Mchungaji Erasto: Upendo aliouonyesha Rais Magufuli kwa Msigwa umesimamia kwenye huu mstari "...Baba uwasamehe hawajui walitendalo"

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
30,383
2,000
Mchungaji Erasto amesema Rais Magufuli ameonyesha upendo mkuu na wa mfano katika kipindi hiki cha Kwaresma kwa kuwasamehe Chadema kupitia mbunge wao Mchungaji Msigwa.

Hii ina maana kubwa na hata mtumishi wa Mungu Msigwa analielewa hili kwamba ametolewa gerezani na mtu ambaye amewekwa kwenye mamlaka na Mungu.... Japokuwa wana uhusiano wa kinduge, anasema Mchungaji Erasto

Pamoja na ukosoaji wa Msigwa kwa serikali inayoongozwa na ndugu yake lakini Roho wa Mungu ametufundisha kusamehe kama Yesu mwenyewe alivyosema kwamba Mungu na awasamehe watesi wake kwa kuwa hawajui walitendalo.....anasisitiza Mchungaji.

Mwisho Mchungaji Erasto Shirima amewataka Chadema kuenenda katika hali ya kumpendeza Mungu kwani uzushi na unafiki ni makemeo makuu wakati wakati huu wa Kwaresma.
Pia amewataka CCM kuacha kuvamia mambo ya msingi yanayofanywa ama na Rais Magufuli au taasisi yake kwa maslahi binafsi ya chama kwani kuna tofauti kubwa kati ya Rais na amiri jeshi mkuu na yule mwenyekiti wa CCM.

Mungu awabariki nyote!
 

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,971
2,000
Hivi kwa kesi hiyo, walistahili kupata ile adhabu?

Sijawahi kusikia hayo makosa ya KIPOLISI, kumi na kitu, yooooote watuhumiwa wakutwe na hatia. Eti kati ya makosa 13, walikutwa na hatia makosa 12,na kila moja na adhabu yake. Kosa moja, linanyambuliwa na kutoa makosa mengine manne!

Hiyo kesi na kesi ya kumnyang'anya Lissu Ubunge, hukumu zake zimenishangaza sana!
Kwa sasa watu badala ya kujadili uhalali na hukumu ya hiyo kesi, wanajadili milioni 38 za JPM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nnangale

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
1,810
2,000
Huyu Mchungaji amekula maharage ya wapi......!!?
Tumefundishwa kutowanenea vibaya watumishi wa bwana lkn siku hizi wahuni wengi wanaitwa mchungaji ya Erasto alikuwa hajui kuwa akwilina aliuawa na polisi waliokuwa wanazuia maandamano ambayo kimsingi ni watu wachache waliokuwa wanafuata barua zao za Utambulisho kwa mkurugenzi ambaye aliwanyima kimkakati barua hizo.
 

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,025
2,000
Ndiyo maana aliwawekea mawakili tangu kesi ilipo anza...Katika ili tumkumbushe kua nae ni mtu na mtoto kama wengine asifikirie labda yeye ni zaidi ya wote. Awezi kujichimbia kaburi na kujizika
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,638
2,000
Ni mchungaji wa kanisa gani? Anatakiwa apimwe akili. Yaani unasema wakati wa kwaresima ni wa kutengeneza visasi na kisha kumsaidia uliyemdhuru ili Mungu akuone wema wako. Mungu wetu ana kazi kweli ikiwa hata watumishi wake ni wa aina hii.
 
Top Bottom