Mchungaji akamatwa kwa kuzidisha muda wa mahubiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji akamatwa kwa kuzidisha muda wa mahubiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 6, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Mchungaji akamatwa kwa kuzidisha muda wa mahubiriMwandishi Wetu, Singida

  JESHI la polisi mkoani hapa, linamshikilia mchungaji Nelson Andreson Mazengo maarufu kwa jina la Muyahudi (36) mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es salaam na wenzake wawili kwa tuhuma ya kuendesha mhadhara wa dini nje ya muda ulioainishwa kwenye kibali.

  Watuhumiwa wengine ni mchungaji Edward Sugi Gwau (55), mkazi wa Mitunduruni na mwinjilisti Jonathani Mfaume(36), mkazi wa Kibaoni mjini hapa.

  Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa, Celina Kaluba, alisema watuhumiwa hao, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.

  Wachungaji hao waliendesha mhadhara wao kwenye viwanja vya Ipembe mjini hapa, na kwamba walikamatwa juzi saa 12.07 jioni na kwamba wahubiri hao, walipaswa kumaliza mkutano saa 12.00 juu ya alama lakini waliendelea na mkutano baada ya muda huo.

  Baada ya muda huo kumalizika huku wakiwa bado wanaendelea na mahubiri, wachungaji hao walikamatwa na polisi na kupelekwa kituo cha kati na kufunguliwa mashitaka ya kukiuka makubaliano yaliyoko kwenye kibali.

  Kundi kubwa la waumini waliokuwepo kwenye mhadahara huo, baada ya kuona viongozi wao wamekamatwa na polisi, nao mara moja waliandamana huku wakiimba nyimbo za kuhamasishana hadi kwenye viwanja vya kituo hicho.

  Walidai kuwa wiki mbili zilizopita, waumini wa kiislamu walikuwa wakiendesha mhadahara mara mbili na wa kwanza ulikuwa ukianza saa 9.00 hadi saa moja jioni na kufuatiwa na mwingine uliokuwa ukiambatana na onyesho la sinema kuanzia saa 2.00 mchana hadi saa 4.00 usiku, lakini hakufanyiwa vurugu na polisi.

  Kamanda Kaluba, alisema jeshi hilo halina kabisa upendeleo wa aina yoyote kwa dhehebu lo lote, ila kila atakayekiuka makubaliano yanayoainishwa kwenye kibali cha kufanya mhadhara, atachukuliwa hatua kali za kisheria. Kundi hilo, lililokuwa limekusanyika kwenye kituo hicho cha polisi, kilitawanyika baada ya kufukuzwa huku wakichahapwa mikanda na askari polisi wa kuzuia fujo (FFU).
   
 2. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #2
  May 6, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kuzidisha dakika saba unakatamatwa na kupelekwa mahakamani?????!!!!!!!! hizo nguvu si wazipeleke kwa akina Rostam Aziz? MIS USE OF PUBLIC FUNDS.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  kuzidisha dakika saba unakatamatwa na kupelekwa mahakamani?????!!!!!!!! hizo nguvu si wazipeleke kwa akina Rostam Aziz? MIS USE OF PUBLIC FUNDS

  kabisa ndugu mungu akutie nguvu .ila tuombe mungu aonekane kwa hili
   
Loading...