Mchukia Fisadi kafiwa

Status
Not open for further replies.
Pole sana MF. Naelewa uchungu wa kufiwa na baba. Mwanzo ni ngumu kukubali. Kubali tuu maana ni kazi ya Mungu na atakutia nguvu na yote yatapita na yatakwisha.
RIP Baba wa MF.
 
Wakuu wote nashukuru sana kwa faraja yenu niliyoipata kutoka kwa kila mtu hapa JF. Wengi wameniletea messages kwa njia mbali mbali na nasikia kufarijika pamoja na tatizo la kuondokewa na baba yangu kwa ghafla.
Baba hakuwa ana tatizo lolote kiafya kwa siku hiyo ya msiba wake. Hata chakula cha usiku alikula vizuri yeye na mama yangu wakiwa katika afya njema na tabasamu kubwa bila kujua nini kingempata baadaye. Walikuwa wanaishi wawili tu maana watoto wao wote saba na wajukuu 19 kila mtu yuko kivyake humu duniani. Kumbuka kuna kumuacha baba na mama na kuambatana na mwenzi wako.
Lakini muda mfupi baada ya kwenda kulala alisikia kama kifua kikimbana na baada ya dakika kama 30 alikuwa ameshapoteza fahamu na hatimaye maisha.
Namshukuru kila mmoja na asanteni wana jf kwa faraja yenu. Nimerudi tena na tunaendeleza mapambano.
Nitamkumbuka baba yangu kama mwana TANU/CCM na kiongozi kwa miaka 30 katika chama hiki. Lakini nakumbuka kwamba katika miaka hii ya mwisho wa uhai wake alikuwa amekwisha kukata tamaa kabisa na jinsi mambo yanavyokwenda katika chama hiki. Nilikuwa nikiiona huzuni yake kila aliposimulia jinsi anavyoona mambo yanakwenda ovyo katika chama alichokipenda na kukithamini. Sidhani angetoa tena kura yake kwa chama hiki katika uchaguzi wowote kwa miaka ya karibuni. Nina imani na ninachokisema maana nilisikia kauli zake siku za mwisho wa uhai wake.
MF
 
Tunashukuru sana kwa taarifa hii.Mungu ampe nguvu za kustahimili majonzi ya kufiwa na baba yake.Tunamuombea safari njema.

Mwenzetu "Mchukia Fisadi" amefiwa na baba yake mzazi usiku wa kuamkia leo na yuko safarini kuelekea Bukoba kwenye mazishi.

Kanifahamisha nami nikaona ni vyema kuwafahamisha. Wale wenye namba yake ya simu mnaweza kuwasiliana naye kwa maelezo zaidi.

RIP mzazi wa mwenzetu.
 
Pole sana MF na familia yote kwa ujumla. Mwenyezi Mungu akupeni nguvu ya kustahimili majonzi katika kipindi hiki kigumu. Tunakutakieni faraja, amani na imani.
R.I.P. Baba.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom