Mchungaji Erasto: Kama kwenu hakuna maendeleo pambana na mbunge wako siyo kuilalamikia Geita!

Tzmzalendo og

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
316
250
Kwahiyo bunge ndilo lililowaambia wananchi walio kwenye majimbo yenye wabunge wa upinzani wakati ule kuwa wakae na wabunge wao, hawatapewa pesa za maendeleo! Unapoandika jambo fukua ndani ya kichwa chako mazagazaga yote ndipo uandike.
Tecnic yenu au strategy yenu ilikuwa kusema fulan ailiuawa na kupigwa risas kwa Lisu , sasa Kama CCM walitumia hiyo strategy unaona ubaya gan, wakat CDM ilikuw ina import tuu chuki dhid ya serikal, ndo maana Kuna keyboard worriors sana hum , tena angeachwa afanye kila analotaka Lisu wenu angezalisha magaid kabisa ambao ndo majinga ya CDM yanaongozwa na mihemuko hayajui kutofautisha mbich na mbivu
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,727
2,000
Kama maamuzi yangekuwa yanafanyika bungeni kusingekuwepo kumsujudu na kumshukuru Magufuli kwa kila mradi unaojengwa hata kukamilisha ujenzi wa matundu ya choo.
Ukiona anasifiwa Rais Magufuli ujue mbunge wako alilala usingizi hakufanya jitihada zozote za kuwaletea maendeleo!
 

wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
6,853
2,000
Kashaletwa na hauna cha kufanya Zaid ya kulefusha Domo na kupiga umbea, na we muoga was kuingia barabaran, Yan maasikar ningewapatia box la mafuta ya mugando ili wawadhibit vzr

Naona pedi yako imekaa vibaya,hebu iweke vzr urudi hapa jukwaani.
 

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,498
2,000
Kama mlichagua mbunge " zuzu" ni wazi kwa miaka mitano mtaendelea kuwa washangiliaji wa maendeleo katika maeneo mengine, anasema mchungaji Erasto.

Kazi ya mbunge ni kupigania maendeleo ya jimbo katika mgao wa keki ya taifa unaofanyika bungeni na siyo kula pipi na kupigia makofi kila jambo.

Kwa mfano huwezi kusikia jimbo la Vunjo wanalialia eti Chato kinajengwa chuo cha Veta, kwa sababu Dr Kimei yuko kimaendeleo na siyo umbea umbea amesisitiza mchungaji.

Mchungaji Erasto amemalizia kwa kusema ni vema wananchi waandae mikutano na wabunge wao kila mwezi kujadili maendeleo yao kama alivyokuwa akifanya Prof Jay pale Mikumi.

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Huyo mchungaji anachunga mifugo ya kiongozi gani huko geita?
 

Nziiri

JF-Expert Member
Jul 23, 2020
448
500
Maamuzi ya maendeleo hufanyika bungeni!
Hiyo ni nadharia tu. Mbunge kazi yake ni kupeleka maoni/mahitaji ya wananchi. Serikali-(serikali za mitaa/halmashauri) ndio hupanga mipango ya maendeleo kisha serikali (hazina) kupeleka pesa ktk halmashauri kwaajili ya utekelezaji. Kwa hiyo nafasi ya mbunge ni kushiriki ktk baraza la madiwani kuainisha mahitaji, kisha wataalam wa halmashauri hutengeneza bajeti, nakuomba pesa serikalini kwaajili ya utekelezaji. Pale bungeni serikali inapeleka bajeti (mgawanyo wa fedha kwa halmashauri zote). Wabunge wanaijadili na kuipitisha. Kile ambacho kimeshapangwa na serikali mbunge hana nafasi ya kubadilisha. Kwa kifupi serikali ndio muamuzi halmashauri ipi ipate nini ja ipi isipate/isubiri. Sasa kutokana na propaganda za siasa wananchi wanadanganywa muulizeni mbunge wenu. Mbunge hana pesa. Ikumbukwe pia kauli ya rais kwamba 'msiniwekee gunzi tochi haitawaka'. Alimaanisha mkichagua mbunge/diwani wa upinzani hatawaletea maendeleo. Maana yake yeye ndio ana uamuzi wa mwisho kuhusu miradi ya maendeleo. Sasa wabunge wote ni ccm, ile propaganda kwamba Chadema wanazuia maendeleo haitumiki tena zigo anaangushiwa mbunge. Ingefaa pia kujiuliza je mgunge wa chato ndiye ana ujuzi/uwezo zaidi wa kuidhawish serikali kuliko yule wa kongwa? kuliko wa ruangwa? kuliko wa maeneo yote yenye umasikini uliokithiri, na ni ngome za ccm ambako elimu/uelewa ni kiwango cha chini kiasi cha kuamini nyerere yuko hai mpaka leo? Kwa kifupi nchi hii kwa sasa kumekua na ubaguzi na upendeleo mkubwa ktk matumizi ya rasilimali mali zilizopo kwaajili yamaendeleo. Sasa tunaweza kuhesabu miradi inayotekelezwa chato- international airport, hospitali ya rufaa, veta, taa za barabarani, msd kanda, uwnja mkubwa wa michexo, mbuga ya wanyama, madaraja, mabenki nk. Hebu tukaribu kuhesabu miradi inayotekelezwa kongwa au ruangwa au majimbo megine- je kuna uwiano wa haki?
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,565
2,000
Basi ngoja na mimi nimbane mbunge wangu ili kanda ya kitovu cha utalii ihame kule chatu ije jimboni kwangu, au nasema uwongo jamani...
 

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
24,804
2,000
Duh aisee sielewi kiswahili siku hizi nasali Ibada ya kingereza tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom