Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,445
Mchungaji Mboro amefika mbele ya Kanisa la Mchungaji Lukau na kumuomba Mungu awasamehe wachungaji wote waongo huku akisema amefika kanisani hapo kwa sababu anaona injili ya Mungu inachezewa huku akimtaka kama kweli ana uwezo wa kufufua basi amfufue Muasisi wa Taifa hilo, Nelson Mandela.
“Nimefika hapa kujua ukweli, hii miujiza ni uongo na kama si uongo nipe kidhibitisho, wacha tuongee kama watu wa Mungu, hii siyo sahihi, kwa niaba ya wachungaji wote na watu wa Mungu, waongo wote tusamehe,” amesema Pastor Mboro huku akiwa pembeni ya gari lake la kifahari BMW i8.