Mchungaji amehukumiwa miezi 18 jera kwa kushindwa kupeleka watoto shule

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imemhukumu Mchungaji Merchades Mugishagwe kutumikia kifungo cha miezi 18 gerezani na kulipa faini shilingi milioni tatu, baada ya kumtia hatiani kwa makosa matatu.

Makosa hayo ni kushindwa kutekeleza wajibu wake kama mzazi, kushindwa kupeleka watoto shule na kujihusisha na vikundi visivyotakiwa kijamii.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Daniel Nyamkerya,pia amemhukumu mshtakiwa namba mbili katika kesi hiyo mke wa mchungaji huyo Agripina Maganja kutumikia kifungo cha nje kwa muda wa miezi sita kwa masharti ya kutotenda kosa katika kipindi hicho, kutokana na kutiwa hatiani.
 

Attachments

  • IMG_20210827_234022.jpg
    IMG_20210827_234022.jpg
    32.6 KB · Views: 1
Hapo kwenye kujihusisha na vikundi vya visivyotakiwa kwenye jamii ni kosa? je hivyo vikundi navyo vimechukuliwa hatua gani? je huvyo vikundi vilikuwa vinashughulika na nini?

Hayo makosa mengine ni ya kumuelewesha tu hayastahili kifungo na kwenye taarifa ya habari niliona kama alikubali kuwapeleka shule.
 
Mchungaji hayuko sawa
ni kweli hapo wala hawaja msaidia wala watoto wake pia alihitaji ushauri nasaha wa kiwango cha juu baadhi ya mambo ya kiimani ukiyabeba bila tafakuri ukaja na tafsiri potofu huharibu afya ya akili
 
Back
Top Bottom