Mchumba atemwa baada ya kutoomba hela ya matumizi kwa miezi 2

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,679
Mwanaume alisikika akilalama "haiwezekani akae kimya kwa miezi 2, anatumia nn? Au kuna mtu mwingine ana mhudumia? Siku za nyuma ilikuwa haiishi wiki".

Haya yameibuka huku kwetu uswazi. Jamani uswahilini kuna vituko.
 
Mbona yule amegoma kuchukua mshahara tangu 2013 lakini amevumiliwa
 
Hahahahaa...ila huyo jamaa ana point pengine huyo dada hana kazi na jamaa ndo anamhifadhi,kwakweli lazima ashangae kwanini haombwi hela..
 
Hata km ni mimi ningemwacha, haiwezekani mpiga mizinga akaacha kunipiga mizinga gafla hivo, nimekosea nini? Ningemhisi ana mtu sio bure
 
labda shem ameweka akiba ya zile alizomwomba hata wik haijapita ila msela anahis kuna ufekfek.
 
Mkiombwa hela mnalalamika tunawachuna sana tujiongeze
Tusipoomba tunaambiwa tunachepuka kuna mtu anahudumia
Viumbe hamna jema nyieeee,nimewatua
 
Mi mwenyewe ninge mtumbua

Ukiona mtu hachukui mshahara jua ana jilipa posho kubwa zaid ya mshahara

Julieth kairuk wa mapenzi uyo
 
Nahisi mwanaume asipoombwa hela hajiskii vizuri japo sina uhakika, hata kama hategemewi atatafuta vijisababu tu vya kumuacha mdada.
 
wale wazee wa kulia lia oohh sijui wanawake mizinga, kuchunwa waje waone responsible man kuna wanaume hata kama anajua una kipato lazima anataka na yeye ahudumie...yan na ole wako ukatae anaweza hata kukuacha...lakini kuna vivulana humu kutwa vinalia wanawake wanapiga mizinga mara wanachunwa
 
Back
Top Bottom