akajasembamba
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 1,177
- 1,790
Ushauri waungwana nina mchumba ambaye nina mpango wa kumuoa, ushauri niliopewa niangalie familia na ukoo wao kwa ujumla, nilichokiona nimeambiwa hafai kuolewa kwa kuwa atakuwa amerithi laana za kifamilia/kiukoo.
Yaani baba yake na mama yake hawakufunga ndoa na mama yake amezaa na wanaume WATATU tofauti pia hali hiyo ni kwa mama zake wakubwa na wadogo( maternal aunties) WOTE WATANO hakuna hata mmoja ambaye amewahi kuolewa kila mtoto na baba yake.
Hali kadhalika kwa ndugu zake yaani watoto wa mama zake wakubwa n wadogo(maternal cousins) nao pia hakuna aliyeolewa wote wamezaa bila ndoa na wanaumetofauti.
Kingine nilichokiona katika familia ya mzaZi wake yaani wajomba zake n mama zake hakuna hata mmoja aliyejenga nyumba wote wameishi mpaka wanafariki katika Nyumba za urithi walizoachiwa na babu yao na wamekaa humo vizazi hadi vinne wakigawana vyumba na wakigombea kodi za wapangaji hakuna anayejishughulisha kufanya kazi zaidi ya kutegemea kodi za wapangaji.
Upande wa baba yake hali kadhalika hakuna hata Shangazi yake mmoja aliyeolewa wote wamezaa tu. Naambiwa wakristo wanaamini kuna laana za kurithi na dalili moja wapo ni ukoo kuwa na asilimia kubwa ya kutoolewa ndoa kuvunjika.
Je waungwana mchumba anayetoka familia ya aina hii anafaa kuolewa hatarithi mikosi Hiyo?