Mchungaji Erasto: Upinzani siyo dhambi ila ukikomaa huzaa usaliti. Amfananisha Lissu na Yuda Iskarioti

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
34,167
2,000
Mchungaji Erasto anasema katika mahubiri yake kuwa upinzani siyo dhambi na upo kwa ajili ya kuwekana sawa ila ukiisha kukomaa huzaa wasaliti miongoni mwa wapinzani.

Mchungaji anasema hata Israel aliwagawa watoto wake yaani yale makabila 12 wengine kwa ajili ya kubariki na wengine kulaani.

Hata Yesu katika wale mitume wake wengine walikaa mkono wa kushoto na wengine mkono wa kulia, wale wa mkono wa kushoto ndio wa kuhoji na kudadisi.

Anamalizia mchungaji kwa kusema hata hawa wapinzani kwenye siasa ndio wale wa mkono wa kushoto ambao siyo watu wabaya bali kazi yao ni kuhoji na kudadisi ndio maana wanapewa ruzuku na serikali. Ila miongoni mwao atatokea msaliti si kwa bahati mbaya... La!..bali atasaliti bila kujijua. Kuna mbunge sasa yuko ugenini akiamini kule ndio salama kuwaeleza habari za nyumbani..... Namfananisha mbunge huyu na Yuda Iskarioti maana hajui atendalo.

Nawatakia Jumapili njema
Maendeleo hayana vyama na si lelemama!
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,026
2,000
Daa aaah Lumumba mmeishiwa baada ya kushindwa kujibu hoja kila loudspeaker ikitumwa inasagwa kama ngano.Mmeamua kuwatumia wajasiliadini wenye usajili wa makanisa kwenye flash ambayo yanaweza futwa na tamko hata LA bashite.Wamehamia kwenye vikanisa uchwara
 
chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,786
2,000
Mchungaji awe mchungaji,siasa ni ya wanasiasa,...Kama mchungaji anatakiwa asiegemee upande wowote kwani anaowahubiria wako wanaomchukia Lissu na wako wanaempenda...

Niliona uzi mwengine humu kuna mchungaji aliemfanananisha Makonda na Yesu,ingelikuwa dini ya kiislam Watu "fake" kama hawa wangelikiona cha mtema kuni..huwezi kucheza na neno la Mungu kwa maslahi binafsi..
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,536
2,000
Mchungaji Erasto anasema katika mahubiri yake kuwa upinzani siyo dhambi na upo kwa ajili ya kuwekana sawa ila ukiisha kukomaa huzaa wasaliti miongoni mwa wapinzani.

Mchungaji anasema hata Israel aliwagawa watoto wake yaani yale makabila 12 wengine kwa ajili ya kubariki na wengine kulaani.

Hata Yesu katika wale mitume wake wengine walikaa mkono wa kushoto na wengine mkono wa kulia, wale wa mkono wa kushoto ndio wa kuhoji na kudadisi.

Anamalizia mchungaji kwa kusema hata hawa wapinzani kwenye siasa ndio wale wa mkono wa kushoto ambao siyo watu wabaya bali kazi yao ni kuhoji na kudadisi ndio maana wanapewa ruzuku na serikali. Ila miongoni mwao atatokea msaliti si kwa bahati mbaya... La!..bali atasaliti bila kujijua. Kuna mbunge sasa yuko ugenini akiamini kule ndio salama kuwaeleza habari za nyumbani..... Namfananisha mbunge huyu na Yuda Iskarioti maana hajui atendalo.

Nawatakia Jumapili njema
Maendeleo hayana vyama na si lelemama!
Waumini wake hawajamuuliza usaliti wa lissu ni nini?yaani mtawala akiwa mbumbumbu ni lazima na watawaliwa wawe mbumbumbu? Sasa sarakasi za makinikia ziliishia wapi kama hawakuwa mbumbumbu? Mbona wameishia kufanya yale yale aliyoyasema Lissu.huyu mchungaji asiwaambukize waumini wake ujinga wake
 
Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,603
2,000
Mchungaji Erasto anasema katika mahubiri yake kuwa upinzani siyo dhambi na upo kwa ajili ya kuwekana sawa ila ukiisha kukomaa huzaa wasaliti miongoni mwa wapinzani.

Mchungaji anasema hata Israel aliwagawa watoto wake yaani yale makabila 12 wengine kwa ajili ya kubariki na wengine kulaani.

Hata Yesu katika wale mitume wake wengine walikaa mkono wa kushoto na wengine mkono wa kulia, wale wa mkono wa kushoto ndio wa kuhoji na kudadisi.

Anamalizia mchungaji kwa kusema hata hawa wapinzani kwenye siasa ndio wale wa mkono wa kushoto ambao siyo watu wabaya bali kazi yao ni kuhoji na kudadisi ndio maana wanapewa ruzuku na serikali. Ila miongoni mwao atatokea msaliti si kwa bahati mbaya... La!..bali atasaliti bila kujijua. Kuna mbunge sasa yuko ugenini akiamini kule ndio salama kuwaeleza habari za nyumbani..... Namfananisha mbunge huyu na Yuda Iskarioti maana hajui atendalo.

Nawatakia Jumapili njema
Maendeleo hayana vyama na si lelemama!
Hii tafsiri ya huyo "mchungaji" ni sahihi kwa "injili" na "biblia" ya ccm. Nina zaidi ya miaka 35 ya kusoma Biblia; sijawahi kuona mstari wowote ndani ya Biblia (iwe ile yenye vitabu 66 au ile yenye vitabu 72) unaosema Israeli aliwagawa watoto wake ili wengine awalaani na wengine awabariki.
Lakini sishangai kwa hili maana kwa ccm hii kusema UONGO NDIO IMANI YAO KUU.
Pamoja na hayo, mlipofikia sipo. Ni hatari sana kutumia NENO isivyo halali, na mkumbuke kuwa MUNGU hadhihakiwi.
 
Hujaelewa.....Watoto wengine aliwatamkia watawabariki watu na mataifa na watoto wengine watawalaani watenda maovu na wale wailaanio Israel.......hicho ndicho alichosema mchungaji!
 
Kunde Ekeke

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
6,631
2,000
Mababu zetu wameteswa wameuliwa wameijenga Marekani na Ulaya kwa jasho la damu bado wana nyonya rasilimali zetu wana anzisha vita mfano Libya.Halafu hao watu wawe wema huwa na washangaa wanasiasa wa AFRIKA eti wanakwenda ulaya kushitaki serikali zao lakini wanashindwa kuelewa kama sio hao Wazungu AFRIKA isingekuwa hivi Leo
 
Janken jr

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,128
2,000
Mchungaji Erasto anasema katika mahubiri yake kuwa upinzani siyo dhambi na upo kwa ajili ya kuwekana sawa ila ukiisha kukomaa huzaa wasaliti miongoni mwa wapinzani.

Mchungaji anasema hata Israel aliwagawa watoto wake yaani yale makabila 12 wengine kwa ajili ya kubariki na wengine kulaani.

Hata Yesu katika wale mitume wake wengine walikaa mkono wa kushoto na wengine mkono wa kulia, wale wa mkono wa kushoto ndio wa kuhoji na kudadisi.

Anamalizia mchungaji kwa kusema hata hawa wapinzani kwenye siasa ndio wale wa mkono wa kushoto ambao siyo watu wabaya bali kazi yao ni kuhoji na kudadisi ndio maana wanapewa ruzuku na serikali. Ila miongoni mwao atatokea msaliti si kwa bahati mbaya... La!..bali atasaliti bila kujijua. Kuna mbunge sasa yuko ugenini akiamini kule ndio salama kuwaeleza habari za nyumbani..... Namfananisha mbunge huyu na Yuda Iskarioti maana hajui atendalo.

Nawatakia Jumapili njema
Maendeleo hayana vyama na si lelemama!
unafiki wa viongozi wa dini unaosababishwa na ubinafsi na uoga hakuanza leo,ata Hitra alitetewa na viongozi wa dini kila uovu wake ulipotetewa,Vaticani ilikuwa nyuma yake siku zote za uovu wake,lakin hilo haliondoi ukweli kuwa alikuwa mwovu na mtawala mbaya,mmoja kati ya askari katika jeshi lake wakati wa vita kuu ya pili alikujakuwa papa wa kanisa la ROMAN catholic,papa Benedict xvi.papa Johnii ndie aliomba msamahaa kwa wote walioumizwa na utawala wa nazi hasa wayahudi a kitendo cha kanisa kutomkemea Hitra.akotoa hutuba kali yenye kichwa kwa nini kanisa lilinyamaza?
viongozi wa dini kwa miaka dahari hasa wanaotetea maslahi yao husimama upande wa watawala wakati wananchi wanateswa.Historia inauonyesha wakati wa mapinduzi ya ufaransa,wakati wa Karl max.
 
Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
6,319
2,000
Mchungaji uchwara wa chini ya mti ,kampeni ya kumsifia jiwe imeaanza nini maana wachungaji na maaskofu wa chiniya mti kina Kakobe ,gwajima ,lusekelo na wengine wamepangwa na jiwe kuzunguka nchi nzima wanasifia ,suala la muda tu mtaliona ,Jana alianza lusekelo Leo hii mchungaji uchwara .
 
Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
12,917
2,000
Kwani Yuda alipigwa risasi 16? Huyo mchungaji mjinga sana. Wasaliti ni hao waliopanga na kumpiga risasi Lissu. Yaani mtu apigwe risasi 16 halafu anapoongelea machungu yaliyompata aitwe msaliti?! Never on earth!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom