Mchuano ubunge Arusha ni Kim, Munisi na Lema, Monaban hana nafasi

mmmmmmh haya mwaka huu mengi yatasemwa kuhusiana na jimbo la Arusha mjini lakin binafsi naamini jimbo litarudi mwaka huu japo tutumia nguvu nyingi sana.
 
Arusha mjini hakuna wakumtoa Lema jimboni. Labda Mungu mwenyewe tu. Hao magamba wanajidanganya tu lakini arusha mjini kirusi CCM alishatokemezwa tokea 2010. Mwaka huu makamanda wameweka nguvu zaidi katika udiwani ili kuhakikisha Meya anatoka chadema bila ya mizengwe.
 
Kuna taarifa na mpango wa chini chini unaofanywa na makada wa ccm kumwomba mfanyabiashara kijana wa madini Thomas Munis kugombea Ubunge ,baada ya kuonekana kada Philemon Molle aliyejitokeza ni mzee na hawezi kumwangusha Lema.
 
Wakuu ni hivi Arusha mjini CCM ipo hoi bin taabani hawana uwezo wa kumwondoa Lema kwasababu zifuatazo.

1. CCM Arusha mjini hawana masikilizano kabisa kila mmoja ni mjuaji hakuna organization kama zamani,Katibu mkuu yupo kivyake,mwenyekiti yupo kivyake,watendaji katika nafasi mbali mbali wapo kivyao.

2. CCM ngazi ya wilaya enzi za marehemu Mzee Kileo ilikuwa inajua mbinu za ushindi hata kama ni kwa kununua ushindi kama walivyofanya mara mbili kwa Godbless Lema.

3. CCM ilijimaliza yenyewe wakati wa uchaguzi wake wa ndani.Mheshimiwa Lowassa mwamba wa kanda ya kaskazini alishindwa kuidhibiti Arusha mjini kwa kipindi kirefu akaja na mkakati wa kuibadili CCM Arusha mjini kuwa ya yenye sura ya kikabila (waarusha na maasai) zaidi ili kufaidi utii anaoupata kupitia mlango wa malaigwanani.Lowassa anajua ukitaka kuwatawala wamaasai hakikisha malaigwanani wapo upande wako.CCM Arusha Mjini ikajigeuzwa ya kikabila zaidi kuanzia Mwenyekiti wa wilaya,Mweka hazina........Matokeo yake wanaCCM hasa waswahili wa mjini wakakosa jukwaaa wakatimkia CUF ambayo haina nguvu Arusha.Kundi hili siku zote lipo CCM wakati wa shida na raha.Kibaya zaidi CUF ipo UKAWA hii ni karata muhimu sana ambayo hata Chifu wa Kizanaki juzi aliwaambia CCM wasiidharau UKAWA.

4. CCM ilijivisha koti la ukabila haina uwezo wa kushinda Arusha mjini kwa karata ya ukabila na ikashinda.ndio maana sasa wanaanza kutapatapa baada ya kugundua wakimleta Mollel watajimaliza mapema kabla ya kipenga hakijapulizwa.Uongozi wa wilaya hauna uwezo wa kufanya kampeni kwakuwa tayari sifa zilizowaingiza katika uongozi zimewakimbiza makada wengi wa CCM Mjini.

5. Mkakati wa ukabila ulikuwa ukiratibiwa na Ole Medeye katika kikao cha Arusha Technical College.Video zipo na baada ya kikao hicho ndio ukaanza mkakati wa kuondoa viongozi wote wasiokuwa waarusha au wamaasai.


Kuna taarifa na mpango wa chini chini unaofanywa na makada wa ccm kumwomba mfanyabiashara kijana wa madini Thomas Munis kugombea Ubunge ,baada ya kuonekana kada Philemon Molle aliyejitokeza ni mzee na hawezi kumwangusha Lema.

litakua jambo jema tuondoe janga la jiji letu

kwa Arusha hakuna wa kumuangusha Lema, Lema kwa Arusha ni sawa na Messi kwa Bacelona
 
Back
Top Bottom