Mchumba wa kike kuvuta sigara mbele za wakwe!!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,462
154,325
Jamani,
Bro katoka Uingereza na mchumba wake, wote ni Watanzania na wameenda ughaibuni mwaka 2010 wakiwa ma boyfriend na nyumbani wakiwa hawamjui huyo binti.
Juzi usiku wameingia Tz kwa ajili ya kutambulisha uchumba wao na mapumziko ya Xmas.
Leo usiku kulikuwa na sherehe ndogo ya utambulisho, baada ya utambulisho binti akaliwasha li Malboro lake.
Moshi nyumba nzima, kwa aibu mama akamuambia tunaomba ukavutie nje, sisi huku Tanzania hatujazoea kuvutia sigara ndani.
 
Duhhh huyo kaka yako awe makini na kumchunga huyo bibie Bujibuji tunavyokujua kwa kupenda wadada,kaka yako akizubaa kidogo tu anakatwa kidizaini!

Mwanangu akija kutambulisha mchumba wake na huyo mchumba awe wa kiume au wa kike akalipuliza mbele yetu,nitawafukuza kwa kweli
 
Last edited by a moderator:

Kimoyomoyo nikasema hivi huyu binti kukaa nje tumiaka tuchache tu kisha sahau mila zetu, je akikaa miaka 10, si atasahau hadi wakweze?
 
bro wko ajiandae sana kwenye ndoa...anunue tray za kutosha...
cigarettes1.jpg
 
mh..wakwe wa siku hizi ni hatal.usikute hata huko alikotoka alikuwa havuti basi tu ushololo.....na kutaka kujionyesha kwamba ameathirika na tamaduni za watu..aende akavute mbele ya wazaz wake..
 
Mchumba amefanya jambo jema na ni jasiri. mchumba anatekeleza sera ya UWAZI na UKWELI.
Hataki matatizo baada ya commitment.
 
Mchumba amefanya jambo jema na ni jasiri. mchumba anatekeleza sera ya UWAZI na UKWELI.
Hataki matatizo baada ya commitment.

kila jambo na wakati wake.
Kuvuta sigara sebuleni sidhani kama ni ujasiri....
Hata ofisini huwezi kuvutia misigara yako, utaenda kuvutia nje.
 
Huu mti vp?? Anatumia?? Manaake wadada wengi wakibongo tena wanaotoka nje ndio wanaojifanya kupinda
 
Attachments

  • marijuana_061313_mt_tif_.jpg
    marijuana_061313_mt_tif_.jpg
    62.2 KB · Views: 136
Issue ni moja, kuvuta sigar hadharani ni kosa la jinai na sio ustaarabu. Ningekuwa wifi yako hizo chafya 30 zingezofuata angeona aibu mwenyewe.
 
Issue ni moja, kuvuta sigar hadharani ni kosa la jinai na sio ustaarabu. Ningekuwa wifi yako hizo chafya 30 zingezofuata angeona aibu mwenyewe.

King'asti huyu binti hana adabu hata chembe, kwa mimambo yake haya ya madharau nyumbani kwetu sidhani kama kuna mtu ataweza kumtembelea nyumbani kwake.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom