Mchumba wangu anahitaji tuzae mtoto wakati mie mwenyewe kimaisha bado sijasimama

Ngoja nikwambie kitu ndugu yangu.... Mtoto ni Baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Usiogope kisa huna mishe za kueleweka, God's good.

You never know, kupata kwako mtoto ndio mambo yako kuwa sawa, na Mungu analeta maajabu yake kwa mtu yoyote
Usipate mtoto ukitegemea hii doctrine ikubebe utapotea.
 
Nina mchumba wangu huyo amekuwa akinishawishi tuzae mtoto upande wangu kiukweli kimaisha bado sijasimama hapa nilipo ninawaza hiyo mimba nitaileaje mtoto nitamleaje wakati kipato changu chenyewe hakieleweki lakini pia kwao sijulikani na yeye kwetu hatambuliki

Lakini binti amekomaa tuzae mtoto ananiambia tusichelewe Sana sababu ya umri wetu umeenda haya mambo mengine yatajiseti mbele kwa mbele mpka sasa sijachukua maamuzi yeyote yale ila tuu naombeni ushauli mzuri wa busara
Kutoka kwenu makonki wa JF

Uamuzi upi sahihi wa kuchukua tuzae tuu au tuendele kusubili wakati sahihi japo mwenzangu ana kiu ya kupata mtoto
Hutafuti mtoto kwa sababu ya umri, Mpaka uwe umejianda kiuchumi kumlea huyo Mtoto, Na wewe una malengo gani kwenye maisha? umefikia wapi kwenye hayo malengo? Maswali ni mengi kabla ya kuamua
 
Hahaha hamna bana nataka niitwe baba aiseee
Sasa we mpaka 36 mambo hayajakaa sawa unatarajia yatakaa sawa lini ili uwe baba? Hii akili imetuchelewesha sana yani, Africa mtoto ni baraka we zaa tu atakuwa tu kwa neema za mungu mzee! Hamuwezi shindwa kumlisha na ndio wanakuwaga chachu ya ku hustle hard!

Ukute huyo binti umeanza kumshikilia miaka karibia 6 nyuma mpo kwenye mahusiano bubu! Zaa nae tu sasa ndio mke wako huyo maana clock yake ishaanza ku tick tock utashangaa umeachwa ghafla uje kufungua nyuzi za vilio humu!
 
Yatakaa sawa akiwa na 50+...lol
 
MKUUUU MKUU. Nimekuita kwa herufi kubwa ili unielewe vizuri yani Kama huna direction ya Maisha ebu achana na huyo MWANAMKE kama anakonmalia suala la kupata mimba yani kulea mtoto sio jambo rahisi hasa kama hukujipanga ni bora itokee bahati mbaya ila sio kupanga kupata mtoto na hujajipanga kimaisha utamtesa mtoto na wew utateseka sana ni bora ufikiri juu ya wewe utakula nini kuliko leo kuambiwa mtoto anaumwa inahitajika LAKI 2 au mama maziwa hayatoki kanunue maziwa ya kopo kaka acha tu nimepita huko ninachokwambia nakijjua vizuri.
Kingine huyo mwanamke anataka umuoe ila anashindwa namna ya kukushawishi lakini ngoja ajifungue huyo mtoto aisee kelele za LINI UNAENDA KUTOA MAHARI..LINI UTANIVISHA PETE YA UCHUMBA SIJUI KWAO WANASEMA LINI UTAENDA KUJITAMBULISHA.. WALAHI UTAJUTA. MWANAMKE AFATE MSIMAMO WAKO KUWA HUTAKI MTOTO KWA SASA. ikimchekea sasa nakwambia utakuja kujuta baadae.
 
Nina mchumba wangu huyo amekuwa akinishawishi tuzae mtoto upande wangu kiukweli kimaisha bado sijasimama hapa nilipo ninawaza hiyo mimba nitaileaje mtoto nitamleaje wakati kipato changu chenyewe hakieleweki lakini pia kwao sijulikani na yeye kwetu hatambuliki

Lakini binti amekomaa tuzae mtoto ananiambia tusichelewe Sana sababu ya umri wetu umeenda haya mambo mengine yatajiseti mbele kwa mbele mpka sasa sijachukua maamuzi yeyote yale ila tuu naombeni ushauli mzuri wa busara
Kutoka kwenu makonki wa JF

Uamuzi upi sahihi wa kuchukua tuzae tuu au tuendele kusubili wakati sahihi japo mwenzangu ana kiu ya kupata mtoto
Nipe mimi uyo mchumba wako,halafu wewe utafute mwingine
 
Kwa umri huo , curve imeshafika kwenye kilele sasa imeanza kushuka kwa wote wawili kwa hiyo nyie zaeni tu, mtoto mmoja hatowaendesha sana.
 
MKUUUU MKUU. Nimekuita kwa herufi kubwa ili unielewe vizuri yani Kama huna direction ya Maisha ebu achana na huyo MWANAMKE kama anakonmalia suala la kupata mimba yani kulea mtoto sio jambo rahisi hasa kama hukujipanga ni bora itokee bahati mbaya ila sio kupanga kupata mtoto na hujajipanga kimaisha utamtesa mtoto na wew utateseka sana ni bora ufikiri juu ya wewe utakula nini kuliko leo kuambiwa mtoto anaumwa inahitajika LAKI 2 au mama maziwa hayatoki kanunue maziwa ya kopo kaka acha tu nimepita huko ninachokwambia nakijjua vizuri.
Kingine huyo mwanamke anataka umuoe ila anashindwa namna ya kukushawishi lakini ngoja ajifungue huyo mtoto aisee kelele za LINI UNAENDA KUTOA MAHARI..LINI UTANIVISHA PETE YA UCHUMBA SIJUI KWAO WANASEMA LINI UTAENDA KUJITAMBULISHA.. WALAHI UTAJUTA. MWANAMKE AFATE MSIMAMO WAKO KUWA HUTAKI MTOTO KWA SASA. ikimchekea sasa nakwambia utakuja kujuta baadae.

Mkuuu wagalatia wanauliza, je akiitapa mimba kimasihara itakuwaje hapoo??
 
Back
Top Bottom