Mchungaji atumia jina la Rais na la Mhe. Lwakatare kwa utapeli

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
676
•Mchungaji Lwakatare kizimbani kwa utapeli

MOROGORO

Na Ramadhan Libenanga

MCHUNGAJI Israel Lwakatare (63) wa Kanisa la Assemblies of God Madizini kata ya Boma mjini hapa amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujipatia sh. milioni 38 kwa njia ya udanganyifu akitumia jina la Rais Jakaya Kikwete na Mchungaji Getrude Lwakatare.

Akisomewa shitaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Bi Erodia Kyaruzi na Mwendesha Mashitaka Salehe Kalulu, mtuhumiwa huyo alidaiwa kutenda kosa hilo Novemba 7 mwaka jana katika maeneo ya hoteli ya Masuka akitokea Dar es Salaam na kuwahamasisha wananchi hao ambao wengi wao ni wanawake kuwa ametumwa na Rais.

Bw. Kalulu alidai kuwa mshitakiwa aliwadanganya wananchi kufungua SACCOS na kuwataka kuanza na hisa 10 zenye thamani ya sh. 100,000 kwa kila mwananchama wa SACCOS hiyo, yenye wanachama zaidi ya 254.

Alisema Mchungaji huyo aliyeanzisha SACCOS na kuipa jina la Fungamano la wajasiriamali, kwa kutumia jina la Rais Kikwete, alikusanya michango ya wananachi hao, ikiwa ni pamoja na kuwataka kuchangia sh. 50,000 kwa ajili ya mchango wa kilimo.

Mshitakiwa alikana mashitaka na kuiomba mahakama kumpa dhamana kwa kuwa alikuwa amefungua kesi dhidi ya wanachama wake kumtishia maisha.
 
Last edited by a moderator:
Bwana/Bi mtanzania, hapo wabunge wanhusikaje?

Ni jina la Lwakatare ndio linaleta tatizo? Nilivyielewa mimi ni kuwa huyo tapeli katumia jina la mh mBunge Rais kufanya utapeli
 
Bwana/Bi mtanzania, hapo wabunge wanhusikaje?

Ni jina la Lwakatare ndio linaleta tatizo? Nilivyielewa mimi ni kuwa huyo tapeli katumia jina la mh mBunge Rais kufanya utapeli

Kandambili,

Samahani, nimechanganya jina. Nilifikiri ni yule mama Lwakatare.

Apology kwa mama Lwakatare.
 
Hii habari imekaa kiudaku sana. kwani haimuhusu hata kidogo mh. mchungaji Rwakatare, ila kuna mtu katumia jina lake tu kutapeli.
 
Ufisadi mpaka makanisani.Alianza Mtumishi Mheshimiwa Nabii GeorDavie,Akaja Mtikila sasa Huyu.
Na Mchungaji Gertrude anaitwa Lwakatare ama Rwakatare?Na yule mbunge wa Bukoba kama Sijakosea naye ni Lwakatare au Rwakatare maana hizi Surnames zetu na tunavyozikosea!
 
Hiki kichwa cha habari hii kimenikumbusha habari flani iliyokuwa kwenye gazeti moja miaka ya nyuma ikiwa na kichwa cha habari "Waziri afumaniwa live!!" alafu ndani yake nikagundua kuwa ilikuwa ikimzungumzia mkazi wa Manzese Bw. Salim Waziri, wakati huo kimia mbili changu cha chips dume nshakispend kwa kununua gazeti!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom