MCHUMBA Vs H.I.V

kizabala

New Member
Sep 15, 2011
2
0
Nataraji kufunga ndoa katikati ya mwaka ujao mjini Dodoma na mchumba wangu tuliyedumu naye kwenye urafiki kwa muda wa miaka 4 sasa, tatizo limekuja baada ya kwenda kupima na mwenzangu amekutwa tayari ni muaathirika wa virusi, nampenda binti huyu na natamani kuishi naye kwa mapenzi ya dhati.
Naombeni ushauri kama naweza kumuoa nami nikawa salama kipindi chote cha uhai wetu.
 
mmmmh inahitaji moyo..muoe then mkapate ushauri jinsi ya kuishi pamoja....na kutumia kinga sasa kwenye kupata mtoto sijui inakuaje.
 
Huo mtihani sio mchezo ila unaweza kuishi nae na ukabaki salama nenda ukapate ushauri jinsi ya kuishi mnaweza kuishi na kupata watoto
 
hongera kwa kupenda kiasi hicho,
Kapate ushauri wa wataalamu na mtaweza tu kuishi salama
 
pole sana kaka mimi namwonaga nandipa wa isidingo ana relationship na wanaonyesha wanatumia institutions zenye kutoa directions za kitaalam. Inaonyesha kuna organizations ambazo zinatoa ushauri jaribu kuingia kwenye website yao unaweza ukakuta address za wataalam. Otherwise, jaribu kutembelea vitengo vinavyoshughulikia waathirika kama pale Muhimbili unaweza ukapata ushauri zaidi.
Ila sikujua mpaka enzi hizi kuna mapenzi ya dhati kama yako. Je, katika miaka yote 4 hamkuwahi kukutana kimwili?tujuze
 
mhh mtihani uoooooooooooooooo....si sjui kwa kweli ngoja wenye akil waje waseme..
<br />
<br />
kwa hyo ww huna akili? Ukijidharau na watu watakudharau,MKUU KAKABALA,LENGO LA KUPIMA KWENU LILIKUWA NI NINI? UKIJIBU HILI SWAL NDIO NTAWEZA KUKUPA USHAURI MANA NITAJUA LENGO LENGU LA KUPIMA LILIKUWA NI NINI
 
pole na hongera ...
  1. je kabala ya kupima ulijamiiana nae???
  2. nini hasa kilipelekea mkapime??? maamuzi yenu au mlilazimishwa???
  3. je nani ajuaye kilichopo????
 
pole sana ndugu yetu.ni mitihani ya maisha.ila kama walivyosema hapo juu ni vyema tungepata information zaidi.kama ifuatavyo:

1.Je kwa kipindi chote icho mliwahi kushiriki tendo?

2.Nini hasa kimewasukuma kwenda kupima....hapa ndio pakuanzia
3.Je umemuuliza kama yupo tayari kuishi na ww kwa hali iyo?...asiwe anajifeel guilty...

4.Inawezekana kuishi nae na kupata watoto.inahitaji ushauri wa karibu sana toka kwa wataalam.
5.Kipindi gani kimepita tangu mmepima?
 
sijaelewa hiyo miaka mi4 mlikua mnaangaliana tu au???na lengo la kupima si ili ka wote mpo salam ndo watu wale kitu cha pilau,au lengo la kupima ni kuongeza idadi ya wapimaji kwenye takwimu ya wizara???
 
Mapenzi ya kweli haya, ila nenda kwa washauri kwanza, na waambie wazazi wako uone watakushauri nini, kapata wpi na ulikuwa nae miaka minne, usijekuwa unachukua mzigo mzito kumbe mwenyewe mwanamke wala sio mwaminifu
 
Back
Top Bottom