Mchovu Yosefu Sinde Warioba ana ajenda gani na vijana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchovu Yosefu Sinde Warioba ana ajenda gani na vijana?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 14, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Nimepitia mara wa kadhaa kuanzia jana yatokanayo na hoja za Waziri Mkuu Mstaafu Yosefu Sinde Warioba kwenye TBC1 jana akiwamwagia dongo vijana kuwa waache kulalamika juu ya uongozi uliopo...................hoja zake ambazo zilinifanya nianze kujiuliza ya kuwa hivi Sinde akiwa na miaka 35 Nyerere alipomteua kuwa Mwanasheria Mkuu hivi kigezo hakikuwa ni nepotism kweli maana sioni kama ni mtu mwenye busara hata chembe................................

  hoja ya Sinde ni kuwa Nyerere alipokuwa Waziri mkuu wa kwanza akiwa na miaka 39 alikuwa kijana...........aliyemrithi pia Kawawa alikuwa ni kijana.................................na wengi wa mawaziri Wakuu ukiwaondoa Msuya na Malecela walikuwa vijana..........................kwa hiyo huo ndiyo ushahidi wake wa ya kuwa vijana wamekuwa wakiongoza nchi hii na kizazi hiki cha vijana kiache malalamiko...........


  Hoja hizi zinanikumbusha profesa mmoja mwalimu wangu aliwahi kusema ukiacha wafanye maamuzi kwa niaba yako watakula pia kwa niaba yako..........

  Kule ufaransa akina Boukassa na Leopald Senghor waliteuliwa kuwa wabunge kwenye Bunge la ufaransa.........................Mkoloni huyo alibuni utaratibu huo ili kuhalalisha uporaji wa mali katika makoloni yake......................kwa hoja ya kuwa acheni kulalamika mbona watu wenu kutoka kwenye makoloni tunakula nao meza moja hapa ulaya?.........................mbinu hizohizo hata Mwingereza alizitumia kwa akina banda wa malawi kuwa daktari wa malkia n.k..................

  tatizo la kizazi cha vijana wa leo siyo kukosa uwakilishi ndani ya taswira ya uongozi ila wao wanashirikishwa vipi katika kuzitambua chachu za maendeleo na kuzipangilia chachu tajwa ikiwemo kutekeleza mipango ya maendeleo..................siyo kuwakilishwa katika High Table pekee...................hakutoshi kuwawezesha kuweka ugali na maharagwe kwenye meza ndani ya vibanda vyao vya nyasi...........................
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,796
  Likes Received: 36,817
  Trophy Points: 280
  Hakutoa mfano wa Nape kama kijana??
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Angetoa mfano wa Nape ningevunja TV au Radio yangu muda ule ule....ingekuwa ni dharau kubwa kwa Taifa,vijana na wananchi kwa ujumla....
   
 4. only83

  only83 JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Huyu mzee katushikia bango sana vijana bila kujua sababu,na wala siioni anachoongea....anataka vijana wa CCM na vijana upande wa upinzani tuungane tuwe wamoja bila kusema tuungane kwa namna gani,hoja yake haiweki wazi anakuwa kama anaogopa vile kuweka wazi mawazo yake....
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  la ajabu hakumwongelea labda aliona nape ni bomu na anadhalilisha vijana kwa kutokuwa na maandalizi ya kutosha.....
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,796
  Likes Received: 36,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu juzi nimesikia Hotuba flani ya Nyerere anasema nanukuu "Upumbavu uko kwa aina mbalimbali kama ambavyo kuna mtu mrefu na mwingine mfupi"
  Kwa maana hii ya Nyerere naamini kiupumbavu Sinde ni mrefu kuliko Hashimu Zabiti.
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mkuu hiyo nami nilisikia na nilicheka sana lol!! Kweli Babu yetu wa Taifa na wengine baba wa taifa kwao aliona mbali sana.....
   
 8. K

  Kamura JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  huyu babu ni mchovu sana sioni jingine.............................angelikuwa ana busara angeliendelea kula sembe yake ya bwerere ambayo nayo ni mfano wa kiubaguzi.......................inakuwaje viongozi wa ngazi za juu kitaifa wawe na pensheni yenye rutuba na wengineo wasiwe nayo..........
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  wewe wala hujanielewa........................vuijana hawataki spoon-feeding bali wanataka kushirikishwa katika kupanga na kusimamia maendeleo yao............hawataki wawekezaji kutoka nje na wao wawe wapagasi wao..........
   
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Wakati wa uhuru wasomi wachache waliokuepo waliingizwa serikalini kuchukua nafasi za wakoloni waliokua wanaondoka. Nikiangalia hoja ya Warioba kuhusu vijana wa sasa,ningekua mtangazaji ningemwuliza yeye na wazee wenzake wamefanya nini kuwezesha vijana kuchukua madaraka? Wamesaidiaje kukuza na kurutubisha demokrasia ya vyama vingi?
   
 12. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana Ruta kwa kulileta hili suala la huyu mzee! Binafsi nmekuwa natafakari kauli zake toka jana, na pia hapa saiv namsoma kwenye Raia Mwema.. . Kwa umri wake na pia kama sehemu ya mjenzi wa mfumo wa nchi yetu, nmesononeshwa sana na mtazamo wa mzee.
  Haikumpasa ye kuishi kutusema tu sie vijana, anatakiwa kwenda mbali zaidi na kutuonyesha ni namna gani mfumo (ambao yeye alikuwa sehemu wa kuujenga) unatakiwa kufanyiwa mapitio ili vijana wawe na nafasi ipi katika kujenga taifa lao kama wao enzi hzo walivyopata kujenga taifa lile la ndoto ya BABA! Mtu makini yeyote anatakiwa kuelewa kuwa vijana leo hii ni waathirika wa mfumo katika taifa lao, tumemomonyolewa ujasiri katika kupambana na mustakabali, tumeaminishwa katika siasa za kichovu na zisizo za kujitegemea. Mfumo umeharibu Elimu (kama chemchem ya nguvu za fikra), hivi mzee Sinde hayajui yote haya? Sawa anayajua, na anasema tusilalamike tupambane.... Ni kweli tunapambana ndio maana tunajenga hoja ni namna gani tupewe nafasi ya kuweka sawa ili uharibifu ambao sisi tumefanyiwa na mfumo walioujenga wao usiende kwa wanetu! Anachokisema Mzee Sinde ni sawa na kutarajia Nzi aliye kwenye chupa iliyofunikwa na mwenyewe, atoke bila kupiga kelele wala kujipiga kwenye kuta.... Eti anampigia kelele?! Huu ni uenda wazimu wa kizee!
  Namna anavyoongea mzee Sinde, ni wazi kuwa anamengi sana kusema na anayajua ila kwa sababu za usalama wake anaamua kukimbilia kundi letu kwa kujua hamna kitu vijana tutafanya... Pia yeye amepoteza hadhi ya ushujaa aliyowahi kuwa nao, kwa vijana kusambaratika mbele ya macho yake huku na yeye akilalamika kuwa vijana wanamkumbusha majukumu yake!
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Anazungumzia vijana wa magamba.
   
 14. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 868
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 80
  Ni vyema Mzee warioba akajua hali ilivyo ndani ya nchi yetu..!utaongeleaje umoja wa vijana wakati vyombo vya dola vinafanya kazi ya kuiba na kujenga ufa..? kidini, kiumri nk
  Lakin pia umoja wa vijana hauwezi kuwepo hadi wezi hawa ccm waondolewe kwanza!
   
Loading...