Mchungaji Erasto: Kama kwenu hakuna maendeleo pambana na mbunge wako siyo kuilalamikia Geita!

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Kama mlichagua mbunge " zuzu" ni wazi kwa miaka mitano mtaendelea kuwa washangiliaji wa maendeleo katika maeneo mengine, anasema mchungaji Erasto.

Kazi ya mbunge ni kupigania maendeleo ya jimbo katika mgao wa keki ya taifa unaofanyika bungeni na siyo kula pipi na kupigia makofi kila jambo.

Kwa mfano huwezi kusikia jimbo la Vunjo wanalialia eti Chato kinajengwa chuo cha Veta, kwa sababu Dr Kimei yuko kimaendeleo na siyo umbea umbea amesisitiza mchungaji.

Mchungaji Erasto amemalizia kwa kusema ni vema wananchi waandae mikutano na wabunge wao kila mwezi kujadili maendeleo yao kama alivyokuwa akifanya Prof Jay pale Mikumi.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Kwani chato kabla ya kuanza kujengwa sasa haikuwa na mbunge?au jimbo la chato kwa mtazamo wa huyo mchungaji umeanza 2015?
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Ndiye aliyeplan mipango ya sasa na ikapitishwa!

Kupanga ni leo kutekeleza kesho!
Kwa maana hiyo wabunge wote wa Majimbo 360 wana plans wanasubiria siku wakiwa marais ndo watekeleze siyo? Au unataka kusema wabunge wa majimbo mengine hawakuwa na plan isipokuwa wa chato tu?
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,727
2,000
Kwa maana hiyo wabunge wote wa Majimbo 360 wana plans wanasubiria siku wakiwa marais ndo watekeleze siyo? Au unataka kusema wabunge wa majimbo mengine hawakuwa na plan isipokuwa wa chato tu?
Mipango siyo lazima uwe Rais bwashee!
 
Samiaagain2025

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
1,764
2,000
Kama mlichagua mbunge " zuzu" ni wazi kwa miaka mitano mtaendelea kuwa washangiliaji wa maendeleo katika maeneo mengine, anasema mchungaji Erasto.

Kazi ya mbunge ni kupigania maendeleo ya jimbo katika mgao wa keki ya taifa unaofanyika bungeni na siyo kula pipi na kupigia makofi kila jambo.

Kwa mfano huwezi kusikia jimbo la Vunjo wanalialia eti Chato kinajengwa chuo cha Veta, kwa sababu Dr Kimei yuko kimaendeleo na siyo umbea umbea amesisitiza mchungaji.

Mchungaji Erasto amemalizia kwa kusema ni vema wananchi waandae mikutano na wabunge wao kila mwezi kujadili maendeleo yao kama alivyokuwa akifanya Prof Jay pale Mikumi.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Mchungaji wa kanisa au mifugo?
 
JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
4,288
2,000
Mimi naona bado. Bahari ihamishiwe chato ili bandari ijengwe pale.

Kuhusu kuhamisha bahari wamcheki Mh Rungwe.

#Mitano tena
Ile chato ndiyo ingekuwa Bagamoyo, sasa hivi lile bandari la kibabe lililokuwa lijengwe pale , sasa lingekuwa ujenzi wake umeshika hatamu.
 
stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
5,156
2,000
Kumbe na sisi tukipata mbunge kama yule wa Chato tutaletewa
1. Uwanja wa kimataifa
2.Hospital ya Rufaa
3.Chuo cha veta
4.Majengo bora ya serikal(mahakama n.k)
5.Uwanja wa Mpira
6.Mbuga ya wanyama
na mengineo mengi...

kwani nasema uwongo ndugu zangu?

kwani unaumia ndugu yangu? ni kumi tena
 
Matrix19

JF-Expert Member
Feb 24, 2020
2,488
2,000
Enzi za unafiki wako

Eti "Maendeleo hayana vyama"

Tena tukaambiwa tusichanganye magunzi na mabetri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom