Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

Naomba nikuweke sawa kaka mkubwa. Huyu KICHEKO w E-fm ambae kwa sasa yupo clauds, sio kicheko wa gari kubwa (HISANI). Wakati hisani wanapiga nyimbo zao enzi hizo kicheko huyu wa genge la singeli alikuwa mtoto mdogo sana. Wale hisani walikuwa wanapatikana mwananyamala wakati kicheko na dogo mfaume wote watoto wa temeke. Kicheko kazaliwa mikoroshini temeke. Hakuwahi kuimba mnanda. Hisani walikuwa dizain kama ya watu wazima kipindi hicho sasa angalia Age ya kicheko sasa hv ni viwili tofauti. Wakati jamaa wanatamba hata huyu marehemu omary omary, Allah amrehemu alikuwa bado mdogo vile vile. Wakati kicheko na omary omary bado ommy ni mkubwa. Hisani walishakuja maeneo ya tandika bandari enzi hizo parifurika watu ikawa historia, katika harakati za kuburudisha likatokea timbwili si unajua tena masela , ilikuwa balaa show ikafa watu walipotea na raia kama wawili walidedi. Hao waliodedi walikuwa masela waliochukuliana demu maana hiyo piga yake balaaa sijui silaha walizipigilia viunoni! Braza wangu alirudi hom na kandambili moja.
Daah hapo nimekupata mkuu, kwa hiyo hizo nyimbo za gari kubwa ww hauna?
 
fanya hivyo mzee ukizipata kama zikiwa kubwa ziupload kwenye soundcloud halafu unaweka link kwenye hii thread, nitashukuru sana nikizipata.
Yah na zile zilikuwa kubwa kweli maana nyimbo ya pili ikiingia walikuwa wanaunganisha wale jamaa. Yaani unaona kinanda kinabadilika.
Mfano ile nyimbo "nawaeleza visonoko wasiopenda hisani,
Na mimi nawaeleza hisani yasonga mbele"
Hii nyimbo inaunganika na Ally mwinyi ni hodari
 
Yah na zile zilikuwa kubwa kweli maana nyimbo ya pili ikiingia walikuwa wanaunganisha wale jamaa. Yaani unaona kinanda kinabadilika.
Mfano ile nyimbo "nawaeleza visonoko wasiopenda hisani,
Na mimi nawaeleza hisani yasonga mbele"
Hii nyimbo inaunganika na Ally mwinyi ni hodari
Mkuu popote ulipo bado ujazipata tu hizo nyimbo.
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom