Mchungaji atupwa jela kwa kukataa kuapa mahakamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji atupwa jela kwa kukataa kuapa mahakamani!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Feb 7, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  MCHUNGAJI wa Kanisa la EAGT lililo Mtaa wa Ichenjezya kwenye mji mdogo wa Vwawa mkoani Mbeya Simon Kitwike, 48, amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukataa kuapa mahakamani kutokana na imani ya dini yake.

  Mchungaji huyo, ambaye alifika mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi katika kesi ya wizi kwenye nyumba yake iliyovunjwa mwishoni mwa mwaka jana na kuibiwa mali kadhaa, aliishangaza mahakama baada ya kukataa kuapa kabla ya kuanza kutoa ushahidi wake.

  Hakimu wa mahakama ya wilaya, Kajanja Nyasige alimtaka asome kifungu katika Biblia kinachomtaka asiape mahakamani, ndipo mchungaji huyo alipofungua kitabu hicho kitakatifu na kusoma Mathayo 5: 35 akisema mistari hiyo ndiyo inayompa msimamo huo.

  Mstari huo ambao alisema unamzuia unaanzia Mathayo 5:34 na kuendelea hadi 5:35 na unasema:

  "Lakini mimi nawaambia, usiape kabisa; hata kwa Mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yaje; wala kwa Yerusalem, kwa maana ndio mji wa Mfalme Mkuu."

  Baada ya kusoma kifungu hicho, Hakimu Nyasige alimuuliza tena mchungaji huyo kama alikuwa tayari kuapa ili aweze kuendelea na kutoa ushahidi wake mahakamani, hata hivyo mtumishi huyo wa Mungu aliendeleza msimamo wake wa kukataa kuapa.

  Kitendo hicho kilifanya hakimu huyo kumsomea kifungu cha sheria na 198 (1) kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 kinachokataza mtu kudharau mahakama na kumwambia kuwa kuendelea kukataa kuapa ni kuvunja sheria na hivyo anatenda kosa la jinai.

  Hata hivyo, Hakimu Nyasige aliendelea kumvumilia mchungaji huyo ili aweze kubadili msimamo wake kwa kumwamuru asome Biblia hiyo tena katika kitabu cha Warumi 13:1- 5, lakini baada ya kusoma kifungu hicho, mchungaji huyo hakubadili msimamo wake na hivyo kumpa mwanya Hakimu Nyasige kutoa hukumu yake.

  Hakimu Nyasige alisema anamtia hatiani mchungaji huyo kutokana na kosa la kuidharau mahakama na hivyo kumhukumu kwenda jela miezi sita na kuwa atatakiwa kurufi mahakamani kutoa ushahidi wake kwa kesi ya msingi Machi 2.

  Akiongea na Mwananchi, mchungaji aliyejitambulisha kwa jina la Mwakasaka alisema amepokea hukumu hiyo kwa masikitiko na mshangao mkubwa kwani mchungaji huyo amenukuu vibaya Biblia, akisema kuwa kitabu hicho kinakataza mtu kujiapiza yeye mwenyewe lakini inaruhusiwa kuapishwa kwa mamlaka iliyo ya duniani.

  Matukio ya waumini wa madhehebu kupingana na sheria yamekuwa yakitokea mara kadhaa wilayani hapa. Wanafunzi wa madhehebu ya Mashahidi wa Yehova wamekuwa na mgogoro na serikali kutokana na kukataa kuimba Wimbo wa Taifa shuleni.

  Pia wakati fulani mgonjwa aligoma kuongezewa damu na kuna wakati wanafunzi sita waligoma kufanya mtihani wa darasa la saba kutokana na imani ya dhehebu lao.

  Habari hii nimeipata kutoka Gazeti la Mwananchi.

   
  Last edited by a moderator: Feb 7, 2009
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  It is shame and sad to see the judge maliciously abused his privilege, and acted wanton disregard while knowing ethical beliefs are at par and/or above par with the law.

   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  Mchungaji ana makosa. He quoted scripture out of context. This is a big problem with under-educated and self appointed religious leaders.

  Hakimu anaadhibu wavunja sheria wote, kwa kufuatia sheria za Tanzania. Kama sheria inasema mtu aape, basi hakuna mtu kujikita kwenye uelewa mbaya wa Biblia na apone.

  Umefanya sawa kabisa Mheshimiwa Hakimu. Ubarikiwe sana.
   
 4. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu Augustine Moshi,

  Hawa ndiyo akina Kibwetere, iko haja ya UwT iangalie sana watu kama hawa la sivyo...
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,210
  Trophy Points: 280
  Mkuu Max Shimba, heshima mbele. Najua wewe ni muumini wa kweli. Yesu alisema 'mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari na mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu'. Mchungaji alipaswa kuapa japo hakimu ametoa adhabu kali pasipo sababu. Baada ya kukataa kuapa angeweza kuendelea kusikiliza ushahidi huo bila kiapo na kuupa uzito mdogo ushahidi huo. Angemhukumu kifungo cha kubaki mahakamani hapo mpaka jioni au angempiga fine.
  Kwa vile Mchungaji ni mtu wa imani kali, hebu fuatilia mambo ya Paulo na Sila yatakamtokea akiwa gerezani.
   
 6. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwani lazima kuapa? Ni sheria gani inayolazimisha mtu kuapa? Je kama mimi ni mhindu, nitaapia kitabu kipi? Au kama ni rastafarian, nitaapia kitabu kipi? Au kama ni atheist, nitaapia kitabu kipi?

  Mahakimu kama hawa ndio waliomhukumu kifo mbwa kwa kuitwa immigration. Uonevu mtupu.

  Amandla....
   
 7. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Hebu tuangalie mfano wa Nebuchadnezza, yeye kama mfalme, aliweka mswada na kuwa sheria kwa kila mtu aliyekuwa Babylon, kusujudu sanamu; Je kwa wanaoamini Mungu wa Kweli kama, Shedrack, Meshack and Abedneggo et al, kugoma kwao kumpa kaisari kusujudu sanamu kwasababu za kiimani, kulikuwa ni makosa?


   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,997
  Trophy Points: 280
  biblia inasema itiini mamlaka iliyowekwa na serikali, sasa basi kabla hakimu ajakuapisha anakuuliza wewe una imani na dini gani, kama ni mkristo na unaamini biblia basi shika biblia na uthibitishe hayo utakayoyasema mahakamani yatakuwa ya ukweli na shahidi wa hayo ni mungu aliye ndani ya kitabu ulichokishika na kama huna dini basi kuna jinsi ya kuapa,
  tatizo kubwa linaloface dini za sasa ni ukosefu wa uelewa wa maandiko matakatifu, kuisoma biblia na kukariri mistari hakukufanyi uwe mwelewa wa maandiko,
  hiyo na nebukadreza ni kitu tofauti sana na hiyo ya mahakamani, nebukadreza alikuwa anawalazimisha wamwache Mungu wao na kumwabudu baali, lakini hapa hakimu anamwapisha mchungaji na shahidi akiwa Mungu wake anyemwamini ni heshima kubwa sana hii
   
 9. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hoja yako ni hafifu sana, kutii mamlaka siyo kufanya kila kinachoamriwa. Biblia inasema kila jambo lipimwe kama linaendana na maandiko ndiyo unalitii kama linapingana na maandiko unaachana nalo hata kama limeamriwa na askofu/rais/mahakama etc.

  Hata hivyo kuapa mahakamani si lazima.
   
 10. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  I wonder if some of you have ever read this verse that brohibit to give oath at all, ad infinitum, or are just writing/post replies to be seen on JF, it is shame and sad.

  Matthew 5:34 (King James Version)

  34. But I say unto you, Swear not at all; neither by heaven; for it is God's throne:

  How arduous is it for someone not to understand a simple sentence like "SWEAR NOT AT ALL?"

  The court and/or the judge has no jurisdiction and/or there is no case law that supports the malicious act of the judge and/or there is no reason in fact or in law that supports the malevolent verdict of the judge, rather than acting wanton disregard, while conciously and knowingly that you can not inforce a law that does not exist.

  Unless someone post a case law that supports the malevolent decree given by the judge, I will conclude that the judge abused his/her privilages, and futhermore, the judge acted wanton disregard, to wit.
   
  Last edited: Feb 7, 2009
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Habari ndio hiyo ,huyu Mchungaji kakataa kuapa kuwa atasema kweli , kweli tupu na Mngu amsaidie.
  Kimsingi ni kusema ataongea kweli tupu na akisema uongo kweli itamhukumu.
  Sasa huyu Mchungaji uelewa wake ni mfupi sana.
  Angejua tu , serikali nayo kupitia sheria inaheshimu sana dini, kiapo ni msingi wa kutengeneza ukweli katika kesi yenyewe, yeye anakataa sasa aeleweke vipi?
   
 12. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2009
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It only reminds me of a story I read on newspapers that some years back seventh day faithful students at SoKoine University of Agriculture were discontinued simply because they refused to write exams after sunset on a friday! However, I hear their church incurred cost to educate them abroad! Blessing in disguise! I am of the views that the pastor narrowly interpreted the bible! There are many verses in the bible and I dont support sticking to a single verse to justify our deeds! BUT, the magistrate maliciously sentenced him to a long term in jail? What if he ignored him and his evidence. A witness or defendant at times do not turn up and that prevents not the hearing and ruling of the case!!!! Six months? Malicious.
   
 13. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160


  Actually...if you read the bible....God commands us not to swear to anything. A true Christian knows that when they say in court " Do you swear....." the response should be, " I give my word."


   
 14. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  In the Scripture we are told that no doctrine is of any private interpretation, which means that all valid doctrines are established by several different passages and verses that are all contextually addressing the same issue in the same way.

  Perhaps if we examine what the Scripture does state about guaranteeing future behavior, and guaranteeing our words, we might have a better understanding of what our real condition is. Moreover, we might get a little more humble about how wonderful we think we are as individuals. We also might gain a better understanding of why it is the LORD made certain it was declared in His word.

  In understanding why this is, we should note that a vow is the same a swearing that one will fulfill a promise, either in word or deed. Which means that people are going to look at you funny if you refuse to swear in court, or upon entrance in government service. (By the way, just how many government officials have broken their oaths of office?) Whether people consider one odd or not, is not the issue here. What is the issue is why we should, or should not swear, and what God does in response to someone swearing an oath – whether they are His child or not. However, to confirm or deny this doctrine, we need to go further, which brings us to the Gospel of Matthew and the words of the Lord Jesus Christ:

  Again, ye have heard that it hath been said by them of old time, Thou shalt not forswear thyself, but shalt perform unto the Lord thine oaths: But I say unto you, Swear not at all; neither by heaven; for it is God's throne: Nor by the earth; for it is his footstool: neither by Jerusalem; for it is the city of the great King. Neither shalt thou swear by thy head, because thou canst not make one hair white or black. But let your communication be, Yea, yea; Nay, nay: for whatsoever is more than these cometh of evil. (Matthew 5:33-37)

  Plainly, the Lord stated here that one should not swear at all – period. He gives a couple of examples of things we have no power to control, and tells us that if we have no power to control these things, we certainly ought not swear concerning future words and deeds. This is briefly confirmed in James, chapter five:

  But above all things, my brethren, swear not, neither by heaven, neither by the earth, neither by any other oath: but let your yea be yea; and your nay, nay; lest ye fall into condemnation. (James 5:12)


   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Huyo hakimu ni mshari tu, ana bahati sijabobea kwenye mambo ya sheria ..Ningekula naye sahani moja. Hakika Mwenyezi Mungu atamlipa kadr ya anavyostahili.

  Halafu watu acheni kimbelembele na kujifanya mnajua mambo, na kunukuu sehemu za Kitabu Pekee cha Uzima,huku mkiwa 'weupe'. Kwa kifupi huo mstari uliounukuu sio applicable ktk hii KADHIA. Ebo!
   
  Last edited by a moderator: Feb 8, 2009
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  UWT ni watu wachafu na wakae mbali na wachungaji wetu, period!
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Context ipi unayoizungumzia? Au ndo vile kuosha kinywa mpaka kitakate kama HIVI :D ?

  Kwa jinsi nilivyofuatilia habari ni kuwa Mchungaji hakuwa comfortable na kiapo na hakutaka kupelekwapelekwa. Sababu za kukataa kwake kiapo ninavoziona ni SAHIHI, kwa sababu hakutaka kumkosea Mungu wake. Kama alikuwa amepotoka alitakiwa aeleweshwe kwa UTUO ni si kwa jazba au ubabe.

  Mahakimu kama hawa mimi ningekuwa bosi wake nafuta kazi mara moja na vyeti vyake vyote namnyang'anya, maana hajui kuwa sheria ni kwa ajili ya KUISAIDIA JAMII na SIO KUIKOMOA.
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkulu Max,

  Hili ni tatizo la vi-pundit uchwara vya JF. Tuvisamehe tu mkuu Max, havijui vitendalo.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kuitii mamlaka is loose statement. Sheria ya kwanza kabisa ktk Ukristu ambayo ipo specific and precisely addresed ni kuwa KUMCHA BWANA MUNGU, KWA MOYO, AKILI, MWILI, NA YOTE ALIYONAYO MJA. Kama wewe ni mkristu hili halitakuwa gumu kwako kulielewa.

  It follows that, amri nyingine yeyote inayofuata inakuwa OVERWRITTEN na hii KUU. Mchungaji alinukuu sehemu ambapo M/Mungu amekata kuapa.

  Kwa hiyo basi, kimsingi wewe na wenzako hapa JF pamoja na hakimu wenu muflisi HAMNA HOJA.Period!
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Osha kinywa mwanangu mpaka kitakate..kama hivi :D
   
Loading...