watu miongoni mwao ni washirika NOa watu wengine nje ya Kanisa nao wamekuwa wakimtafuta ili kupata ukweli Wa matamshi hayo ya Polisi

Mchungaji huyo ambaye Kwa mtazamo ni mpole, mkimya Na mwenye maneno yaliyonyooka, akasema kwamba kuna taarifa aliletewa Na walinzi wa Kanisa kwamba kuna kijana mdogo tu alikuwa akidai yeye ndiye Kinara wa sakata Hilo la kumteka daktari huyo..Na walinzi Hao wakampeleka kituoni Na kumkabidhi huko.. Sasa cha Ajabu ni taarifa ya Jana ya jeshi la polisi juu ya uhusika wa tukio Hili..

Na yeye Kama kiongozi imemgharimu kuwaita Upya wale walinzi Na kupata kutoka kwao taarifa hiyo Na hatimae kesho kwenye Ibaada maalum ataelezea Mkasa wote ulivyokuwa ili jamii ielewe nini kilichojiri..

Nimepitia comment nyingi za watu humu kila Mtu akinadi Na kusema lake, wapo wanaotukana Na wapo wanalalamika Kwa namna wajuao.. Labda nitoe rai kwamba ni vema tuwe Na subira Na kupata Picha kamili hiyo kesho..

Mimi mwenyewe nitawahi mapema Na Kama kawaida ya TAMKO nitawajuza kila kitu..matusi kejeli si mahali pake nadhani kuna kamchezo kanaendelea ambako lazima kafichuliwe sasa.. Jambo Hili si Dogo linagusa masikio ya mataifa mengi Kwa sasa..

..

..

Kabla ya kesho Gwajima atakuwa ameulimbokiwa!!!
 
Tapeli tu huyu mchungaji
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la ufufuo na Uzima kesho atatoa ukweli kuhusu kilichotokea kuhusu mtu aliyekamatwa. Mtu huyo anaonekana alitumwa akamteke mchungaji huyo ambaye anaikosoa sana serikali. Kama unaweza hudhuria ibada ya kesho pale Tanganyika Packers
 
Ajue tu kama ni Bwana Yesu ninayemshuhudia maishan mwangu-hakika hapendi makorokocho
 
Huyu ndio mchungaji Gwajima. tujihadhali sana na watu wa namna hii.

[h=2]Monday, May 14, 2012[/h] [h=3]Mchungaji Mtikila Adai Mchungaji Gwajima Anawalipa Watu Kujifanya Misukule[/h]
MWENYEKITI wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amemtuhumu mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko Kawe Tanganyika Packers, kuwaahidi watu fedha wajifanye misukule awafufue.

Mtikila alidai hayo mahakamani mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ilvin Mgeta wakati akitoa ushahidi wake katika kesi inayomkabili ya kuchapisha na kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.

Akitoa ushahidi wake alidai kuwa chanzo cha kesi hiyo kinatokana na yeye kumfuata mchungaji Gwajima akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya muda ya Ukristo ya kutetea amani mwaka 2010, kumweleza tabia hiyo anayofanya sio nzuri.

Alidai Gwajima hakufurahia kitendo hicho akamuahidi kumshitaki kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu waraka aliokuwa akiusambaza (Mtikila) ili afungwe.

Alidai aliamua kumfuata mchungaji huyo baada ya watu kumweleza kwamba Mchungaji Gwajima aliwaahidi Sh 300,000 ili wajipake vumbi na kuvaa magunia wapigwe picha na kujitangaza kuwa walikuwa wamekufa halafu Gwajima ajifanye amewafufua.

“… tena mmojawapo ni mtumishi wako wa mahakamani hapa ila nimesikia amehama, walinifuata na kunieleza kuwa waliahidiwa fedha ili mtoto wake ajifanye alikuwa amefichwa chini ya ziwa Victoria kwa miaka saba na wakatangaza kuwa aliuawa na baba yake mzazi kumbe ni mbinu ya Gwajima ajifanye amemfufua,” alidai Mtikila. Aidai kuwa baadaye alifuatilia na kugundua mtu huyo alikuwepo na hakuwahi kufa.

Aliendelea kudai kuwa anaamini kushitakiwa kwake katika kesi hiyo kunatokana na Mchungaji Gwajima kwa sababu baada ya kupokea malalamiko hayo kutoka kwa waumini wa kanisa lake la Ufufuo na Uzima, aliambatana nao pamoja na wachungaji wengine kumfuata akidai kuwa nia yao wamkemee kama neno la Mungu linavyosema.

“Hatukufanikiwa, Gwajima alibadilika akasema anaongea na Rais nifungwe kutokana na waraka niliouandika, akasema kabisa anaweza kumpigia simu wakati huo huo. Hivyo naamini kabisa msingi wa kesi hii ni Gwajima,” alidai Mtikila.

Mtikila alidai kuwa alimpa Rais Kikwete waraka huo aliouandaa ambao ulikuwa ukisambazwa nchi nzima lakini hakufikishwa mahakamani na kuhoji kuwa iweje aburuzwe mahakamani baada ya kwenda kwa mchungaji Gwajima.
Mchungaji Gwajima

Alidai kuwa siku moja alfajiri nyumba yake ilizingirwa na askari kama 12 wakimtaka afungue mlango akidai kuwa kutokana na yeye kuwa mzoefu wa kupekuliwa na askari, alipofungua alipekuliwa na kutakiwa kwenda kituo kikuu cha polisi.

Alidai alipowauliza askari sababu ya kupelekwa polisi kuwa ni kwa ajili ya waraka ule, walikiri na ndipo aliwatolea nakala kila mmoja na yake akawapa wasome na akakumbuka maneno ya mchungaji Gwajima kuwa atamfunga.

Aliendelea kudai kuwa aliwaomba askari wale wamsubiri atoe nakala 70 zaidi ili awapatie watu waliokuwa wakisubiri kwa sababu alitakiwa kwenda na kompyuta yake polisi. Alipofika huko aliwakuta watu 14 ambao walikuwa wakimhoji na wanne kati yao walimhoji kama alikuwa na tofauti na Gwajima.

Aidha, Mtikila alidai kuwa mchungaji Gwajima alikuwa ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa Jamhuri lakini hakutokea mahakamani akidai kuwa alijua amemkosea Mungu na kanisa badala yake walikuja watu wake ambao hawakuwepo siku alipokwenda kwa Mchungaji huyo.

Katika ushahidi wake Mtikila alidai kuwa alialikwa kuhubiri Agosti mosi hadi 3, 2009 Mwanza kwenye kongamano, yale aliyohutubia wakamuomba ayaweke kwenye maandishi ili ujumbe uwafikie viongozi wote Wakristo nchini ambapo zilizalishwa nakala 1,000, ziligawiwa 700 akabaki na 300 kwa ajili ya kusambaza.

Mtikila alikiri maelezo yake ya polisi Aprili 15, 2010 yaliyosomwa na kutolewa mahakamani kama kielelezo katika ushahidi wa Jamhuri. Alikiri kuwa kweli aliuandaa waraka huo na kuusambaza mwaka 2009, lakini alikanusha kwamba haukuwa wa uchochezi kwani unahusu maneno ya Mungu.

Mtikila alikiri zilikuwa nakala 100,000 ambazo zilisema kwamba Rais Kikwete anaangamiza Ukristo na amekuwa jasiri kuingiza Uislamu katika Katiba ya Jamhuri, wakristo waungane kuweka mtu Ikulu’.

Kesi hiyo itaendelea Juni 25 mwaka huu kwa ajili ya Mtikila kuendelea kutoa ushahidi wake. Alidai kuwa kesi hiyo imekusudiwa ifungwe kwa sababu ni mtakatifu hana dhambi anatetea Ukristo.

Source: Habari Leo.
 
Huyu ndio mchungaji Gwajima. tujihadhali sana na watu wa namna hii.

[h=2]Monday, May 14, 2012[/h] [h=3]Mchungaji Mtikila Adai Mchungaji Gwajima Anawalipa Watu Kujifanya Misukule[/h]
MWENYEKITI wa Chama cha DeOmocratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amemtuhumu mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko Kawe Tanganyika Packers, kuwaahidi watu fedha wajifanye misukule awafufue.

Mtikila alidai hayo mahakamani mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ilvin Mgeta wakati akitoa ushahidi wake katika kesi inayomkabili ya kuchapisha na kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.

Akitoa ushahidi wake alidai kuwa chanzo cha kesi hiyo kinatokana na yeye kumfuata mchungaji Gwajima akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya muda ya Ukristo ya kutetea amani mwaka 2010, kumweleza tabia hiyo anayofanya sio nzuri.

Alidai Gwajima hakufurahia kitendo hicho akamuahidi kumshitaki kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu waraka aliokuwa akiusambaza (Mtikila) ili afungwe.

Alidai aliamua kumfuata mchungaji huyo baada ya watu kumweleza kwamba Mchungaji Gwajima aliwaahidi Sh 300,000 ili wajipake vumbi na kuvaa magunia wapigwe picha na kujitangaza kuwa walikuwa wamekufa halafu Gwajima ajifanye amewafufua.

“… tena mmojawapo ni mtumishi wako wa mahakamani hapa ila nimesikia amehama, walinifuata na kunieleza kuwa waliahidiwa fedha ili mtoto wake ajifanye alikuwa amefichwa chini ya ziwa Victoria kwa miaka saba na wakatangaza kuwa aliuawa na baba yake mzazi kumbe ni mbinu ya Gwajima ajifanye amemfufua,” alidai Mtikila. Aidai kuwa baadaye alifuatilia na kugundua mtu huyo alikuwepo na hakuwahi kufa.

Aliendelea kudai kuwa anaamini kushitakiwa kwake katika kesi hiyo kunatokana na Mchungaji Gwajima kwa sababu baada ya kupokea malalamiko hayo kutoka kwa waumini wa kanisa lake la Ufufuo na Uzima, aliambatana nao pamoja na wachungaji wengine kumfuata akidai kuwa nia yao wamkemee kama neno la Mungu linavyosema.

“Hatukufanikiwa, Gwajima alibadilika akasema anaongea na Rais nifungwe kutokana na waraka niliouandika, akasema kabisa anaweza kumpigia simu wakati huo huo. Hivyo naamini kabisa msingi wa kesi hii ni Gwajima,” alidai Mtikila.

Mtikila alidai kuwa alimpa Rais Kikwete waraka huo aliouandaa ambao ulikuwa ukisambazwa nchi nzima lakini hakufikishwa mahakamani na kuhoji kuwa iweje aburuzwe mahakamani baada ya kwenda kwa mchungaji Gwajima.
Mchungaji Gwajima

Alidai kuwa siku moja alfajiri nyumba yake ilizingirwa na askari kama 12 wakimtaka afungue mlango akidai kuwa kutokana na yeye kuwa mzoefu wa kupekuliwa na askari, alipofungua alipekuliwa na kutakiwa kwenda kituo kikuu cha polisi.

Alidai alipowauliza askari sababu ya kupelekwa polisi kuwa ni kwa ajili ya waraka ule, walikiri na ndipo aliwatolea nakala kila mmoja na yake akawapa wasome na akakumbuka maneno ya mchungaji Gwajima kuwa atamfunga.

Aliendelea kudai kuwa aliwaomba askari wale wamsubiri atoe nakala 70 zaidi ili awapatie watu waliokuwa wakisubiri kwa sababu alitakiwa kwenda na kompyuta yake polisi. Alipofika huko aliwakuta watu 14 ambao walikuwa wakimhoji na wanne kati yao walimhoji kama alikuwa na tofauti na Gwajima.

Aidha, Mtikila alidai kuwa mchungaji Gwajima alikuwa ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa Jamhuri lakini hakutokea mahakamani akidai kuwa alijua amemkosea Mungu na kanisa badala yake walikuja watu wake ambao hawakuwepo siku alipokwenda kwa Mchungaji huyo.

Katika ushahidi wake Mtikila alidai kuwa alialikwa kuhubiri Agosti mosi hadi 3, 2009 Mwanza kwenye kongamano, yale aliyohutubia wakamuomba ayaweke kwenye maandishi ili ujumbe uwafikie viongozi wote Wakristo nchini ambapo zilizalishwa nakala 1,000, ziligawiwa 700 akabaki na 300 kwa ajili ya kusambaza.

Mtikila alikiri maelezo yake ya polisi Aprili 15, 2010 yaliyosomwa na kutolewa mahakamani kama kielelezo katika ushahidi wa Jamhuri. Alikiri kuwa kweli aliuandaa waraka huo na kuusambaza mwaka 2009, lakini alikanusha kwamba haukuwa wa uchochezi kwani unahusu maneno ya Mungu.

Mtikila alikiri zilikuwa nakala 100,000 ambazo zilisema kwamba Rais Kikwete anaangamiza Ukristo na amekuwa jasiri kuingiza Uislamu katika Katiba ya Jamhuri, wakristo waungane kuweka mtu Ikulu’.

Kesi hiyo itaendelea Juni 25 mwaka huu kwa ajili ya Mtikila kuendelea kutoa ushahidi wake. Alidai kuwa kesi hiyo imekusudiwa ifungwe kwa sababu ni mtakatifu hana dhambi anatetea Ukristo.

Source: Habari Leo.
..
SEMENI MSEMALO.. Kesho wanaume tupo pahala hapo.. Tutajua huko huko mbivu Na Mbichi..
 
Kabla ya kesho Gwajima atakuwa ameulimbokiwa!!!
Kweli. Hawa watu walivyo desperate, si wakusubiri kuueleza umma kesho. If it isn't a conspiracy anaweza asiione hiyo kesho. Nadhani mkutano wa CCM pale Jangwani huyu mchungaji ndiye alichangia vipaza sauti.
 
..
SEMENI MSEMALO.. Kesho wanaume tupo pahala hapo.. Tutajua huko huko mbivu Na Mbichi..
Hili fungu la 10 litawapeleka motoni huku mnajiona, sasa Mtikila ni mchungaji na Gwajima ni mchungaji je nani mkweli? I don,t buy you're story. hata Rwakatare aliwahi kutuambia kuna mchawi kanasa kwenye paa la kanisa lake akitoka kuwanga. nyinyi ndio mtageuzwa kuni siku ya Judgement day.
 
Mmmmmmh napita tu inanikumbusha ngoma ya shagy church ! Teh teh teh teh usalama wetu upo shakani watanzania mpaka nchi jirani wanakuja kututeka na kutupiga wakiwa na silaha na gari lisilo na number. Halafu mnatuambia ulinzi ni haki ya kila raia nathani ni haki ya kila kiongozi na kada wa.....
 
Muvu inazidi kunoga sehemu yakwanza na ya pili tayari sehemu ya tatu ni mchungaji Gwajima usikose ndugu mtazamaji

sehemu ya nne ndio nzito zaidi Uli akitimba Bongo...mbona joka atajisaidia aja zote.
 
Hili fungu la 10 litawapeleka motoni huku mnajiona, sasa Mtikila ni mchungaji na Gwajima ni mchungaji je nani mkweli? I don,t buy you're story. hata Rwakatare aliwahi kutuambia kuna mchawi kanasa kwenye paa la kanisa lake akitoka kuwanga. nyinyi ndio mtageuzwa kuni siku ya Judgement day.
..
Mbona unaogopa hivyo hata kamata kamata haijaanza.. Mtajibeba Mbona mwaka huu.. Mtajua nchi Ina wenyewe..Na wenyewe ndio tunaamka saa.. Kamata Wezi men..!!! Mbona mtahama nchi!!!
 
Siku zote MUNGU hataniwi na endapo utamtania adhabu yake ipo hapa hapa sasa nakuonya Mchungaji chonde chonde usimchezee mungu. kama ni danganya toto upo katika imani za FREEMANSON utuambie mapema ili waumini mwako tukukimbie.
 
tatizo la wachungaji hawa hasa Gwajimahasemi siri hiyo mpaka mmetoa sadaka, mnaoenda nendeni hapo hakuna lolote kwani Dr Ulli wakati anatekwa na silaha na kupakiwa katika gari isiyokuwa na No. yule aliyemteka alikuwa Mtu mhuhimu mbona asishtuke kuwa hawa ni majambazi? Bado asubuhi akakamatwa mwingine chooni Muhimbili bado akawa sio Mkenya
Ushauri huyo Askofu asijidhalilishe kwa kupandikizwa kwani maneno ya Mtikila yatakuwa ni kweli
 
Guys, kuna mtu anamfahamu sana huyo Mchungaji alinieleza ukweli kuwa huyo Mchungaji sio real, anafanya hivyo ili kujitajirisha kwa sadaka za waumini, aliniambia hana lolote kabisa na wala nisimweke akilini kama ni Mchungaji wa kweli, naona apart ya kutaka kujitajirisha kwa sadaka anataka pia kujiongezea kipato kwa kuifanyia serikali kazi zake chafu za kuipotosha, kuwapumbaza wananchi kwa kutumia huo Uchungaji wake wa kitapeli, badala ya kufanya ya Mungu au kwa baadhi ya Wachungaji wanaoaminiwa zaidi, badala ya kufanya wanayoagizwa na Mungu wanafanya mambo ya faida zao binafsi, wanajaribu kupumbaza Taifa ili tuweze kupelekwapelekwa kirahisi na viongozi wabovu, hawa adhabu yao itaendana sambamba na ya hao wahuni wenzao
 
Hivi hizi fedha zote wanazotumia kusuka upuuzi wao, wangekuwa wameshaongeza vitanda vingapi kwenye wodi za wazazi, yaani wajawazito wanalala wanne wanne kwenye kitanda wodini, wenyewe wanatapanya hela, wanawapa wahalifu wajenge majumba ya kifahari kwasababu ya kuwatimizia kazi ya kuwadhuru raia wao wema, eti kwa kuwa kosa lao ni kuwaambia ukweli, kuwakosoa, kutetea haki na kusimama kwenye ukweli, guys, viongozi wetu wengi ni wapuuzi, ukiwafikiria, unapata hasira
 
Back
Top Bottom