MCHUNGAJI GWAJIMA AITIKISA TANGA, MKUTANO WAKE WAVUNJA REKODI (Picha Ufufuo na Uzima Blog)

Status
Not open for further replies.

davidm

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
393
127
MM7.jpg MM4.jpg A+25.jpg M+1.jpg K+33.jpg

Mkutano wa Mchungaji Josephat Gwajima umevunja rekodi ya maudhurio ya watu katika mikutano ya mjini hapa Tanga; baada ya kushuhudia kwa mara ya kwanza maelfu kwa maelfu ya watu wakiwa katika mkutano wa injili jambo ambalo si kawaida mkoani hapa; Mkutano huo wa siku nane ni kana kwamba ulisimamisha shughuli nyingi wakati wa jioni kwa umati ulioonekana. Jeshi la polisi lililazimika kuruhusu mikutano kufika hadi usiku kwasababu ya umati wa watu ambao ulikuwa ukihimiza kuwa mahubiri yaendelee hata baada ya saa kumi na mbili jioni, hivyo kufanya siku zote nane kushuhudia mikutano ikiisha saa moja usiku huku watu wakigoma kuondoka uwanjani.

Pamoja na miujiza mingi iliyotokea, ni pamoja ya watu wengi kumwamini Yesu Kristo, misukule kurudishwa na wenye mapepo wengi kufunguliwa. Ukiacha upinzani wa baadhi ya watu, mkutano huo umevunja rekodi katika mji wa Tanga kwa sasa. hivi sasa Mchungaji Gwajima anaendelea na Mkutano wa Injili mkoani Morogoro ikiwa ni programu ya kuzinguka nchi nzima; ilianzia Arusha, Moshi, Tanga, sasa morogoro, baadaye Kilombero, Iringa, Njombe, Songea, Mbeya, Rukwa hadi Tanzania yote.
 
utadhani mziki wa M4C, kumbe watu now wamepata mwitikio wa kumjua MUNGU, thats gud!!
 
Daima nitamtegemea na kumsifu mungu.
Pia ni yeye aniokoe na kila roho wa Mpinga kristo.
Na yeye Awabariki wachungaji wote!
 
Duh mwanasiasa angepata nyomi kama hiyo kalele zingekuwa nyingi sana pande hizi
 
Sasa anazunguka mikoa ile ile inayomjua Kristu, kwa nini asiende na huko walikojaa walio wazito kumkubali Kristo?
 
vuta picha nyomi kama hilo lingekuwa limekusanyika kuwasikiliza tembo kinana,nepi na yule bmkubwa aliye underpeform UN.!
 
Umasikini na kukata tamaa ya maisha unachangia sana wengine kupiga pesa ndefu..ni mchezo wa akili tu...akili kichwani..!
 
Nabii hakubaliki kwao..
Piga kazi baba wanadamu hawana hiana..
Ukimtangaza Mungu visa ukitangaza uchawi visa..sasa mnataka nn????
Mtaenda tuu hata kwa mijeledi..
All da best man of God..!
 
Ooooh Haleluya, Glory to God. Injili itahubiriwa kwa kila kiumbe.
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom