Mchungaji Erasto: Nape, January na Ngeleja wamesamehewa kwa kuwa hawakujua walilokuwa wanalitenda

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,553
2,000
Mchungaji Erasto amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwasamehe wabunge watatu ambao ni Nape. January na Ngeleja na amemwombea baraka zaidi kutoka kwa Mungu.

Mchungaji Erasto anaamini kwamba wabunge hawa wamesamehewa kwa sababu hawakujua kile walichokuwa wanatenda kina madhara ya kiwango gani. Unajua Rais wa JMT ni amiri jeshi mkuu na isitoshe ndiye Mwenyekiti wa CCM na pia yeye ni sehemu ya bunge, amesisitiza mchungaji Erasto.

Kwa hiyo ukiyaelewa vizuri madaraka ya Rais huwezi kumletea upuuzi na mizaha hata kidogo, ni jambo jema wabunge hawa wametubu na Rais Magufuli amewasamehe amemalizia mchungaji.

Mwisho mchungaji anauliza unadhani kosa alilofanya mbunge Joshua Nassari lilikuwa halisameheki?!!........ndio ujue kuna binadamu wamebarikiwa talanta ya kusamehe!

Jumapili njema.
 
kidyongo

Senior Member
Oct 21, 2018
127
250
Anasamehewa aliyeomba msamaha kwa dhati,hata Mungu huwezi kumkosea harafu akakusamehe tu bila wewe mwenyewe kuomba radhi/kutubu
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,579
2,000
Anasamehewa aliyeomba msamaha kwa dhati,hata Mungu huwezi kumkosea harafu akakusamehe tu bila wewe mwenyewe kuomba radhi/kutubu
Lakini kuna tofauti kati ya mungu mtu na Mungu alieumba mbingu na nchi..mungu mtu ataweka kamera akurekodi na ataenda kukutangaza kwamba ameniomba msamaha..ametuma meseji usiku wa manane..ila Mungu alieumba mbingu na nchi yeye hataki sifa yeye ni kimya kimya tu...
 
mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,457
2,000
Mchungaji Erasto amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwasamehe wabunge watatu ambao ni Nape. January na Ngeleja na amemwombea baraka zaidi kutoka kwa Mungu.

Mchungaji Erasto anaamini kwamba wabunge hawa wamesamehewa kwa sababu hawakujua kile walichokuwa wanatenda kina madhara ya kiwango gani. Unajua Rais wa JMT ni amiri jeshi mkuu na isitoshe ndiye Mwenyekiti wa CCM na pia yeye ni sehemu ya bunge, amesisitiza mchungaji Erasto.

Kwa hiyo ukiyaelewa vizuri madaraka ya Rais huwezi kumletea upuuzi na mizaha hata kidogo, ni jambo jema wabunge hawa wametubu na Rais Magufuli amewasamehe amemalizia mchungaji.

Mwisho mchungaji anauliza unadhani kosa alilofanya mbunge Joshua Nassari lilikuwa halisameheki?!!........ndio ujue kuna binadamu wamebarikiwa talanta ya kusamehe!

Jumapili njema.
Mchungaji una uhakika gani kuwa walikuwa hawajui watendalo? Au wanalijua ndio maana wameomba msamaha?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom