Mchumba hajawahi kuulizia chochote kuhusu wazazi wangu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,554
44,725
Just imagine una mwanamke mchumba wako mna mahusiano karibia Mwezi wa Tano mnaishi mikoa tofauti ila ni mikoa jirani, mimi nimewahi kumuuliza historia yake na hata picha za wazazi wake nilimuomba akanitumia ila yeye binti hawajui wazazi wangu na hajawahi hata siku moja kuulizia tu.

Kama wazazi wangu wapo hai kama ni wazima wanaendeleaje yaani in short hata kinafki tu aulizie walipo hakuna sasa najiuliza kweli anafaa kuwa mke kwa Hali hio.

Ina maana ana uwezo mdogo wa kiutambuzi au tatizo hapo ni nini na kila siku mnachat mnaongea sana ila hakuulizi chochote kuhusu familia yako hata kukuuliza tu Kama una wadogo zako hakuna Sasa na mi nikasema labda kajisahau tu nikae kimya nimpe muda nimpime.

Maana siwez me kuanzisha maada kuhusu ndugu zangu wakati ni wajibu wake awaulizie, naona miezi inakatika tu halafu eti ndo mwanamke anatarajia tutaoana na ni mtu kasoma mpaka ngazi ya cheti.

Swali langu ni je, hii ni hali ya kawaida kweli mbona kama nahisi atakuwa na roho mbaya?.
 
Mkuu tuliosomea saikolojia hapo inaonesha binti huyo anaona ww sio hazi yake ,kuna rank anayohitaji pole sana na achana nae
Tumwambie tu ukweli ni hajamvutia
yupo nae 7bu anamtumia viela ela vya matumizi so anazugazuga muda kukupotezea muda wewe

Mwanamke mwenye nia ya kuingia NDOANI kitu cha kwanza ukiacha swali unafanya kazi gani basi
basi swali litakalofuata ni kuhusu umepanga au unaishi kwa wazazi
ukijibu nimepanga litafatia wazazi wako wapi na mmezaliwa wa wangapi na wewe wangapi kuzaliwa

sasa mkuu km hamna hayo maswari basu hapo hakuna mchumba ni mdangaji anakulia ela zako tu
 
huyo hafai, wanawake tunapenda kujua taarifa za ndugu wa karibu wa mtu tumpendae na mara nyingi tunatania tuongee na mama mkwe😂😂😂
Mimi nilivyo na kiherehere napendaga vibaya mmo naweza mpa zawadi mama wa mpenzi wangu wakati hata mpenzi wangu sijampa chochote. Kila saa ntataka kujua habari zake nitataka kujua anapenda kula nini.

Itoshe kusema penye miti hakuna wajenzi.

Huyo dada hafai.

"Sisi yanga tuna watu" team kubwa africa mashariki na kati😂😂
 
Endelea kumshawishi zaidi ili akuelewe hapo huyo binti Hana malengo na wewe anakuchezea tu na kukupotezea mdaa anyways mpe mdaa zaidi maana hawa viumbe ni shida
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom