Mchungaji: Chanzo cha Kuchoma Makanisa ni CCM kuingiza Kadhi Katika Ilani ili JK apite!!!!!!

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
Kuna Mchungaji ametoa Kauli kuwa Chanzo cha Kuchoma Makanisa ni CCM ambayo iliingiza kinyume cha Sheria kipengele cha Mahakama ya Kadhi ili wapate Madarak amwaka 2005. Amesema mtu wa kulaumiwa hapa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa (JK) ambaye aliomba kura kwa Wananchi kwa kutumia sera ya dini yake badala ya sera za vyama vya siasa.

Amewataka Waislamu na jamii ya Watanzania wapenda amani wasielekeze lawama kwa Waislam bali Waelekeze lawama kwa watawala walioingia madarakani kwa sera ya kuwagawa Watanzania kwa mfumo wa dini ili iwefundisho kwa watawala wanaotaka madaraka kwa kumwaga pesa katika nyumba za ibada.
Amewataka Maaskofu kutokuwa Wanafiki kwa kukwete kueleza ukweli juu ya Madhara yaliyoletwa na CCM kupitia Kipengele cha Mahakama ya kadhi bali wanapaswa kueleza ukweli hata kama watawala hao watatembelea Makanisa !!
Pando walilolipanda watawala sasa linaleta matunda na yafaa Waachie ngazi ili amani ipatikane.
Udini katika siasa ni Mbegu Mbaya kuliko hata maandamano ya kuutoa utawala na Msajili wa Vyama vya siasa anapaswa kuangalia vyama vilivyochocheo udini huu na kuchukua hatua
Source : Tz Daima pg 2 na Vyanzo vingine.
[h=2]Monday, October 15, 2012[/h] [h=3]JK ATUNUKIWA NISHANI YA JUU NA SULTAN WA OMAN[/h]
Picha ya Juu; Sultani wa Oman, Qaboos bin Said Al Said akimtunuku Rais Jakaya Kikwete, nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman kwa kiongozi wa nje, wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake Oktoba 15, 2012 kwenye kasri ya AL Alam jijini Muscat. wakati picha ya chini

Rais Kikwete akimpa Sultani Qaboos bin Said Al Said zawadi ya picha ya Tembo, kuonyesha utajiri wa maliasili uliopo nchini Tanzania
(Picha na Ikulu)

Posted by Khals at 9:40 PM Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
 
Mungu ibariki tanzania haya mambo enzi za mwalimu hayakuwepo wala kwa mkapa,kaja jamaa watu wanataka mahakama ya kadhi kumbe kuna maagano enhee sema sema
 
kwani wao si ndo walimkampenia 2005 na kusema ni chaguo la mungu?
Au walifanya kampeni bila kusoma ilani?
 
Kikwete alijua kabisa kuwa hana uwezo wa kuwapa waislamu Kadhi,kilichomfanya aweke katika ilani ya mwaka 2005-2010 ni hiki ambacho yeye na washirika wake walijua kitatokea maana mwaka 2010 walipoamua kulitoa suala hilo kwenye ilani yao ilikuwa ni kugeuka ili kupata kura za upande mwingine,sasa mambo yote haya yanatugharimu wakati wao wamekaa kimya huku wakifaidi jasho letu bila wasiwasi.
 
Huyo mchungaji amesema ukweli nusu nusu!!
Kwanini wakristo hawakuhoji hilo wakati ule na badala yake viongozi wa kikristo wakawapofusha macho waamuni wao kwa kudai Kikwete ni ''Chaguo la Mungu''?
 
Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa.

Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini.

Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana.

Tunawataka wakiristo na watanzania wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa (M4
C).

Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo na watanzania wote wapenda amani tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia za kuleta mabadiliko za kweli.
 
waginga ndio waliwao,huuu ndio ujinga wa Watz, wakidanganywa kidogo tu wanakubali harafu, hawaachi kulalamika, mifano ni mingi nahatujifunzi. Angalia vigogo walivyopanga watoto wao na ndugu zao, najiuliza hawa hujipigia kura wenyewe????, wapumbavu hawalioni hili na bado wawachangua ile waendelee kuwalaani.

ukombozi utakuja lakini kivile kama tulivyo pata uhuru. jasho lazima litoke ili akili nanidhamu za watu zilejeshwe.
 
ni lipi jema sasa kufanyika, pamaoja na mambo yote yanayotendeka, utumiaji wa dini kama kigezo, uvunjwaji wa amani,? huku wakristo wakisali na kuomba, waislam ndo tu wanaonekana kupata nguvu ya ziada juu ya sheria, kwa kutumia imani yao. huku imani ya wakristo ikiwakataza kulipiza kisasi, kufanya ubaya kwa ubaya. lipi lililo jema kufanyika katika kipindi hiki cha machafuko
Mungu ibakiriki Tanzania
 
its too late... kichatokea inabidi serikali makini ndo ipitishwe mwaka 2015 ili tuondokane na udini...ni wazi kabisa kwamba sera kuu ya CCM ni kuendeleza UMASIKINI, UJINGA na UDINI miongoni mwa watz maana hizo ndo mtaji wao wa kisiasa...angalia CUF zamani..ati chama cha waislamu CHADEMA ati chama cha wakristo wao ni wapagani nini??? CCM haifai sita fanya osa tena kuchagua ccm hata mjumbe wa nyumba kumi..ni waginga kweli kweli wanaleta matatizo kwenye nchi yetu
 
Kikwete kuna wakati alishasema ilani ni ya CCM,waliiandaa wakamkbidhi yeye kama mgombea akimaanisha kwamba hatawajibika kwa yote yaliyoko kwenye ilani kwani yeye sie mwaandaji wake.

Pia naomba kueleweshwa mahakama ya kadhi iko kwenye ilani,au na ahadi ya Kikwete mwenyewe
?
 
NINACHOFAHAMU:- DINI SIYO MSINGI WA MAISHA
1-Nchi yetu(TZ) haina dini ila raia wake; nchi haiongozwi kwa misingi ya dini-point.
2-Kila mtanzania anaruhusa ya kuchagua kwa hiari yake dini anayoitaka.-point
3-Kila mtanzania ana uhuru wa kueneza dini yake kwa wengine ilimradi tu asivunje sheria za nchi, kwa kutumia nguvu, kulazimisha wegine wajiunge na dini yake na kuvuruga amani.-point
4-Kila dini iliyoko hapa nchini ina haki sawa na dini nyingine; hakuna dini ya kulazimisha kuwa ndiyo bora kuliko nyigine, bali katika sera zake iwaachie watu waichague wenyewe kwa hiari yao.-point
5-Siyo lazima kila Mtanzania awe na dini, bali akae katika misingi ya sheria za nchi hii, zilizo halali.-point
6-Kila Mtanzania kwa njia moja au zaidi amepokea dini ambazo siyo asili ya nchi hii.-point
7-Serikali inao wajibu wa kuhakikisha amani ya nchi yetu inadumu, la sivyo lazima iwajibishwe na wananchi wastaarabu.-point
8-Tusikubali WAENDAWAZIMU ama kutoka nje ya nchi au ndani ya nchi kutumia dini kutuvurugia amani. Amani ni haki ya kila Mtanzania.-Point
9-Dini yoyote, haipaswi kulazimisha sheria zake kuongoza nchi yetu; hii italeta vurugu. -point
10-Dini moja inapokuwa na waumini wengi zaidi ya dini nyingine, kamwe haipaswi kupora uhuru wa wale wachache wasioiamini dini hiyo, huo utakuwa ni uonevu.-point
11-DINI YOYOTE HAIPASWI KUTANGAZA KUSHIKA DOLA-HUO NI UDIKTETA, UKANDAMIZAJI na KUTOKUJALI HAKI ZA WENGINE.-Point
12-DINI SIYO SERIKALI-Hakuna ulazima wa kila mtu kufuata sheria za dini fulani.-point
13-Serikali yetu inapaswa kumtetea na kumlinda mtu yeyote, anayetaka kuihama dini yoyote ama anataka kuwa huru au anataka kujiunga na dini nyingine. KAMA MTU ANAVYOAMUA KUJIUNGA NA DINI FULANI KWA HIARI YAKE, VIVYO HIVYO ANAKUWA HURU KUIACHA DINI HIYO WAKATI WOWOTE APOGUNDUA KWAMBA DINI HIYO HAIMFAI-Point
14-Hatupaswi kuiga mfano mbaya wa chi za nje, zilizojitangazia kuwa na DINI RASMI na kuwanyima baadhi ya raia wake uhuru wa kumwabudu Mungu wanayeona anawafaa.Nchi hizo bado zimeweka watu wake utumwani.-Point
15. Kila Dini inapaswa kutumia Msahafu wake katika kujitangaza. Namna yoyote ya kutumia msahafu wa dini nyigine na kukashifu ni uchokozi wa wazi.-Point
16-KILA KIONGOZI WA NCHI HII ANAPASWA KUAMINI UWEPO WA MUNGU NA HIVYO KUIOGOPA HUKUMU YAKE; BILA KUIEGEMEZA NCHI KATIKA MISINGI YA DINI FULANI, HATA KAMA NDIYO DINI YAKE.-Point
17-Kwa mambo haya tutadumisha amani.-Point
Mwisho: MAISHA YALIKUWEPO KABLA YA DINI; NA BILA DINI MAISHA YATAENDELEA
 
Umesahau Point Moja muhimu saaaanaa... nayo ni uvumilivu baina ya wananchi wenye tofauti za imani. Katika dunia hii
ambayo binadamu anaendelea kudai na kupata uhuru (Ukiwamo uhuru wa maoni kutoa na kupata habari), zama hizi za
mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano tutaendelea kusikia maoni ya watu wengine ambayo yanapingana
na imani zetu au hata kuchukiza...lakini ili kumuhakikishia binadamu uhuru ni lazima tujifunze kuvumilia maoni ya wengine.
 
Huyo mchungaji amesema ukweli nusu nusu!!
Kwanini wakristo hawakuhoji hilo wakati ule na badala yake viongozi wa kikristo wakawapofusha macho waamuni wao kwa kudai Kikwete ni ''Chaguo la Mungu''?

Hivi hili tamko lilitolewa na jumuiya za kikristo au mtu binafsi ambaye alitumia uhuru wake kutoa maoni yake? Tena wazo hili liwe fundisho kuwa wakristu huchagua mtu bila kuzingatia dini yake.
 
Nafarijika sana ninaposoma mawazo ya watanzania wenye upeo wa juu na wapenda amani. Hakika hii si vita ya uislamu kama ambavyo baadhi ya watu wanavyotaka iaminike. Uislamu hauna ugomvi wowot na ukristo toka zama hizo. Tatizo ni serikali yetu imeandaa mazingira haya kwa manufaa yao binafsi. Nawakumbusha tu viongozi wetu wa serikali damu ya watanzania itawahukumu. Nawaomba sana watanzania wenzangu akili zetu zifanye kazi ya ziada vinginevyo tutaingia katika machafuko makubwa mno muda si mrefu. Hongera sana wakristo kwa kulitambua hili pia waislamu hongereni kwa kung'amua mtego huu. Tutafakari madhara ya vurugu hizi, bila amani hakuna dini yoyote itakayokuwa na nafasi. Hivi ni kwanini tunaidhalilisha Tanzania mbele za Mataifa? Mungu inusuru nchi yetu. Naipenda sana Tanzania! naipenda Afrika.!
 
Back
Top Bottom