Mchungaji awashauri wenye UKIMWI wasiache dozi kwa kisingizio cha kuokoka

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,645
2,000
WATU walioambukizwa Virusi vya UKIMWI (VVU) na wenye maradhi ya Ukimwi walioanzishiwa dozi ya ARVs na baadaye kuamua kuokoka, wameshauriwa kutokatiza dozi zao kwa imani ya wokovu, kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuwasababishia madhara zaidi kiafya, kabla ya kufikiwa na uponyaji wa Mungu.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ibada mbalimbali kanisani Karmeli Deliverance Ministry International (KDMI), Tangibovu-Mbezi Beach, Dar es salaam hivi karibuni, Mchungaji na Nabii Dk. Enock Mwasambogo alisema, kutupa ARVs ni imani iliyopita kiasi, ambayo, kama mwonaji na mshauri wa kiroho hamuungi mgonjwa yeyote kuivaa hata kama ameokoka.

Kwa mujibu wa Dk Enock, ARVs haziwezi kumponya mwenye UKIMWI wala kumuondolea VVU aliyeambukizwa, bali zinampunguzia makali ya maradhi hayo na kumfanya aonekane mwenye afya na matumaini wakati wote anapokuwa kwenye maombi akiutafuta uponyaji wa Mungu.

Dkt. Enock alisema: “ Ukimwona mgonjwa wa UKIMWI aliyeokoka anatupa ARVs zake wakati hajapokea uponyaji mwambie asiige yasiyoigwa, na wala asijaribu kuonyesha kuwa na imani zaidi hata ya Yesu mwenyewe.

Alisema kwa sababu wakati wa uponyaji unaamuliwa na Mungu mwenyewe kwa kadri apendavyo, mtu kutamka kuwa ameokoka, kuhudhuria kanisani kwenye maombi na maombezi na kuamini katika miujiza ya uponyaji hakumaanishi kuwa ni lazima apone muda huo.

Kutokana na ukweli huo, alisema ili mgonjwa asijishindwe kwa kuchoka mwili kutokana na kukongoroka na p engine kushindwa kumaliza safari ya kuutafuta uponyaji kanisani ni vyema akaendelea kumeza dawa zake kwa utaratibu ufaao na si kuruka dozi.

“Hakuna mahali Mungu alipokataza watu waliookoka wasiende hospitali au wasitibiwe, ndio maana tunahubiri na kuwashauri wagonjwa wanaokuja kanisani wahakikishe hawapuuzi ushauri wa madaktari wakati uponyaji wa Mungu ukiendelea.”

“…Wengi wanakufa kwa imani ambazo hata Mungu mwenyewe haziungi mkono. Una malaria, unapewa dawa kunywa umalize dozi usitupe eti kwa kuwa umeokoka, ukicheza utakufa na tutakuzika,”alisema na kuongeza kuwa mambo ya rohoni yafanyiwe kazi kiroho na ya mwilini yafanyiwe kazi kwa njia bora za mwilini ili Mungu naye ayabariki.
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
9,217
2,000
Kumbe Yesu haponyi tena!

Kuna mgonjwa mmoja kutoka "Mashahidi wa Yehova" hataki kabisa kuongezewa damu eti haruhusiwi, anahitaji operesheni ila damu haitoshi lakini hataki kusikia!
 

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
2,118
45
Huyo mchungaji namuunga mkono sana kuna kifungu kwenye bible kinasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hapa ndio mahali pake.
Miaka takribani 20 iliyopita mwingereza mmoja wa kanisa la YEHOVA aliugua akataka kuongezea damu akapinga akasema imani yake inakataza kuongezewa damu maana uhai uko kwenye damu kweli yule mgonjwa alikufa.
Mama mmoja wa hapa nchini kwetu alikuwa dr by profession alikuwa anafanya hospitali binafsi alikuwa anapinga sana mtu kuongezea damu hata kama kaugua malaria kwa imani hiyo hiyo utawala ulimgundua kwa kweli walimfukuza kazi.
Madhehebu mengine wanahubiri watu wasitumie dawa za mitishamba kisa ni ushirikina wanashindwa kujua asilimia 90 ya dawa zote zinatokana na mimea mfano quinine inatokana na mmea wa cinchona na penicillin inatokana na uyoga n.k
Pombe kweli ni haramu kwa dini nyingi lakini ukweli kuna dawa zingine zinawekwa alcohol kidogo kama matrix.Ili kitu kiwe alcohol lazima kiwe na R-OH yaani methyl group lililojishikiza na OH group.Hata vitakasa mikono vya CORONA unaambiwa vinatakiwa view na asilimia 68 ya ethanol ambayo tayari ni pombe.
Siungi mkono unywaji wa pombe ila nia yangu ni kuwaasa watu tuabudu mungu wetu kama kawaida lakini tutumie pia akili kujua kibaya na kizuri na kipi mungu hapendi
 

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,444
2,000
Kumbe Yesu haponyi tena!

Kuna mgonjwa mmoja kutoka "Mashahidi wa Yehova" hataki kabisa kuongezewa damu eti haruhusiwi, anahitaji operesheni ila damu haitoshi lakini hataki kusikia!
Yesu hajaacha kuponya. Tusimpangie njia gani atumie kuponya. Anaweza kutumia dawa za hospitalini kuponya. Kumbuka madaktari wanatibu ila aponyaye ni Mungu. Madaktari wapo duniani kwa mpango wa Mungu pia. Na kazi yao ni njema sana.


Hao wanaijiita mashahidi wa Yehova ni watu wa imani potofu. Usiambatane nao.

hakika KRISTO YESU ni Bwana na Mwokozi!
 

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
2,118
45
ila kuna lile dhehebu kubwa sana duniani na tajiri huwa linapinga sana uzazi wa mpango na matumizi ya condom huwa nawashangaa sana hawa watu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom