Mchoro wa wizi wa mafuta Bandarini uliowapa sifa Gazeti la Jamhuri. Wengine waige...

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
image.jpg

Kwa wale wasiouona mchoro ambao ulimfanya Rais Magufuli atoe sifa kwa gazeti la Jamhuri hii ni fursa pekee. Hili ni funzo kwa magazeti mengine yanayojifanya yanaandika habari za uchunguzi kumbe yamejaa udaku. Mwanahalisi na Marehemu MAWIO yanahusika hapa
 
Wakiandika Magu arudishe nyumba za serikali utasikia gazeti linaandika mambo ya uchochezi.

Ni nini Tanzania hii kisichojulikana na hapa ina maana magu amekubali gazeti Fulani ndiyo liwe linampa taarifa, mawio au mwanahalisi hapana kwa sababu linawafuatilia wao.

Mwambie Magu ajianze yeye mwenyewe kwa kurudisha nyumba za serikali kisha ajipime kama anafaa kuendelea kutumbua majipu au hafai
 
Badala uwaulize uhuru na mzalendo unauliza mwanahalisi, kweli nyani haoni.. mwanahalisi ameandika mengi sana kwa kujua ni hatari kwa uhai wa utawala wenu mkaja na gia za kuyafungia hovyo magazeti, haya yangeandikwa awamu ya 4 ungesikia ni uchochezi na lingefungwa mara moja, wakati linaandika uozo wa maliasili mlikuwa mnasema gazeti la kufungia vitumbua, leo magufuli kalisifia nanyi vijana #46 mnalisifia, kweli kujitia upofu ni janga.
 
Badala uwaulize uhuru na mzalendo unauliza mwanahalisi, kweli nyani haoni.. mwanahalisi ameandika mengi sana kwa kujua ni hatari kwa uhai wa utawala wenu mkaja na gia za kuyafungia hovyo magazeti, haya yangeandikwa awamu ya 4 ungesikia ni uchochezi na lingefungwa mara moja, tunaj
Uhuru na Mzalendo hawajinasibu wanaandika habari za kiuchunguzi. Hao Mwanahalisi ndo wanajinasibu hivyo
 
Lizaboni mbona huko nyuma hukuwa hivyo? Kwani magazeti yote lazima yaandike jambo moja tuu?
Mbona Uhuru ambalo liko karibu zaidi na system hulisenei?
Nimelitaja Mwanahalisi kwa sababu specifically linajifanya linaandika habari za kiuchunguzi. Ni wakati sasa wabadili mtazamo wao. Badala ya kusema wanaandika habari za kiuchunguzi, waseme wanaandika habari za Udaku. Waungane na Eric Shigongo
 
Ina maana Mwanahalisi hakuna uozo waliowahi kuufichua kwa Maslahi ya Taifa? Wewe kwa kuwa Jamhuri limesifiwa na Magufuli basi ndiyo umechanganyikiwa nalo!? Achana na Mwanahalisi, gazeti la Mfanyakazi enzi hizo liliandika habari za Loliondo na Mwandishi wa Habari hiyo Stan Katabalo akaishia kufa kifo cha ajabu ajabu, lakini serikali tangu ya Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli zimefanya nini kuhusu mbuga hiyo ya Loliondo?

Hata hivyo kazi iliyofanywa na gazeti la Jamhuri ni ya kutukuka!!
 
Nilitegemea wao ndio wangepokea pongezi kutoka kwa rais, na sio wale wenye magazeti ya kufungia maandazi.
Haswaaaaa! Binafsi sijawahi kutoa fedha yangu kununua gazeti la Mwanahalisi wala Marehemu MAWIO.
 
Wakiandika Magu arudishe nyumba za serikali utasikia gazeti linaandika mambo ya uchochezi.

Ni nini Tanzania hii kisichojulikana na hapa ina maana magu amekubali gazeti Fulani ndiyo liwe linampa taarifa, mawio au mwanahalisi hapana kwa sababu linawafuatilia wao.

Mwambie Magu ajianze yeye mwenyewe kwa kurudisha nyumba za serikali kisha ajipime kama anafaa kuendelea kutumbua majipu au hafai
Yaani kwa kazi anayopiga Magufuli, hata kama atachukua lile PPF Tower haina neno. Kaokoa mabilioni mengi sana yaliyokuwa yanapotea kwa njia za kifisadi. Nyumba ni kitu gani!
 
Haswaaaaa! Binafsi sijawahi kutoa fedha yangu kununua gazeti la Mwanahalisi wala Marehemu MAWIO.
Lakini rais anayasoma na alisema "andikeni sie tunasoma magazeti" anayoona yanamfaa anayafanyia kazi ambayo hayamfai ana achana nayo, ndio maana hakukashifu vyombo vya habari wala waandishi wa habari, sijui mkapa anajisikiaje maana alishasema waandishi wa nchi hii ni wa hovyo hovyo.
 
Ila kuna mahala alisema kuwa wapo waandishi wa habari wanaandika as if nchi hii si yao. Kila siku wao ni kuchonganisha na kuandika mabaya tu. hilo aliliweka wazi kabisa. Ndo maana nikatolea mfano wa gazeti la Mwanahalisi na Marehemu MAWIO
 
Badala uwaulize uhuru na mzalendo unauliza mwanahalisi, kweli nyani haoni.. mwanahalisi ameandika mengi sana kwa kujua ni hatari kwa uhai wa utawala wenu mkaja na gia za kuyafungia hovyo magazeti, haya yangeandikwa awamu ya 4 ungesikia ni uchochezi na lingefungwa mara moja, wakati linaandika uozo wa maliasili mlikuwa mnasema gazeti la kufungia vitumbua, leo magufuli kalisifia nanyi vijana #46 malisifia, kweli kujitia upofu ni janga.

Mkuu ndio walivo hao, wana kazi ya kusifia mke wa jirani anapendeza wakati yeye ana mke wake na hamjali!
 
Back
Top Bottom