Mlundilwa Jr
JF-Expert Member
- Dec 11, 2019
- 2,889
- 4,294
Habari wana jf
Kadri siku zinavyoenda nimekua naiangalia hii tamthilia anayoicheza mdogoangu hapa Duniani bado inaniweka njia panda
Iko hivi, mdogoangu alianzisha mahusiano na mwanaume ambaye kiukweli hakumjua vizuri na niseme tuu hata yule Boy hakumjua vizuri dogo kutokana na muonekano wake
Kiukweli dogo ni mweupe sana na Mungu kamjalia nywele za singasinga
Hali iliyopelekea jamaa amuhisi ni Mpemba au Mwarabu, basi bwana mahusiano yao yalikua ya siri sana hatimae wakapeana Mimba hapo ndipo harakati za kutaka kuchukuana ili wakaishi mume na mke zikaanza kwani jamaa alianza kuwashirikisha ndugu zake
Basi alipoenda kumtambulisha kwao familia ya jamaa ikamhoji mbona kama Mwarabu jamaa naye kwakutaka sifa akasema ndiyo
Basi naye mwenzangu na mie akaja na jamaa nyumbani ili kumtambulisha na mm binafsi sikujua kama dogo kapewa Mimba
Hatimaye siku ya kuja kumposa dogo tulishangaa jamaa na ndugu zake wanakuja na ostazi tena wakiwa wameambatana na watu wanaotokea huko Zanzibar wakiamini mwenzangu na mimi moja kwa moja ni muislam kitendo kilichofanya nihamaki na kujiuliza huyu dogo tayari kabadili Dini kumbe hapana bali wao walijua dogo ni muislamu
Ikabidi tuanze sisi akina kaka kujitambulisha ndipo wao wenyewe wakahamaki kumbe mkiristo? Basi ingawa hawakuonyesha dalili za moja kwa moja kushituka ikabidi waghairi kile walichojia na kusema basi mtaandika gharama za posa theni mtuletee
Basi walivyoenda kwao huko wakamshauri jamaa nenda kawaambie hadi Azae ndiyo tutatoa hiyo posa, basi bana siku zikaenda miezi ikasonga, hatimae dogo akajifungua
Wakamtuma tena jamaa nenda kawaambie kwanza mimi sina kazi pia Baba yangu alikufa ila ukweli nikwamba familia ilishamshauri usioe mwanamke Dini tofauti na wewe
Na ukiangalia mtu mwenyewe anatokea familia Duni
Sasa narudi kwa mwenzangu na mie ambaye ni mdogoangu yaani pamoja na danadana zote hizo bado yupo gizani akiamini ipo siku watamtolea posa. Ilihali familia ya jamaa ilishamuwekea x kutokana na Dini yake na anayejua hii siri ktk familia yetu ni mimi tuu
Na chaajabu anaenda kwa mwanaume kulala na kurejea hasubuhi nyumbani kwa Maza
Sasa wakuu najiuliza hivi hii character aliyopewa dogo itaisha vipi ktk hii tamthilia ya uhalisia
Nihayo wakuu yanayoendea huku Duniani.