Mchungaji atuhumiwa kumbaka mwaanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji atuhumiwa kumbaka mwaanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Apr 18, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,692
  Trophy Points: 280
  MMOMONYOKO wa maadili unaelekea kuiathiri jamii ambapo sasa baadhi ya viongozi wa dini wanazidi kuingia matatani kutokana na kushiriki katika vitendo vya ngono.

  Mchungaji wa kanisa la African Inland- (AIC) ambaye pia ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Chona, wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Pasia Dickson (36), ametuhumiwa kufumaniwa Jumatano akifanya mapenzi na mwanafunzi wa darasa la saba.

  Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Daudi Siasi amethibitisha tukio hilo akisema kwamba, mtuhumiwa ameshatiwa mbaroni na amefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kubaka na kushambulia.

  Siku ya tukio mwalimu huyo alikwenda nyumbani kwa mwanafunzi huyo na kufanya naye tendo la ndoa chumbani kwa mama wa mwanafunzi, ambaye wakati wa tukio hilo alikuwa amekwenda gulioni kununua mahitaji ya nyumbani.

  Naye Diwani wa Kata ya Chona iliyopo umbali wa kilomita zaidi ya 50 kutoka Kahama Mjini, Mabala Mlolwa amesimulia tukio akisema kwamba, alishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuyaokoa maisha ya mchungaji huyo.

  “Ni tukio la kweli, na mimi nimeshiriki katika kumnusuru kwa sababu baada ya fumanizi alijiokoa kwa kumng’ata kaka wa binti na baadaye alitimua mbio akiwa mtupu hadi kwenye ghala la kuhifadhia nafaka katika nyumba ya jirani. “Wananchi wenye hasira walitaka kummaliza huko huko ghalani, nikawasihi wasubiri polisi na kweli baadaye polisi walikuja kumchukua, mimi ndiye niliyemchukulia nguo, na sasa wanamshikilia …”

  Mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza kwamba, Mchungaji huyo alikuwa na uhusiano wa muda mrefu na mwanafunzi huyo. “Hata siku ya tukio, jamaa alikwenda akijua kabisa ratiba ya mama wa mwanafunzi, bila woga alikwenda na pikipiki akaiegesha nje naye kuzama ndani na hawara yake…

  “Kaka mtu ndiye aliyeshitukia mchezo mchafu wa mchungaji, kwani alipofika nyumbani alishangaa kuona pikipiki nje, baada ya kuingia ndani alimkuta mchungaji huyo katika kitanda cha mama yao akiwa utupu wakifanya mapenzi na mdogo wake mwenye umri wa miaka 16.

  “Ndipo katika kukurupushana huku mchungaji akitaka kutoka akiwa utupu na kaka mtu akijitahidi kumzuia kutoka huku akipiga kelele, mchungaji aliamua kumng’ata kaka mtu na kukimbia, lakini hakufika mbali kwa sababu hakuwa na nguo,” alisema Mlolwa. Kesi ya Mchungaji Dickson inatarajiwa kuendelea Aprili 30, mwaka huu.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  HATUJAKATAA WALA KUKUBALI......! kama tujuavyo zilivyo habari nyingi za upande mmoja, waweza kuta.....ALIWAHI KUWA MCHUNGAJI, NI MUUMINI MZURI WA KANISA HILO, KUITWA MTAANI MCHUNGAJI AU YEYE MWENYEWE KUJIITA MCHUNGAJI NA HAPA TWAAMBIWA NI MWALIMU WA SHULE YA MSINGI CHONA
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Acha utetezi usio na maana! Habari ndiyo hiyo na kwa taarifa yako huyp Pastor anastahiki kupigwa mawe hadi afe kwa vile alimnajisi mtoto wa Kiislamu.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Shida ya Pdidy ni "copy and paste expert"...Mi sitaki hata kuchangia hoja zake, maana anabandika kitu na kuwahi kwa mkewe, hachangii kitu!...
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hii kali! Mtoto asiye na dini au wa dini nyingine hapaswi kupewa haki?
  Mzinzi huyu atastahili kufa tu kwa vile aliyenajisiwa ni mtoto wa kiislamu?!!!
  Wonders will never cease!
   
 6. m

  mlaylucila New Member

  #6
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 17, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha!! Me nafikri hapa swala la udini tuliweke mbali, bali tuchukulie zaidi kile kitendo kilichofanyika. Si cha kiubinaada haswa kama hapakuwepo na makubaliano kati yao nalenga zaid kwa wale minor(under18).Hapa sheria chukue mkondo wake na kutenda haki kama ipasavyo bila kupendelea.
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yaa! That reflects the response in question! Ungeanza kushangaa kwa yule asiefahamu kuwa hili halina upadiri au ushehe bali ni ushetani. Nikitegemea zaidi ya mshangao wako! Hata hivyo hakuna pahala nilipoonyesha kuwa msichana hana haki, pengine wewe ulibaini hilo?
   
 8. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wengine huandika bila kufikiri Ngekewa. Mradi kaona kuna neno uislamu tu basi kosa.
   
 9. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  Eeh lazima huyu mchungaji afahamu kazi ya kuchunga kondoo wa bwana sio kama kazi nyingine za kutatua ukali wa maisha bali ni kazi ya kujitoa mhanga kwa kusalimisha maisha yako kwanza kwa Bwana Yesu. Sasa ubaya wa dini umefanya kazi za kanisa kuwa ajira ya kujipatia kipato na hivyo wamekaribisha kila aina ya ndege wachufu katika huduma za kitumishi. Wacha huyo mchungaji akumbane na mkondo wa sheria na afahamu kwamba nje ya Yesu, hata mbingu na nchi zitapokuwa zimeondoka haitatanguka nukta moja ya sheria(TORATI).
   
 10. stanluva

  stanluva Senior Member

  #10
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 7, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Eeeh! No Comment! Dunia hadaa Ulimwengu ....................
   
 11. M

  Muuza Maandazi Member

  #11
  Apr 18, 2010
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
   
 12. c

  capten New Member

  #12
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii sii Mchezo ...
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  pdidy jitete mkuu, yawezekana ikawa kweli - ha ha ha
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,692
  Trophy Points: 280
  hata kudesa umeshindwa

  SOMA HOJA YA MMOJA HAPO JUU ALIEKUWEPO...UTAONA SINA HAJA YA UTETEZI

  COURTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTT
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,692
  Trophy Points: 280
  safi sana si kila kitu kiko kuchangia jf
  ukiwa na tabia hizo utashangaa shemijio katoa hapa mada anavyoteswa na dadako
  ukaishia kuchangia mfukuze akirudi nyumban unalalama na vikao wakati umeshauri mwenyewe
  big up paka j
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sio kweli Bro! Niandikapo siku zote sikurupuki. Ushehe au Upadri kwangu nauweka katika ubinaadamu sawaq na sisi tusio mashehe au mapadri.
  Sasa mtu anapoingiwa na wasiwasi na habari zile tu ambazo katajwa Shehe au Padri na akuziacha habar nyengine withou benefit of doubts una muweka fungu gani huyo mtu? Kwa ufupi fuatilia hiyo thread bila kujali dini yako na utaona wapi kosa lilipo.
   
 17. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Aende jela miaka 30 akamtafute Mungu huko jela
   
Loading...