davidm
JF-Expert Member
- Jan 10, 2012
- 393
- 127
Mkutano wa Mchungaji Josephat Gwajima umevunja rekodi ya maudhurio ya watu katika mikutano ya mjini hapa Tanga; baada ya kushuhudia kwa mara ya kwanza maelfu kwa maelfu ya watu wakiwa katika mkutano wa injili jambo ambalo si kawaida mkoani hapa; Mkutano huo wa siku nane ni kana kwamba ulisimamisha shughuli nyingi wakati wa jioni kwa umati ulioonekana. Jeshi la polisi lililazimika kuruhusu mikutano kufika hadi usiku kwasababu ya umati wa watu ambao ulikuwa ukihimiza kuwa mahubiri yaendelee hata baada ya saa kumi na mbili jioni, hivyo kufanya siku zote nane kushuhudia mikutano ikiisha saa moja usiku huku watu wakigoma kuondoka uwanjani.
Pamoja na miujiza mingi iliyotokea, ni pamoja ya watu wengi kumwamini Yesu Kristo, misukule kurudishwa na wenye mapepo wengi kufunguliwa. Ukiacha upinzani wa baadhi ya watu, mkutano huo umevunja rekodi katika mji wa Tanga kwa sasa. hivi sasa Mchungaji Gwajima anaendelea na Mkutano wa Injili mkoani Morogoro ikiwa ni programu ya kuzinguka nchi nzima; ilianzia Arusha, Moshi, Tanga, sasa morogoro, baadaye Kilombero, Iringa, Njombe, Songea, Mbeya, Rukwa hadi Tanzania yote.