Mchungaji adai Kupanga uzazi ni kumkosea Mungu..................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Nimeiona hii kwenye gazeti la Tanzania Daima nikaona niwamwagie kwenye jamvi tuijadili .....hivi imekaaje vile.......................







Mchungaji: Kupanga uzazi ni kumkosea Mungu


na Danson Kaijage, Dodoma


amka2.gif
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelistic Asembless of God (EAGT) James Ibrahimu maarufu kwa jina la Majembe Makali amewataka Watanzania kuacha dhana potofu ya uzazi wa mpango inayohamasishwa na taasisi mbalimbali na serikali.
Akiwahubiria waumini wa kanisa hilo wakati wa ibada iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Siloam Ipagala, Dodoma mjini, alidai kitendo cha uzazi wa mpango ni kufuru mbele za Mungu.
Mchungaji Majembe Makali alisema pamoja na taasisi mbalimbali na serikali kuhamasisha aina hiyo ya uzazi ni tendo la aibu ndani ya nchi na jambo linaweza kusababisha laana kwa taifa.
Akihubiri kanisani hapo alisema inasikitisha kuona watu wanajiita walokole nao wanaingia katika mkumbo huo aliouita wa kishetani wa kutumia vidonge vya majira huku akifafanua kwamba uzazi wa mpango unatakiwa kufuatwa na wasiomwamini Mungu kwa maelezo kuwa ni mpango kutoka kuzimu.
Mchungaji huyo alikwenda mbali zaidi akidai kuwa mpango huo ni dalili za mtu kushindwa maisha kwa visingizio mbalimbali na kubainisha kuwa wote wanaofunga kizazi wanamkosea Mungu na kwa mtaji huo wanatakiwa kutubu kwa kumwekea Mungu mipaka ya uumbaji wake.
Kanisa la EAGT linapinga uzazi wa mpango na hata Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dk. Moses Kulola huwahimiza washirika wake kuacha matumizi ya vidonge vya majira na njia zote za uzazi wa mpango.
 
Huyu mchungaji nimwonavyo mimi anatunga Biblia yake mwenyewe...........ni vyema angelinukuu ni vifungu vipi ndani ya maandiko matakatifu vinapinga uzazi wa mpango kulingana uwezo wa kumudu gharama za kuihudumia familia....................

Mwenyezi Mungu aliposema nendeni mkaijaze dunia hakumaanisha tufanye hivyo bila kutafakari juu ya uwezo wa kuituna familia zetu..................

Labda ndiyo maana huyu mchungaji wanamwita ni majembe makali........................
 
yeye mwenyewe ana watoto wangapi? labda tuanzie hapo. siyo swala la kukataza wenzie wakati yeye anatumia
 
Mkuu mimi nadhani mtu unatakiwa kufikilia kabla hujawaleta watoto duniani mambo yafuatayo:
Msosi bora (sio ilimradi washibe)
Elimu bora (sio kusoma na kuandika tu)
Maradhi bora (sio bora usingizi)
Mtaji wakutosha (sio kuhangaika na ajira za kibongo)
 
Mkuu mimi nadhani mtu unatakiwa kufikilia kabla hujawaleta watoto duniani mambo yafuatayo:
Msosi bora (sio ilimradi washibe)
Elimu bora (sio kusoma na kuandika tu)
Maradhi bora (sio bora usingizi)
Mtaji wakutosha (sio kuhangaika na ajira za kibongo)

Ahsante ELIA ila hapo kwenye nyekundu una maana MALAZI BORA?
 
Back
Top Bottom