Rais Magufuli amlipia Peter Msigwa Tsh. Milioni 38 ili atoke gerezani, CHADEMA wadai wameshamlipia Mil 40

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,482
20,426
Upendo ulioje? JPM amlipia Msigwa mil 38 kati ya mil 40.

Taarifa zaidi inakuja

====

maxresdefault.jpg

Rais wa Tanzania, John Magufuli amemlipia Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa faini ya Sh38 milioni kati ya Tsh 40 milioni anazotakiwa kulipa mbunge huyo ili atoke jela.

Baada ya ndugu kuchangishana na kupata Milioni 2, ikabidi wamfuata rais Magufuli kama mwanafamilia naye achangie. Mtoto wa Dada yake Msigwa(Mpwa wa Msigwa) amemuoa Mtoto wa Rais Magufuli.

Msemaji wa Ikulu Gerson Msigwa amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya ndugu kuchanga na kupata milioni mbili tu na hivyo kumtafuta Magufuli kupata msaada.

Ambao bado wapo katika gereza la Segerea ni Mbowe(Mbunge wa Hai), John Heche (Tarime Vijijini), John Mnyika (Kibamba), naibu katibu mkuu wa chama hicho-Zanzibar, Salum Mwalimu na Mchungaji Msigwa.

Wakati huo huo, CHADEMA wanadai wameshamlipia faini Mchungaji Msigwa Milioni Arobaini.

"Sisi kama chama tumelipa Sh100 milioni ya watu watatu ambao ni Peter Msigwa, John Mnyika na Salum Mwalimu na tumewalipia kupitia benki tawi la Azikiwe.

Tumeshapeleka malipo mahakamani, tunasubiri risiti za mahakama. Kama kuna mwingine amemlipia Mchungaji Msigwa hatuna ushahidi na uhakika nao, kama chama mahakama haijaturejeshea fedha za Msigwa kwamba kalipiwa mara mbili.” Amesema John Mrema.
1584018514357.png

1584018578916.png




















Pia soma:
1). Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini ya Tsh. Milioni 350 au kwenda jela, Wapelekwa Segerea

2). Rais Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati akitoka kutoa heshima za mwisho kwa Dada wa Mch. Peter Msigwa
 
Back
Top Bottom