Mchumi ashauri fedha zilizoibwa BoT zirejeshwe na riba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchumi ashauri fedha zilizoibwa BoT zirejeshwe na riba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 1, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 59,059
  Likes Received: 32,471
  Trophy Points: 280
  Kuna haja ya kumuuliza JK, huu utamaduni wa mafisadi waliokupua mabilioni ya mapesa ya walipa kodi na hatimaye kuzirudisha pesa hizo huku wakiendelea kuwa huru umetoka wapi!? Kwa nini wasirudishe mapesa hayo huku wakiwa lupango wakisubiri kufikishwa mahakamani?

  Posted Date::3/1/2008
  Mchumi ashauri fedha zilizoibwa BoT zirejeshwe na riba
  Na Ally Sonda,Moshi
  Mwananchi

  WAKATI watuhumiwa wa ufisadi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakidaiwa kurejesha serikalini zaidi ya Sh50 bilioni za EPA, mfanyabishara maarufu wa mjini Moshi, Patrick Boisafi amesema lazima fedha hizo zinazorejeshwa zilipiwe riba.

  Boisafi ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro,amesema pamoja na kwamba serikali haijasema wazi kuwa mafisadi hao walizichukuaje fedha hizo kutoka BoT na hivyo kuamua kuzirejesha baada ya mchezo mchafu kubainika ni lazima watozwe riba ili thamani ya fedha iliyochotwa isipotee

  Mwenyekiti huyo ambaye kitaaluma ni mchumi amesema thamani ya fedha inabadilika kila dakika na kwamba watuhumiwa walichukua fedha hizo muda mrefu uliopita wakiwa wanazitumia kwenye biashara zao na hivyo kuzalisha faidi kubwa.

  "Nimesikia waliochota mabilioni BoT wameanza kurejesha fedha hizo, mimi sipingi huo urejeshaji, bali ninachotaka kieleweke ni kwamba fedha hizo wamekuwa nazo kwa muda mrefu,wamezalisha hivyo ni lazima wawekewe riba walipe," alisema Boisafi.

  Vilevile, Boisafi amemwomba,Waziri wa Fedha na Mipango, Mustafa Mkulo, kuwataja hadharani mafisadi waliorejesha fedha hizo ili waeleweke kwa jamii ambayo alidai inaweza kufichua mali zilizofichwa na mafisadi hao.

  "Sioni mantiki yoyote ya kuficha majina ya hao watuhumiwa, namwomba Waziri wa Fedha na Mipango, awataje hadharani wahusika, inawezekana ni watu tunawafahamu pamoja na mali anazomiki tukiwajua tutasaidia uchunguzi zaidi," alisema.

  Alisema fedha za EPA ambazo ni zaidi ya Sh133m bilioni ni nyingi sana na hivyo si vema zikarejeshwa bila kuongezewa riba na wahusika.
   
 2. S

  Semanao JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 208
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  That is very true hata mtu ambaye si mchumi anaweza kukwambia hii kitu. Kikawaida ukipewa pesa na benki lazima urudishe na RIBA. Na kwa hawa wezi sio riba tu bali wafike kwa pilato, hii itakuwa fundisho kwa watu wengine wanaopnda maisha mazuri na ya kulingishia wengine kwa kutumia pesa za wizi na ulaghai.
   
 3. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hao walioiba hayo mapesa ni wateule, na ikiwa mteule huwezi kuwa treated kama wanavyokuwa treated wezi wengine. Wateule hapa bongo wanaundiwa TUME na kama wewe sio basi wanaku-MAHALU au wanaku-KIULA.
   
Loading...