Mchumba wangu kanisaliti!! Niko kwenye maumivu makali naombeni ushauri

Wakubwa zangu shikamooni, vijana wenzangu habari vipi?
Ndugu zangu, nipo serious sanaa katika ombi langu, nakuomba unipe muda wa kunisikiliza kidogo na unishauri kama inafaa.

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 29, ni mwajiliwa serikalini idara ya Afya. Kuna binti nilianza nae uchumba 2017 mwanzoni yeye akiwa chuo flan cha afya, Mimi ni Mgogo yeye ni Mbulu ana miaka 24 sasa.

Tulianza mapenzi akiwa ameonesha msimamo wa kutoshiriki tendo lolote na mimi mpaka mwaka mmoja ulipopita ndo tukaanza kukutana kimwili. Ni binti ambae niliona huyu anafaa kuwa mke wangu kabisaa maana alikua ana msimamo sanaa hata kwa watu wengi waliokua wakimtongoza maana alikua ananionesha sms na calls zao, bas nikawa namshauri wajibu wewe ni mke wa mtu na unahitaji heshima, kiukweli nilijipa moyo hapa nimepata mke kweli kweli.

Basi akamaliza chuo 2017 mwishoni nikamtaftia ajira ya kujishikiza mahali flani mkoa wa Mwanza. Sasa nikawa nimeongea na mtu mmoja awe anafatilia nyendo zake wakati mimi nipo mbali.

Alipotimiza miezi miwili kazini nikapata taarifa kuna kabwana mdogo ka umri wa miaka 22 - 24 kanatembea nae hapo hapo alipopanga chumba, sikutaka kuamini, ikanibidi siku moja nifanye kusadiri kwenda kumtembelea kimya kimya bila taarifa, nikafika akanipokea vizuri. Ilipofika usiku nikamwambia sasa mpenzi unaweza kunihakikishia huku huna mchezo wowote mchafu wa kimahusiano? Akanijibu hapana kabisa mpenzi wangu naomba uniamini.

Nikamuuliza, Je, unaweza kunipa simu yako nikague chochote? Akapata kigugumizi sanaaaaa, nikamuuliza Unanipenda na unajiamini? Akajibu ndio, nikamwambia bas naomba simu yako, akapata kigugumizi kizito sanaaa.

Basi ikanibidi nichukue simu yake nipitie sms na whatsap, aseee niliyoyakuta ni mazito mnooooooo wallahi Nimepata simanzi kubwa sanaaa, ikanibidi niondoke usiku huo huo kwenda kutafta Lodge nikalala na kesho nikaondoka kurudi kazini.

Mchumba wangu huyu nilikua nimeshafahamiana na ndugu zake baadhi na mama yake mzazi alikua ananijua kwa picha tu na alikua tayari karidhia niwewe mkwe wake kabla hata sijaenda kujitambulisha maana matendo niliyomfanyia mwane ni mwanaume mwenye malengo mazuri wazi wazi. Kinachoniuma zaidi ni kwamba nimetumia muda mwingi sanaaa kumjenga kiimani, kumjenga juu ya tabia za wanaume wenye tamaa, kiukweli niliamini huyu mwanamke sasa hakuna atakae weza kumshawishi maana hata mimi binafsi nilikua nimebadilika sanaaa kitabia sikuwa nnahamu na michepuko tena niliona sasa huu ni muda wa kutulia na mwanamke mmoja sina haja ya kutanga tanga na dunia ya leo.

Ndugu zangu niko serious sanaaa, naombeni ushauri cha kufanya, mwanamke huyu alikua anatembea na kijana wa mwenye nyumba tena kwa kulala nae chumbani kwake karibu kila wiki.

Mwanamke alionesha sanaaa kunipenda tulikua tunawasiliana kila siku zaidi ya mara 5 kila siku ya Mungu. Leo naona dunia imenigeuka, nina maumivu makali sanaaaa, niliplan nije kumtambulisha kwetu mwaka huu December, na kwao ningeenda kujitambulisha November ili mwakani Mungu akijaalia tufunge Ndoa. Wakuu, niko gizani, nina msongo wa mawazo, mimi ni jasiri sanaaa lakini nakuomba wewe ndugu yangu ushauri wako katika hili, nakuomba usinitukane wala kunikejeli maana utaniongezea majonzi makubwa.

Naamini thread yangu hii itawafunza na wengine watakao kumbwa na mkasa kama wangu.
ASANTE kwa Muda wako

Sent using Jamii Forums mobile app
KAMA WEWE NI MWANAUME WA DODOMA NAKUOMBA USIENDE KULIALIA NA KUGALAGALA KAMA WENGINE WANAPOVISHANA PETE ZA UCHUMBA!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukuran boss Sent using Jamii Forums mobile app
Rudi tu Dodoma ukabidhiwe kit kikali cha kigogo
ndugu yangu Wambulu huwawezi HUWAWEZI hawawezekani hapo tu umesoma sms na missed calls
je ungebana nje ya dirisha la chumba chake si ungezimia mtoto wa mwenye nyumba anavyotwanga?
Pole sana najua mtarudiana na wal usimkorofishe wewe akileta kula tembelea mama yake na nduguze lakini USIMUOE MBULU
 
Maumivu mengine ni yakujitakia. Kwann upekue simu yake? Kwani ulisikia yeye hana mihemko? Kwann ukae nae mbali kwa muda mrefu? Kwann wewe huna mahusiano nje yake? Kwani bikra ulimtoa wewe? Acha ulimbukeni
 
Wahenga walisema Fimbo ya mbali haiuwi nyoka, yaliwakuta.. Fanya maamuz mapema either ni kumkanya aache tabia hiyo km unahisi atakuelewa au kusonga mbele uepuke kupoteza muda.!!

Mm namshauri huyu mtoa mada amuoe huyo mdada, maana karibia kila mwanamke ana-cheat au ana mapungufu mengine..sasa ataacha wangapi? As long as huyo mdada ana tabia na personality nzuri mengine yanavumilika as long as huyo mdada asimletee magonjwa au kumdharau huyo mkaka Mis powers
 
Mpende mama yako au mlezi wako tu inatosha,

Mim huwa nashangaa sana mtu kuumia kisa mapenzi au maumivu yake.

Nikwambie kitu ukikiendekeza bhasi ushatawaliwa.

Endlea kutawaliwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama umegundua ni kuwa ulipoanza kumfuatilia ndio ukaanza kupata tabu.

Ungemwacha tu usimfatilie saizi ungekuwa na raha na maisha yanaenda
 
Ninatabia hiyo pia nahisi ni nature yangu, nilidhani nakosea.
Hahah unamkazia mpaka mwenyewe anatia akili. Kuna kamoja nakapeleka mchaka mchaka mpaka sio vizuri. Kila kitu napinga tu kama chalii ya BAVICHA. Namaindisha vitu vidogo yani inshort staki anizoee kabisa. Heshim ibaki pale pale tu.

Sahivi sidekezi manzi kabisa. Ati "mbona unani treat harshly sana mpenzi" kimoyomoyo najisemea hamnaga shukurani mbwa nyieee!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ogopa sana mwanamke anayekwambia anakupenda,waliambiwa watutii tu hayo mengine ni uhuni.

Na usisahau kuwa wanawake ndio binadamu pekee waliokutana na shetani na kupanga njama za kumlaghai Adamu.
.
.
Hawaaminiki,hawaridhiki na hawala utu wala fadhira.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka ha
Wakubwa zangu shikamooni, vijana wenzangu habari vipi?
Ndugu zangu, nipo serious sanaa katika ombi langu, nakuomba unipe muda wa kunisikiliza kidogo na unishauri kama inafaa.

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 29, ni mwajiliwa serikalini idara ya Afya. Kuna binti nilianza nae uchumba 2017 mwanzoni yeye akiwa chuo flan cha afya, Mimi ni Mgogo yeye ni Mbulu ana miaka 24 sasa.

Tulianza mapenzi akiwa ameonesha msimamo wa kutoshiriki tendo lolote na mimi mpaka mwaka mmoja ulipopita ndo tukaanza kukutana kimwili. Ni binti ambae niliona huyu anafaa kuwa mke wangu kabisaa maana alikua ana msimamo sanaa hata kwa watu wengi waliokua wakimtongoza maana alikua ananionesha sms na calls zao, bas nikawa namshauri wajibu wewe ni mke wa mtu na unahitaji heshima, kiukweli nilijipa moyo hapa nimepata mke kweli kweli.

Basi akamaliza chuo 2017 mwishoni nikamtaftia ajira ya kujishikiza mahali flani mkoa wa Mwanza. Sasa nikawa nimeongea na mtu mmoja awe anafatilia nyendo zake wakati mimi nipo mbali.

Alipotimiza miezi miwili kazini nikapata taarifa kuna kabwana mdogo ka umri wa miaka 22 - 24 kanatembea nae hapo hapo alipopanga chumba, sikutaka kuamini, ikanibidi siku moja nifanye kusadiri kwenda kumtembelea kimya kimya bila taarifa, nikafika akanipokea vizuri. Ilipofika usiku nikamwambia sasa mpenzi unaweza kunihakikishia huku huna mchezo wowote mchafu wa kimahusiano? Akanijibu hapana kabisa mpenzi wangu naomba uniamini.

Nikamuuliza, Je, unaweza kunipa simu yako nikague chochote? Akapata kigugumizi sanaaaaa, nikamuuliza Unanipenda na unajiamini? Akajibu ndio, nikamwambia bas naomba simu yako, akapata kigugumizi kizito sanaaa.

Basi ikanibidi nichukue simu yake nipitie sms na whatsap, aseee niliyoyakuta ni mazito mnooooooo wallahi Nimepata simanzi kubwa sanaaa, ikanibidi niondoke usiku huo huo kwenda kutafta Lodge nikalala na kesho nikaondoka kurudi kazini.

Mchumba wangu huyu nilikua nimeshafahamiana na ndugu zake baadhi na mama yake mzazi alikua ananijua kwa picha tu na alikua tayari karidhia niwewe mkwe wake kabla hata sijaenda kujitambulisha maana matendo niliyomfanyia mwane ni mwanaume mwenye malengo mazuri wazi wazi. Kinachoniuma zaidi ni kwamba nimetumia muda mwingi sanaaa kumjenga kiimani, kumjenga juu ya tabia za wanaume wenye tamaa, kiukweli niliamini huyu mwanamke sasa hakuna atakae weza kumshawishi maana hata mimi binafsi nilikua nimebadilika sanaaa kitabia sikuwa nnahamu na michepuko tena niliona sasa huu ni muda wa kutulia na mwanamke mmoja sina haja ya kutanga tanga na dunia ya leo.

Ndugu zangu niko serious sanaaa, naombeni ushauri cha kufanya, mwanamke huyu alikua anatembea na kijana wa mwenye nyumba tena kwa kulala nae chumbani kwake karibu kila wiki.

Mwanamke alionesha sanaaa kunipenda tulikua tunawasiliana kila siku zaidi ya mara 5 kila siku ya Mungu. Leo naona dunia imenigeuka, nina maumivu makali sanaaaa, niliplan nije kumtambulisha kwetu mwaka huu December, na kwao ningeenda kujitambulisha November ili mwakani Mungu akijaalia tufunge Ndoa. Wakuu, niko gizani, nina msongo wa mawazo, mimi ni jasiri sanaaa lakini nakuomba wewe ndugu yangu ushauri wako katika hili, nakuomba usinitukane wala kunikejeli maana utaniongezea majonzi makubwa.

Naamini thread yangu hii itawafunza na wengine watakao kumbwa na mkasa kama wangu.
ASANTE kwa Muda wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpaka hapo sijaona uthibitisho wa usaliti, hujashuhudia tendo lolote ovu LA huyo Dada, umekuta tu SMS kwenye simu. Hizo unazifuta na unasonga mbele. Si kila SMS kwenye simu inathibitisha matendo, zingine ni story tu. Heri huyo Dada ulomfunza tabia kuliko kuzoa mwingine aliyefunzwa na wenzio. Huyo wako no rahisi kumrekebisha. Mke ni wako ukiwa Naye, mtaftie kujishkiza hapo ulipo. Timiza mchakayo wa ndoa mapema, tangia 2017 yipo tu anakusubiri we we, kakuvumilia sana huyo, msamehe na umtunuku tuzo
 
Nashukuru kwa ushauri Boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom