Mchungaji Godfrey Mtui a.k.a WAG garege amefikishwa mahakamani kwa wizi

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
Soma vizuri kabla hujachangia

Mchungaaji Godfrey Mtui anamiliki Kanisa la Tanzania Pentecoste mission Church lililopo nje kidogo ya mji wa Moshi na anamiliki Garage iitwayo WAG Garage ambayo ipo nyumbani kwake.

Mtui amefikishwa katika makahama ya mwanzo mjini Moshi na kusomewa shitaka moja la wizi kwa njia ya mtandao wa kibenki,

Kwamba mwaka jana kuna mtu gari lake lilipata ajali,baada yakupata ajali akawasiliana na Bima wakamshauri akatengeneze Gari hilo kwenye garage ambayo inatoa risiti za EFD mashine na akafanya hivyo kwa kuunganishwa na fundi na Bima wakatuma mtathimini na kupata hesabu ya Milioni 2.6 na kuruhusu gari itengenezwe wakati wakianda taratibu za malipo.

Mwenye gari akaona isiwe shida akaanza kutengeza gari kwa gharama zake ili pesa ya Bima ikitoka achukue pesa yake.

Lakini Sharti la Bima ni kwamba pesa hiyo italipwa kupitia WAG Garage na WAG atampatia mteja huyo pesa hiyo lakini mchungaji wa kondoo wa bwana baada ya mpunga kuingizwa kwenye akaunti yake akausunda wote na jamaa akamwambia benki wamekomba pesa yote kwa vile wanamdai.

Hata hvyo baada ya benki kubanwa wakaweka mambo wazi kwamba mchungaji alishakomba pesa zote na alizichukua kwa awamu mbili ya kwanza alichukua Milioni 1.2 na ya pili akachukua Milioni 1.4

Baada ya jamaa kubanwa akajilipua kimaandishi kwamba atazirejesha pesa hizo na mpaka muda huu amerejesha Milioni moja na ushee na baada ya hapo amegoma kumalizia hilo salio na mkondo wa sheria ukafuata kwa kufikishwa mahakamani na ushahidi umembana kila kona kwamba pesa hiyo si yake ila ilipitia kwenye akaunti yake ili amlipe jamaa wa gari.

Mashahidi wametoa ushahidi wao leo na mahakama imemuona kuwa ana kesi ya kujibu na jumatatu anatakiwa aanze kujitetea kwa njia ya kuleta mashahidi

Tuendelee kunywa mtori nyama tutazikuta chini
 
Wote matapeli itakuwa mwenye gari na huyo mtathimini na mchungaji wamezikana hizo pesa za bima

Gharama za kutengeneza zaweza kuwa ilikuwa laki mbili zinazobaki wagawane
 
Kila mahali nchi inakuwa ngumu
BTW

Lazima tuwe na uwezo wa kutenganisha na kuelewa kuna utofauti mkubwa sana kati ya kuwa muumini , mchungaji ,askofu wa kanisa fulani na kuwa na hofu ya Mungu au kuwa na mahusiano binafsi na Mungu

Najua watakuja watu nakuponda makanisa yote nitaka niwaambie tu kosa la ujinga la mtu mmoja isiwe kigezo chaku hitimisha makanisa ni mabaya

Kiuhalisia makanisani watu wengi wanafungiliwa wale waliopitia kipindi kigumu na kukumbana na nguvu za giza watanielewa .

Achukuliwa hatua huyo mwamba inshort kazingua

Naomba kuwasilisha.
 
Kwamba mwaka jana kuna mtu gari lake lilipata ajali,baada yakupata ajali akawasiliana na Bima wakamshauri akatengeneze Gari hilo kwenye garage ambayo inatoa risiti za EFD mashine na akafanya hivyo kwa kuunganishwa na fundi na Bima wakatuma mtathimini na kupata hesabu ya Milioni 2.6 na kuruhusu gari itengenezwe wakati wakianda taratibu za malipo.

Mwenye gari akaona isiwe shida akaanza kutengeza gari kwa gharama zake ili pesa ya Bima ikitoka achukue pesa yake.

Lakini Sharti la Bima ni kwamba pesa hiyo italipwa kupitia WAG Garage na WAG atampatia mteja huyo pesa hiyo lakini mchungaji wa kondoo wa bwana baada ya mpunga kuingizwa kwenye akaunti yake akausunda wote na jamaa akamwambia benki wamekomba pesa yote kwa vile wanamdai.

Nyumba za ibada zinanajisiwa sana, nahisi laana zitaanza kutuandama kutokana na hayo ya kufanyia udanganyifu kupitia nyumba takatifu, nikikumbuka ile statement ya "...kiongozi mkubwa yuko ofisini anachapa kazi, mlitaka aende Kariakoo... wakati yuko kwenye mitungi ya hewa safi" Mungu atusamehe
 
Back
Top Bottom