Mchuano mkali wagombea Uenyekiti CHADEMA Kanda: Kamati Kuu yaweka uteuzi hadharani

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Kamati Kuu ya CHADEMA imetoa rasmi orodha ya wagombea wa nafasi mbalimbali katika kanda zake zote 10 baada ya mchujo mkali.

Kati ya Orodha hiyo mvuto mkubwa ni nafasi ya Uenyekiti kanda ya Kaskazini ambako kuna mtifuano mkubwa kati ya wabunge wake wawili machachari Godbless Lema na Joseph Selasini.

Kanda nyingine yenye mvutano mkubwa ni kanda ya Serengeti ambako mafahali wawili wabunge John Suguta Heche na Esther Matiko wanawania nafasi ya Uenyekiti.

Kanda nyingine inayotizamwa na mashabiki wa siasa nchini ni Kanda ya Kati ambapo Alhonce Mbassa na Lazaro Nyalandu wanachuana kugombea Uenyekiti

Kanda ya Kusini nako si haba kwani wababe wawili wa siasa za kusini Suleiman Mathew na Cecil Mwambe wanachuana kugombea uenyekiti.

Hata hivyo Kanda ya Pwani inayotizamwa kama Kanda Kiongozi Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Tluway Sumaye amepita bila kupingwa kugombea Uenyekiti hiyo ikionekana kama heshima kubwa kwake.

Ikumbukwe kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA washindi wote wa nafasi ya Uenyekiti wa Kanda moja kwa moja watahesabika kama wajumbe wa Kamati Kuu.

1574671460767.png
 

Attachments

  • 2220826_UTEUZI_WAGOMBEA_KANDA-1.pdf
    588.3 KB · Views: 2
Uchaguzi wa uwongo watu wa makao makuu wanachagua na kupitisha hata walioshindwa kwa kigezo cha maagizo kutoka kwa mbowe na ukabila juu pale morogoro lijualikali alishinda mkampa Devotha minja kisa ni mchaga

State agent
 
Hao ndio walioteuliwa na Kamati Kuu kugombea Katika uchaguzi wa Kanda mbalimbali za Chama nchini.

Nafasi hizo za walioteuliwa ni Mwenyekiti wa kanda, Makamu mwenyekiti na muweka hazina.

Fungua kiambatanisho hapa chini kusoma.
Screenshot_20191124-195537~2.png
 

Attachments

  • UTEUZI WAGOMBEA KANDA-1.pdf
    588.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom