Mchumba wangu kanisaliti!! Niko kwenye maumivu makali naombeni ushauri

Wakubwa zangu shikamooni, vijana wenzangu habari vipi?
Ndugu zangu, nipo serious sanaa katika ombi langu, nakuomba unipe muda wa kunisikiliza kidogo na unishauri kama inafaa.

Mimi ni kijana nina umri wa miaka 29, ni mwajiliwa serikalini idara ya Afya. Kuna binti nilianza nae uchumba 2017 mwanzoni yeye akiwa chuo flan cha afya, Mimi ni Mgogo yeye ni Mbulu ana miaka 24 sasa.

Tulianza mapenzi akiwa ameonesha msimamo wa kutoshiriki tendo lolote na mimi mpaka mwaka mmoja ulipopita ndo tukaanza kukutana kimwili. Ni binti ambae niliona huyu anafaa kuwa mke wangu kabisaa maana alikua ana msimamo sanaa hata kwa watu wengi waliokua wakimtongoza maana alikua ananionesha sms na calls zao, bas nikawa namshauri wajibu wewe ni mke wa mtu na unahitaji heshima, kiukweli nilijipa moyo hapa nimepata mke kweli kweli.

Basi akamaliza chuo 2017 mwishoni nikamtaftia ajira ya kujishikiza mahali flani mkoa wa Mwanza. Sasa nikawa nimeongea na mtu mmoja awe anafatilia nyendo zake wakati mimi nipo mbali.

Alipotimiza miezi miwili kazini nikapata taarifa kuna kabwana mdogo ka umri wa miaka 22 - 24 kanatembea nae hapo hapo alipopanga chumba, sikutaka kuamini, ikanibidi siku moja nifanye kusadiri kwenda kumtembelea kimya kimya bila taarifa, nikafika akanipokea vizuri. Ilipofika usiku nikamwambia sasa mpenzi unaweza kunihakikishia huku huna mchezo wowote mchafu wa kimahusiano? Akanijibu hapana kabisa mpenzi wangu naomba uniamini.

Nikamuuliza, Je, unaweza kunipa simu yako nikague chochote? Akapata kigugumizi sanaaaaa, nikamuuliza Unanipenda na unajiamini? Akajibu ndio, nikamwambia bas naomba simu yako, akapata kigugumizi kizito sanaaa.

Basi ikanibidi nichukue simu yake nipitie sms na whatsap, aseee niliyoyakuta ni mazito mnooooooo wallahi Nimepata simanzi kubwa sanaaa, ikanibidi niondoke usiku huo huo kwenda kutafta Lodge nikalala na kesho nikaondoka kurudi kazini.

Mchumba wangu huyu nilikua nimeshafahamiana na ndugu zake baadhi na mama yake mzazi alikua ananijua kwa picha tu na alikua tayari karidhia niwewe mkwe wake kabla hata sijaenda kujitambulisha maana matendo niliyomfanyia mwane ni mwanaume mwenye malengo mazuri wazi wazi. Kinachoniuma zaidi ni kwamba nimetumia muda mwingi sanaaa kumjenga kiimani, kumjenga juu ya tabia za wanaume wenye tamaa, kiukweli niliamini huyu mwanamke sasa hakuna atakae weza kumshawishi maana hata mimi binafsi nilikua nimebadilika sanaaa kitabia sikuwa nnahamu na michepuko tena niliona sasa huu ni muda wa kutulia na mwanamke mmoja sina haja ya kutanga tanga na dunia ya leo.

Ndugu zangu niko serious sanaaa, naombeni ushauri cha kufanya, mwanamke huyu alikua anatembea na kijana wa mwenye nyumba tena kwa kulala nae chumbani kwake karibu kila wiki.

Mwanamke alionesha sanaaa kunipenda tulikua tunawasiliana kila siku zaidi ya mara 5 kila siku ya Mungu. Leo naona dunia imenigeuka, nina maumivu makali sanaaaa, niliplan nije kumtambulisha kwetu mwaka huu December, na kwao ningeenda kujitambulisha November ili mwakani Mungu akijaalia tufunge Ndoa. Wakuu, niko gizani, nina msongo wa mawazo, mimi ni jasiri sanaaa lakini nakuomba wewe ndugu yangu ushauri wako katika hili, nakuomba usinitukane wala kunikejeli maana utaniongezea majonzi makubwa.

Naamini thread yangu hii itawafunza na wengine watakao kumbwa na mkasa kama wangu.
ASANTE kwa Muda wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeye ni binadam kwanini ulimwamini hivyo na kwanini ulimtafutia kaxi mbali na wewe huku ukijua pua kule anakoenda kuna vijana rijali. Je uliitoa bikra yake. Sasa nakushauri ukipata mwanamke usikae nae mbali itakula kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani mahusiano ni kurekebishana tabia na kuvumiliana lakini sio kila kosa uhukumu, Bila hivyo wazazi wetu wasingetuleta Duniani. Chakufanya kaka mkanye kwa Mara ya kwanza na umshauri atakuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ushauri ni kwamba tafuta mchumba mwingine. ukirudiana naye utakuwa udhaifu mkubwa sana, na atazidi kukuumiza coz atajua ulishawahi kumfumania na ukaendelea naye. hiyo tabia kwake haitakoma. wanawake wako wengi duniani huyo Mungu amekuonyesha sio chaguo lako
 
Endeleeni kutulelea sie twala kitonga tu na kuhongwa juu. Unampa pesa zako ananipa mimi
 
Pole sana ila kuna kosa moja kubwa sana ulifanya... Kosa la kupekua simu yake bila ridhaa yake kwa asilimia mia moja.... Ni vema usitafute matatizo bali yaache matatizo yaje yenyewe.... Hakuwa na jinsi ya kukukatalia na hakupenda ugomvi.. Huyo kwangu bado ni mwanamke bora
Kosa la pili ulilofanya ni kuondoka bila kumpa nafasi ya kujieleza.... Haya mambo yapo, hasa mnapokuwa mbali mbali... Kuna ngono na kuna mapenzi... Si kila tunaolala nao tuna mapenzi nao, sometimes ni situation tu.....
Huwezi kujua alikuwa anapitia maisha gani, furaha zake, huzuni zake changamoto zake, upweke, stress nk...
You still have the chance to make it again... We are all not perfect, sisi si wakamilifu, tuna mapungufu ya kila aina... Amekosea sawa lakini kumuacha kuna maumivu mengi kuliko ku reconsile....
Kakosea hii ni mara ya kwanza you still have chances... Mrudie kwa upendo mlitengeneze hili anaweza kuja kuwa mwanamke bora kama ulivyokwisha kusema mwenyewe... Mpe nafasi ya kujutia alivyofanya lakini bila manyanayaso, bila kebehi bila matusi.... Safari ya mapenzi, mahusiano mpaka ndoa huwa ni ndefu na changamoto ni nyingi... Ichukulie hii kama changamoto, ameteleza hajaanguka, mshike mkono msonge mbele
Una shock ya kile ulichokiona... It happens! Chukua muda kutafakari jinsi ulivyowekeza kwake... Tukio hili lisizime ndoto yenu kubwa... Ndoa ni zaidi ya ngono
Usijiumize usijitese! Kama yuko tayari kujutia na kutengeneza... Fanyeni hivyo sasa... Utaokoa maumivu mengi


Jr
Mkuu uzalendo huo unao wewe peke yako kwenye watu million 20.
 
Ila story yako haijakamilika. Mwanamke baada ya hayo kutokea amefanya nini? Kakiri kosa,kajaribu kukutafuta kwa simu au sms ili muyajenge?
 
Hahah unamkazia mpaka mwenyewe anatia akili. Kuna kamoja nakapeleka mchaka mchaka mpaka sio vizuri. Kila kitu napinga tu kama chalii ya BAVICHA. Namaindisha vitu vidogo yani inshort staki anizoee kabisa. Heshim ibaki pale pale tu.

Sahivi sidekezi manzi kabisa. Ati "mbona unani treat harshly sana mpenzi" kimoyomoyo najisemea hamnaga shukurani mbwa nyieee!!!
haha hiyo ndo dawa yao mkuu amna namna
 
BASI MSAMEHE KWA MARA YA KWANZA
mana Nina imani nawe ushakosea wengi na ulihitaji msamaha wao

Mimi ni mmoja wa wanaume ambao nahukumu Sana wanawake wa aina hiyo ila kwa hali Kama ulivyoielezea MSAMEHE KWA MOYO WOTE, Kwa ajili ya utu, kwa ajili yako na kwa ajili yangu japo hunijui

Huyo mwanamke bado anakupenda sana na ndo maana anajuta to the maximum
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokukuta,kwanza mshukuru Mungu hili limetokea kwenye uchumba,ingekua mbaya zaidi kama lingekupata wakati mmefunga ndoa,kifupi huyo binti sio mwaminifu hata mngeoana bado angechepuka tu...nikutoe hofu wanawake waaminifu bado wapo tena wengi tu,tulia jipe muda na mwombe Mungu atakupa mke mzuri mwaminifu...niliwahi kua na mchumba 4yrs,nilimpenda sana,tukiwa 3months before marriage dada akagoma wakati maandalizi yamefanyika,nilipomuhoji akasema anahitaji ajipange na afanye kazi kwanza miez 6 ndio afikilie kuoana...nikakaa chini kutafakari nikiwa na maumivu pia nikifikiri wazazi,ndugu na jamii wamejiandaa kwa harusi aibu kubwa....nilipiga moyo konde moyoni nikasema huyu hanifai....baada ya miez michache nikasikia ana mchumba na kampeleka kwao kumtambulisha....kufupisha stori lile jaribu nililivuka salama kabisa,nilikaa miaka 4 nikaoa mke mzuri ambaye nafurahia maisha...na yule dada mpk kesho hajaolewa na amebaki na majuto makuu...tulia wanawake waaminifu wapo wengi sana,utapata.
 
POLE, KWANZA ULIKUWA NA NIA NJEMA LKN HUKUPATA CHAGUO AMBALO NI LAKWAKO, KIKUBWA KAMA UKO VZUR KIIMAN, MUULIZE MUNGU JUU YA HILO, THEN MWAMBIE MUNGU NIPE MKE MWEMA, MUNGU HAJAWAH KUSHINDWA, INAWEZA IKAWA MUNGU KAKUEPUSHA NA MTU AMBAYE SIO WAKWAKO, HUYO YAWEZA KUWA ANA MWENZAKE MBELEN.......WACHA KUTESEKA ...MUNGU YUPO KWA AJILI YAKO....THEN KINGINE.....A GAL IS STILL TOO YOUNG KAKA MBONA HVO? 29 YA KWAKO....GAL ANA 24 NDO TU KATOKA KWENY ADOLECENSE STAGE......CHAGUA LADY ATKEAST AMBAYE ANA 25 AU 25+ HAO WATOTO WAACHE KWANZA BHANA...BADO TAMAA ZINAWAANDAMA......M NIMEOA NINA MIAKA 32 MKE WANGU ANA MIAKA 28 UNAONA HAPO.....HAKUNA UJINGA NDANI TUNAISHI MAISHA MAZUR LKN KIKUBWA PIA SISI KABLA YA KUOANA TULIAMUA KWENDA KUTUBU KWANZA NDO MAISHA YAANZE.....SISI MAISHA YETU MUNGU MBELE ...WENGINE BADAE SANA....INATUSAIDIA SANA....NDOA INA MIAKA MINNE....SIJUI KITU KUKOSA AAMANI NDANI YA NDOA....MUNGU NI MWEMA.....LA MWSHO......NILIWAH KUAMBIWA NA MAMA YANGU OA KABILA LOLOTE TANZANIA LKN USIOE KABILA LETU WENYEWE......YAAN NISIOE KABILA LANGU...MM SIJUI NI KABILA GANI....ANGALIA JINA LANGU......SO UCHAGUZ KUOA WAPI NAAKO KUNAMATTER NAJUA BINTI WA KIMBULU NI WAREMBO HATAR...LKN HUOI UREMBO...UNAOA MKE AMBAYE UTAKAA NAYE SIKU NYINGI KULIKO MTU MWINGINE APA DUNIAN...BARIKIWA...ACHA NAA FUTA MACHOZI RUDI KWA MUNGU...USILALAMIKE ...MUNGU NDO JIBU LAKO...AMINA
 
KINGINE NILISAHAU.....USIPENDE KUMKAGUA MWANAMKE SIMU.....MFUNDISHE NA KUMPA MAARIFA YA KUAMINIANA....HUJAMUOA BADO PLS....UKIMUOA AMINIANENI WENYEWE LKN
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom