Uchaguzi 2019 Mchungaji Erasto: Tunamshukuru Mungu kampeni za uchaguzi zimemalizika kwa amani na jukumu la kesho Jehova atalisimamia

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
25,311
Points
2,000

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
25,311 2,000
Mchungaji Erasto ambaye wiki iliyopita alifanya maombi maalumu ya kuombea uchaguzi amemshukuru Mungu kwa baraka zake ambapo kampeni zimekamilika kwa amani kabisa.

Mchungaji amesema Mungu atawasamehe wale wote waliosusia uchaguzi kwa kuwa hawajui walitendalo.

Kadhalika mtumishi huyu wa Mungu amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kuchagua viongozi kwani siyo haki wala wajibu hapo basdae kumlaumu kiongozi ambaye hukushiriki kumpigia kura iwe ya kumkubali au kumkataa.

Mwisho mchungaji Erasto amewatakia wananvhi uchaguzi mwema.

Ahsanteni

Maendeleo hayana vyama!
 

S.Liondo

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Messages
3,398
Points
2,000

S.Liondo

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2011
3,398 2,000
Anaposema wale waliosusia uchaguzi Mungu atawasamee, anataka kutuaminisha kuwa kutokushiriki uchaguzi pamoja na kutoshiriki mchakato wake mzima ni dhambi mbele za Mungu?!! Viongozi wengine wa dini watakuwa na matatizo ya kiufahamu.
 

Kweyunga

Member
Joined
Dec 28, 2009
Messages
14
Points
45

Kweyunga

Member
Joined Dec 28, 2009
14 45
Anaposema wale waliosusia uchaguzi Mungu atawasamee, anataka kutuaminisha kuwa kutokushiriki uchaguzi pamoja na kutoshiriki mchakato wake mzima ni dhambi mbele za Mungu?!! Viongozi wengine wa dini watakuwa na matatizo ya kiufahamu.

Ndugu, Africa ina mengi nafikiri ni kwa huruma za Mungu kwamba bara hili mpaka sasa halijawa-colonized tena. Kuna watu leo ni wachungaji, mapadre, maaskofu n.k. kesho akija mtu akasema Tanzania ni colony lake, wanaweza kutuambia kumpinga au kusema hapana ni dhambi na waliosema hapana au kupinga waombewe wasamehewe..... Kiongozi wa kiimani hawezi kutambua mambo na ana wafuasi wanaamini anawafundisha mambo kwa usahihi, kazi kweli kweli
 

VAPS

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
3,204
Points
2,000

VAPS

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2012
3,204 2,000
Mambo yanaenda kasi sana awamu hii ya Tano, kigezo cha kusajili kanisa huenda wakaongeza Wadhamini kanisa wawe wanachama wa ccm hai walau kwa miaka miwili.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,294
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,294 2,000
Mie naanza kuamini kuna Mungu wawili.
Yupo Mungu baba mwenye enzi yote,muumba wa mbingu na dunia na huyo mwingine anaye itwa vilevile mungu wa kina mashimo, Tito na huyo sasa Erasto.
 

Forum statistics

Threads 1,381,428
Members 526,091
Posts 33,799,965
Top