mchumba

Fmewa

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
292
81
wadau, najitokeza katika hili jukwaa kuomba ushauri.
Nina miaka 27 na kuna binti ambae nimetokea kumpenda na nimeamua kumuoa awe mke wangu. kwa vile nimekuwa sina mazoea nae ya karibu sana nilimuuliza mtu ambae anamfahamu na wako karibu nikitaka kujua kama yule binti yuko tayari kuolewa kwani bado ana 18years, alipoulizwa yule binti alisema kuwa yupo tayari ila alitaka kunifaham kwani alikuwa hanifahamu vizuri. Tulipokutana na kuongea yule binti alisema kuwa hayupo tayari kwa sasa kwani wazazi wake wana mpango wa kumpeleka chuoni mwakani september ila akasisitiza kuwa umri wake bado ni mdogo sana na hafikirii kuolewa kwa sasa kwa umri wake. Nilipoendelea kuongea nae aliendelea kusisitiza kuwa yeye umri wake bado ni mdogo na anadai kuwa alikuwa hajafikiria kuolewa kwa sasa eti kwa ajili ya umri.
Kufuatia majibu hayo nashindwa kujua kua labda anajaribu ili ajue msimamo wangu kama niko serious au ndo mambo ya kina dada yaani niko njia panda ila kwa kweli nampenda na ninamaanisha kumwoa. naombeni ushauri ndugu zangu
 
Mwache ale maisha kwanza uking'ang'aniza atakuja kukusumbua badae.na ni hivyo tena anaenda chuo utakua unalia kila cku .......ila na ww mkuu mbona hivyo ht hamjafahamiana ushatangaza ndoa!!!
 
Wewe siye chaguo lake hivyo mission fail, jipange pengine maana mapenzi yakulazimishana na yale yakuondo mkosi wa ndoa siku hizi hakuna kabisa.
 
Mbona nyie wote umri wenu bado mdogo hauendan na presha mliyonayo ya ndoa?niisliongelee sn kwan hayo ni maamuzi ya mtu binafsi!Inawezekana kbs hayuko tayari kuolewa km alivyokueleza malengo yake ni kuendelea na masomo,pia km mwanzon alimkubalia huyo uliyemtuma kuwa yuko tayari kuolewa lkn mlipoonana akageza kibao inawezekana hakukupenda baada ya kukuona na kuongea na ww,au pia labda anakupima msimamo wako pia,nakushauri usiwe na haraka peaneni muda wa kufahamia vizuri kwan kwa mujibu wa story yako hakuna anayemjua mwenzie vizuri,fahamianeni na km kila mmoja akiridhika na mwenzie ndio mfikie kuongelea ndoa,ndoa si mchezo waulize waliooa watakupa habari yake,acha kukurupuka!
 
at 27 ni sawa kabisa kuoa,ili kuingilia programme ya mwenzio ya masomo sio sawa.Mwonyeshe upendo,jaribu kuwa karibu naye,take your time atakuzoea na pole pole atakupenda.Ukiwa mvumilivu unaweza umpate na may be in 3 years time mnaweza oana .best wishes.
 
atakusumbua huyo age difference kubwa sana, mara nyiingi huwa wanashauri age difference isizidi 5 yrs. huyo atakusumbua akishaanza kujua maand ya mapenzi ingawa siku hizi wanaanza mapema sana kuanzia 15yrs. good luck
 
Wewe si unampenda? Kama unampenda kuwa na subira basi! Huyo bado anataka kukufahamu vizuri kama kweli uko siriaz na unachokisema! Wewe cha msingi ni kuacha kumkumbushakumbusha habari za ndoa kila mara na utaona matokeo yake, hiyo thread aliyokuwa hataki hata kuisikia ataianzisha mwenyewe! Fuata ushauri wangu kaka!
 
Hakuna cha kukujaribu hapo msikilize anachokuambia! 18???? Au unataka, msomeshe kwanza. Halafu usituambie 'eti anasema hajanifahamu vizuri', wewe sema ukweli mmefahamiana lini isijekuwa we ndo umemfahamu muda mrefu tofauti na yeye basi unaforce naye akufahamu! Embu tupe ufafanuzi!
 
Mhhhh!! she is too young kuolewa..............kama kweli umempenda, mwache asome shule kwanza, na kama anakupenda na wewe then akifikisha kama 23 hivi ndo muoane. Usisahau kumshirikisha Mungu katika utafutaji wako. All the best.

Stay blessed.
 
Atakusumbua sana baadae, muache kwanza asome na akili yake ikue.....
 
nawasukuruni nyote kwa ushauri wenu mzuri mmenifungua ufahamu kuelewa yale a,bayo nilikuwa siyaelewi. ila kwa habari ya kusoma mie sijakataa ila napata wasiwasi kwani ilikuwa kwamba aende kusoma mwaka huu lakini tatizo ni fedha ila hiyo mwakani kuna rafiki wa baba yake amabe anasema kama hali itakuwa mjema anaweza kumpeleka chuoni kusoma.
Nashukuru kwa msaada wenu wa mawazo
 
mi napita tu kuna FATAKI namtafuta.. aliyemuona aniambie kaelekea upande gani?
 
Usimlazimishe kufuata matakwa yako, mpe muda na uhuru ili aamue mwenyewe
 
Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii? we kaka vipi mbona huyo bado mdogo

muache aende shule atimize ndoto zake kama unampenda msubiri

sasa we lazimisha kumuoa halafu uje tena hapa jamvini mke wangu ananisumbua

anapenda starehe alei mtoto vizuri,umri baba haurusu.
 
ata mimi niliambiwaga hivohivo kwamba bado mdogo eti nisubiri labda baada ya miaka 3,nilipokuja kurudi kijijini nikakuta ameolewa..bahati nzuri ni kwamba nilikua na wachumba wengine watatu so nikachukulia poa..nakushauri uwekeze sehemu zaidi ya moja..ni hayo tu.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom