Mchungaji Anthony Lusekelo aibukia kwa Rais Magufuli aonya makanisa kutumika

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
321
346
NA MWANDISHI WETU
MCHUNGAJI wa Kanisa la GRC, Ubungo jijini Dar es Salaam Anthony Lusekelo amewashukia wagombea wanaotumia nyumba za ibada kusaka kura na kusema kuwa ni wagombea waliokosa mvuto wa kisiasa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji Lusekelo alisema, baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotumia nyumba za ibada kujinadi ni ishara ya kupoteza mvuto kwa wananchi.

Kiongozi huyo wa Kiroho alisema, Taifa linahitaji kupata mgombea anayenadi sera zake ambazo zitakubalika na wananchi na sio kutumia nyumba za ibada kutafuta kura.

Alisema kuwa Taifa alijajengwa katika misingi ya udini hivyo wananchi wanapaswa kuwaepuka wagombea wa haina hiyo.

“Hili Taifa halina dini na wala halihitaji mgombea anayetokana na dini fulani bali aliye na sera zinazokubalika…ukiona mgombea anatumia nyumba za ibada kutafuta kura huyo hana nguvu za kisiasa,” alisema.

HAMAHAMA

Mchungaji Lusekelo alionyesha kuchukizwa na baadhi ya viongozi wanaohama hama vyama vya siasa na kusema kuwa hatua hiyo inapoteza uaminifu kwa wananchi waliowachagua.

Hivi karibuni baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakihama vyama hivyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hatua inayosababisha kurudi katika uchaguzi mdogo.

, siasa sio uadui lakini kitendo cha baadhi ya viongozi kushindwa kusimamia kauli zao na kuamua kujiondoa katika vyama vyao vinapoteza uaminifu.

Aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanatumia vyama vyao na kuyasimamia yale wanayoyaahidi kwa wananchi kwa kuhimiza umoja, mshikamano na uzalendo.

“Kuhamahama sio shida lakini kwangu mimi nachukizwa na vitendo hivyo kwani inaonyesha wazi viongozi hao hawawezi kuyasimamia yale wanayoyaahidi,” alisema.

UCHAGUZI

Mchungaji Lusekelo alisema, kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa hauna tija ni kutaka kuihamsha na kulisumbua Taifa.

Alisema kuwa kuna sherehe nyingi Rais John Magufuli ameweza kuzifuta hivyo kama angeweza kumshauri kiongozi huyo uchaguzi huo ungesogezwa na kufanyika mwakani 2020 ili kupunguza gharama.

“Kama ningekuwa Waziri Mkuu au Waziri wa Tamisemi ningeshauri na kumuomba Rais awaache viongozi waliopo madarakani wa serikali za mitaa wakaendelea wao na uchaguzi tukaufanya mwaka 2020,” alisema.

Kiongozi huyo wa kiroho alisema, hatua hiyo itaweza kulifanya Taifa likaendelea kupumua na viongozi wakaendelea kusaidia kufikia maendeleo ya uhakika.

Kumkosoa Rais

Alisema kuwa sio maadili kumkosoa kiongozi wa nchi kihuni na kuwataka wale wanaokosoa kusubiri kiongozi huyo atakapoondoka madarakani watumie fursa hiyo kumkosoa.

Aliwataka wanaohitaji kukosoa kuwaachia wabunge ambao wanaweza kutumia muhimili huo kukosoa kwa weledi.

MABENKI

Mchungaji Lusekelo alimpongeza Rais Magufuli kwa kuamua kubadilisha mfumo na kuzirejesha fedha zote za serikali zilizokuwa zimehifadhiwa katika mabenki ya biashara.

Alisema kuwa hatua hiyo imesababisha mtikisiko kwa baadhi ya mabenki hayo na wananchi.

Akitolea mfano kufungwa kwa baadhi ya maduka ya kubadilishia fedha kwani imesababisha ugumu wa maisha kwa wananchi.

UJAMBAZI

Alimpongeza Rais Magufuli kwa kuwa na uongozi bora ambao ameweza kudhibiti matukio ya ujambazi hasa yale yaliyokuwa yakitokea mkoani Pwani.

Mchungaji Lusekelo alisema, kwa kipindi kifupi Rais Magufuli amesaidia usalama wa nchi kutulia na hata waliokuwa wakishirikia vitendo hivyo wamepungua.

ATCL

Mchungaji Lusekelo alisema, ni vyema watanzania wakamuacha Rais Magufuli aweze kufanya kazi kwa juhudi ili kuwaletea maendeleo.

Alisema kuwa hatua ya kiongozi huyo kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeonyesha namna alivyo na nia ya dhati ya kuleta maendeleo kwa Taifa.

“Tumuache Rais Magufuli afanye kazi kwani amefufua ATCL na kutuletea ndege nane na nyingine mbili ziko njiani zinakuja, sasa tunahitaji kiongozi wa aina gani,” alihoji.

MAADILI

Lusekelo aliwashukia watendaji wa serikali ambao wanashindwa kudhibiti mmomonyoko wa maadili unaoendelea nchi ambao inafikia baadhi ya viongozi wa kiroho wakidhalilishwa kwa kutolewa picha chafu.

“Hawa viongozi wanadhalilishwa inashusha heshima yao kwanza wao wana familia, wana waumini wanaowaongozi sio jambo jema kabisa kwa Taifa letu hivyo ni wajibu wa watendaji wa serikali kuchukua hatua kupambana na vitendo hivyo,” alisema.

Mwisho
 
Atakuwa mwehu huyu Lusekelo

Unamkosoa mtu hai ili ajirekebishe asiwapeleke kaburini

Deleva anaendesha vibaya tusimkosowe tusubirie mpaka tufike? Wapi akitupatisha ajali tukafa huo ukosowaji atafanya nani, kwa faida ipi? Maana tumeshapata ajali na tumekufa......hivi hii nayo akili?

Tusubirie rais atoke madarakani ndipo tumkosowe hii inafaidagani kwetu kama sio wazo la kipumbavu na kijinga.

Mawazo ya mtu mwehu na mwendawazimu
 
Hakuwahi kuwa na hekima wala busara zaidi ya ndumba za kuwavutia wasiojitambua kwenda kumsujudia badala ya kumwabudu na kumtukuza Mungu! Kaamua kumkampenia aliyeshindwa kujikampenia! Ama kweli chaguzi zijazo zinakwenda kuangusha mlima!
 
NA MWANDISHI WETU
MCHUNGAJI wa Kanisa la GRC, Ubungo jijini Dar es Salaam Anthony Lusekelo amewashukia wagombea wanaotumia nyumba za ibada kusaka kura na kusema kuwa ni wagombea waliokosa mvuto wa kisiasa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji Lusekelo alisema, baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotumia nyumba za ibada kujinadi ni ishara ya kupoteza mvuto kwa wananchi.

Kiongozi huyo wa Kiroho alisema, Taifa linahitaji kupata mgombea anayenadi sera zake ambazo zitakubalika na wananchi na sio kutumia nyumba za ibada kutafuta kura.

Alisema kuwa Taifa alijajengwa katika misingi ya udini hivyo wananchi wanapaswa kuwaepuka wagombea wa haina hiyo.

“Hili Taifa halina dini na wala halihitaji mgombea anayetokana na dini fulani bali aliye na sera zinazokubalika…ukiona mgombea anatumia nyumba za ibada kutafuta kura huyo hana nguvu za kisiasa,” alisema.

HAMAHAMA

Mchungaji Lusekelo alionyesha kuchukizwa na baadhi ya viongozi wanaohama hama vyama vya siasa na kusema kuwa hatua hiyo inapoteza uaminifu kwa wananchi waliowachagua.

Hivi karibuni baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakihama vyama hivyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hatua inayosababisha kurudi katika uchaguzi mdogo.

, siasa sio uadui lakini kitendo cha baadhi ya viongozi kushindwa kusimamia kauli zao na kuamua kujiondoa katika vyama vyao vinapoteza uaminifu.

Aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanatumia vyama vyao na kuyasimamia yale wanayoyaahidi kwa wananchi kwa kuhimiza umoja, mshikamano na uzalendo.

“Kuhamahama sio shida lakini kwangu mimi nachukizwa na vitendo hivyo kwani inaonyesha wazi viongozi hao hawawezi kuyasimamia yale wanayoyaahidi,” alisema.

UCHAGUZI

Mchungaji Lusekelo alisema, kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa hauna tija ni kutaka kuihamsha na kulisumbua Taifa.

Alisema kuwa kuna sherehe nyingi Rais John Magufuli ameweza kuzifuta hivyo kama angeweza kumshauri kiongozi huyo uchaguzi huo ungesogezwa na kufanyika mwakani 2020 ili kupunguza gharama.

“Kama ningekuwa Waziri Mkuu au Waziri wa Tamisemi ningeshauri na kumuomba Rais awaache viongozi waliopo madarakani wa serikali za mitaa wakaendelea wao na uchaguzi tukaufanya mwaka 2020,” alisema.

Kiongozi huyo wa kiroho alisema, hatua hiyo itaweza kulifanya Taifa likaendelea kupumua na viongozi wakaendelea kusaidia kufikia maendeleo ya uhakika.

Kumkosoa Rais

Alisema kuwa sio maadili kumkosoa kiongozi wa nchi kihuni na kuwataka wale wanaokosoa kusubiri kiongozi huyo atakapoondoka madarakani watumie fursa hiyo kumkosoa.

Aliwataka wanaohitaji kukosoa kuwaachia wabunge ambao wanaweza kutumia muhimili huo kukosoa kwa weledi.

MABENKI

Mchungaji Lusekelo alimpongeza Rais Magufuli kwa kuamua kubadilisha mfumo na kuzirejesha fedha zote za serikali zilizokuwa zimehifadhiwa katika mabenki ya biashara.

Alisema kuwa hatua hiyo imesababisha mtikisiko kwa baadhi ya mabenki hayo na wananchi.

Akitolea mfano kufungwa kwa baadhi ya maduka ya kubadilishia fedha kwani imesababisha ugumu wa maisha kwa wananchi.

UJAMBAZI

Alimpongeza Rais Magufuli kwa kuwa na uongozi bora ambao ameweza kudhibiti matukio ya ujambazi hasa yale yaliyokuwa yakitokea mkoani Pwani.

Mchungaji Lusekelo alisema, kwa kipindi kifupi Rais Magufuli amesaidia usalama wa nchi kutulia na hata waliokuwa wakishirikia vitendo hivyo wamepungua.

ATCL

Mchungaji Lusekelo alisema, ni vyema watanzania wakamuacha Rais Magufuli aweze kufanya kazi kwa juhudi ili kuwaletea maendeleo.

Alisema kuwa hatua ya kiongozi huyo kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeonyesha namna alivyo na nia ya dhati ya kuleta maendeleo kwa Taifa.

“Tumuache Rais Magufuli afanye kazi kwani amefufua ATCL na kutuletea ndege nane na nyingine mbili ziko njiani zinakuja, sasa tunahitaji kiongozi wa aina gani,” alihoji.

MAADILI

Lusekelo aliwashukia watendaji wa serikali ambao wanashindwa kudhibiti mmomonyoko wa maadili unaoendelea nchi ambao inafikia baadhi ya viongozi wa kiroho wakidhalilishwa kwa kutolewa picha chafu.

“Hawa viongozi wanadhalilishwa inashusha heshima yao kwanza wao wana familia, wana waumini wanaowaongozi sio jambo jema kabisa kwa Taifa letu hivyo ni wajibu wa watendaji wa serikali kuchukua hatua kupambana na vitendo hivyo,” alisema.

Mwisho
Eti tumuache afanye kazi?! Kwamba hiyo kazi anayofanya haituhusu au? Haturuhusiwi kuwa na maoni? Eti tusubiri atoke madarakani ndio tumkosoe?! Wakati huo tutakuwa tunamkosoa ili iweje?
 
Naungana naye kwa kuwaasa wale wanaowashwa washwa kutulia tulii, wamuache Rais Kipenzi cha watanzania awatumikie waliomtuma akawatumikie.
Mimi natofautiana naye anaposema wanaomkosoa rais wasubiri hadi atoke madarakani. Itakuwa haina maana kwani anakosolewa ili arekebishe pale inapowezekana kurekebisha.
 
Back
Top Bottom