Mchungaji ‘aliyeji-selfie na Mungu’, amtaka mchungaji Lukau amfufue Nelson Mandela

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
maxresdefault-2-1024x576.jpg
MCHUNGAJI mmoja nchini Afrika Kusini, Paseka Motsoeneng, maarufu kama Pastor Mboro, ambaye alishawahi kudai kuwa alifika mbinguni na kupiga picha na Mungu (kwa kutumia simu – ‘selfie’) amempa changamoto mchungaji mwenzake raia wa Congo DR, Alph Lukau, anayeishi nchini humo ambaye hivi karibuni alijinasibu kumfufua marehemu.


Pastor-Mboro-1024x768.jpg



Mchungaji Mboro amefika mbele ya Kanisa la Mchungaji Lukau na kumuomba Mungu awasamehe wachungaji wote waongo huku akisema amefika kanisani hapo kwa sababu anaona injili ya Mungu inachezewa huku akimtaka kama kweli ana uwezo wa kufufua basi amfufue Muasisi wa Taifa hilo, Nelson Mandela.


55b7348c88684d51a59f1910f9fc0c4e.png






“Nimefika hapa kujua ukweli, hii miujiza ni uongo na kama si uongo nipe kidhibitisho, wacha tuongee kama watu wa Mungu, hii siyo sahihi, kwa niaba ya wachungaji wote na watu wa Mungu, waongo wote tusamehe,” amesema Pastor Mboro huku akiwa pembeni ya gari lake la kifahari BMW i8.
 
Wote hao manabii wa uongo. Ulokole umekuwa chanzo cha vurugu kubwa katika ukristo ni vigumu kujua nani ni nani siku hizi.
 
Hahaa hilo jina tu .. linaonyesha kwamba waumini wake wa jinsia Ke hawako salama ... aise mke wangu marufuku kwenda kusali kwenye kanisa la huyo mchungaji ....(pastor mboro )

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom