Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

Hisani "Gari kubwa" hii bendi ilishakufa baada ya waimbaji wake baadhi kuhamia morogoro, baadhi waliobaki Dar wakaamua kuanzisha kundi jipya na jina jipya ikaitwa JAGWA MUSIC.
HISANI au GARI KUBWA wapinzani wao wakubwa walikuwa wanaitwa TOPAZ ambayo nayo pia haikudumu muda mrefu ikavunjika baadhi yao wakaanzisha kundi jipya likiitwa SEVEN SURVIVOR yaani waliosalia na kuanzisha kundi jipya walikuwa ni watu saba chini ya kiongozi wao JUMA MPOGO a.k.a GENERAL LUPOZ.
Kipindi cha ambacho bendi hii ya HISANI na TOPAZ zipo kwenye chati OMARY OMARY alikuwa bado hajaanza kusikika, baadae hizi bendi zilivyokufa na kuzaliwa upya yaani JAGWA na 7 SURVIVOR ndipo OMARI OMARI nae akaja na bendi yake ikiitwa ATOMIC na wimbo wake uliotamba sana ni "said dabani" na baadae "mfungwa hachagui gereza" na nyingine nyingi tu.
Kipindi hicho hata Bongo flavour haijulikani.
 
HABAR.....KUNA MWENYE NAYO MFUNGWA ACHAGUI GEREZA YA ATOMIC BAND OMARY OMARY
Mimi ninayo ila nashindwa kuapload humu, nitumie namba ya WhatsApp nitakutumia. Halafu kuna WhatsApp group la Mchiriku lipo ukitaka utaunganishwa, huko utapata kila unachotaka kuhusu Mchiriku.
 
Tulikua tumekaa, maskani Lebanon ferry,
Tumestarehe Sina lile wala hili,
Kumbe kuna msela mmoja mtaani kafanya zari,
Mara mda mdooogo,
Wakaja Polisiii,
Wakaja na gari laooooo,
Kufika wakatukamataaa,
Mahakamani tukafikaaaaa,
Tukasomewa Shitakaaaaaaa.
 
Tulikua nimekaa, maskani Lebanon ferry,
Tumestarehe Sina lile wala hili,
Kumbe kuna msela mmoja mtaani kafanya zari,
Mara mda mdooogo,
Wakaja Polisiii,
Wakaja na gari laooooo,
Kufika wakatukamataaa,
Mahakamani tukafikaaaaa,
Tukasomewa Shitakaaaaaaa.
bonge la ngoma ilooo ndugu yangu nitumie..............aiseeee
 
Kikundi cha Hisani kilikufa.
Tupo mbioni kukifufua.Hivi punde mtatupata hewani katika management mpya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom