Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

Yaah ilikuwa hivyo.Halafu kuna ile Tulikuwa maskani maskanii famagusta .
Mwendelezo umenitoka kidogo hapo mtu akikumbuka ashushe mistari hiyo
tulikuwa maskaani
maskani famagusta
kukaa kidogo kaja mtu
kaja anatuuliza
Kipaka kafa saa ngapi?
watu wote tukashangaa
tulikuwa hatuna habari
kwenda kuuliza kumbe kweli
Alihamdulillah


sio yeye peke yake
safari hii yetu sotee
yeye ametangulia
hata bwana Nanga na wewe utakwenda tu
sio yeye peke yake
yeye ametangulia
hata bwana Gusa utakwenda tu
........................
 
tulikuwa maskaani
maskani famagusta
kukaa kidogo kaja mtu
kaja anatuuliza
Kipaka kafa saa ngapi?
watu wote tukashangaa
tulikuwa hatuna habari
kwenda kuuliza kumbe kweli
Alihamdulillah


sio yeye peke yake
safari hii yetu sotee
yeye ametangulia
hata bwana Nanga na wewe utakwenda tu
sio yeye peke yake
yeye ametangulia
hata bwana Gusa utakwenda tu
........................
Mule mule swahiba yangu nimekumbuka mbali kiasi ya muongo mmoja na nusu.
 
Acha kabisa, jamaa alikiwa na mkwara sio mchezo, alikuwa na pingu kiunoni, bastola, Rungu na kifimbo cha polisi
Na sarakasi juu! Nilikuwa namuona TAIFA, siku za mechi. Atakuwa kastaafu.
 
"Hisani"
"Gari kubwa"

Yes. Ilisumbua sana enzi hizo. Hawakuwa na mpinzani kwa muda mrefu mpaka alipokuja kuibuka mtu alieitwa OMARY OMARY.

HISANI sina uhakika kama bado ipo. Ilipitia changamoto nyingi sana ikiwemo ile ya MCHIRIKU kukosa taswira chanya kwa jamii na jeshi la police.

Kingine HISANI ilipata pigo baada ya baadhi ya nyota wake KULOWEA MOROGORO na kuanzisha band kule!

Huo wakati ambao OMARY OMARY kashika kasi na bado kulikuwa na vikundi vingine vinakuja juu!

Labda nikuambie, kama weee ni msikilizaji wa GENGE la eFM kuanzia saa mbili usiku, yule jamaa anaemiliki ile SHOW anaitwa KICHEKO.

KICHEKO alikuwa uti wa MGONGO wa HISANI sambamba na MUDDY KADOGO, MFAUME, CHIDIDE, THOMSON, BWANA KULWA naomba niwataje wache.

Kwa kifupi ni kwamba, pale eFM ule mziki wa SINGELI umepewa mwenyewe. HAMAD! KUCHA NA UPELE, HIVI HAPA.
Kumbe kicheko ni wa kitambo kwenye game ta muziki wa kitaaa.
 
Ah nalialia mama, nakulilia mama we,
Uko wapi mama, napata tabu mama we, sikuoni mama nakutafuta mama we
Hawa jamaa walikuwa wanaimba, kama kuna link ya kupata nyimbo za gali kubwa, 7 survivor, atomic nk aiweke hapa
 
Ah nalialia mama, nakulilia mama we,
Uko wapi mama, napata tabu mama we, sikuoni mama nakutafuta mama we
Hawa jamaa walikuwa wanaimba, kama kuna link ya kupata nyimbo za gali kubwa, 7 survivor, atomic nk aiweke hapa
7 survivor na jagwa ndo zinapatikana mtandaoni za gari kubwa hata hazionekani labda utafute wakongwe wanaweza kuwa nayo,
 
HISANI MUSICAL CLUB maskani yake ilikuwa mwananyamala MANJUNJU enzi hizo miaka 93 94 kama sikosei basi 95 KOMANDO YOSSO wakiwa HEWANI(upgrade to PANYA ROAD now)
na kina MUDDY KADOGO CHIDIDE nk maskani yake ilikuwa pale MWANANYAMALA Kwa manjunju na album yao kari iliotamba ni ya GARI KUBWA TISHIO ikiambatana na nyimbo kali zenye vionjo vikari kama
"nalialia ooh mamaoo uko wapi mama ooh"
"shemeji kaulamba mkopo wa sukari"
"nataka kubebwa ooh nataka kunyonya eeh"

Tulikuwa maskanii
Kukaa kidogo kaja mtu
Kaja anatuuliza
Eti bwana kipaka kafaa saa ngapi
Watu wote tukashangaa
Kwenda kuuliza kumbe kweli !!

Sio yeye peke yakee
Yeye ametanguliaaa
Hata bwana darcity atakwenda tuuu "

bwana CHIDIDE sina ubaya naee
MUDY kadogoo sina ubaya naee
slim5 sina ubaya naee
guasa amboni sina ubaya naee
Hikma sina ubaya naee
maswara kudensa ooh maswara kupeta oooh
ilikuwa hatari sana enzi hizo ni watoto pori
kumtoa mwali linafungwa hilo GITA hiyo ngoma bagamoyo pande za MATIBWA nikikumbuka hiyo siku nawakumbuka masela wangu wengi sana sema ndo hivyo miaka hairudi nyumaa

rapa wao mkari MUDDY KADOGOO ezi hizo madem wanamshobokea usipime sasa hivi kachoka mbaya na unga bonge la teja lipo pale kinondoni manyanya mara ya mwisho nilimuona mwaka juzi ferry anauza samaki akaniambia yupo sana pale manyanya
washikaji wengne sijui wapo wapi ila karibu nusu yao wamekufa na hiyo bendi haipo tena ilikufa tangu miaka ya 97 98 hivi baada polisi kulifutilia mbali kundi la Kijambazi la KOMANDO YOSSO na bendi ikapotea hapo wengine walikimbia mikoani wengne walidakwa wapo kolokoloni mpk sasa wengine walidedishwa
baadae ilihasisiwa JAGWA MUSIC watoto wa jolijo baada kuibuka
7 SUVIVAL kwa kasi
We jamaa ni noma sana.
 
Kumbe kicheko ni wa kitambo kwenye game ta muziki wa kitaaa.
Naomba nikuweke sawa kaka mkubwa. Huyu KICHEKO w E-fm ambae kwa sasa yupo clauds, sio kicheko wa gari kubwa (HISANI). Wakati hisani wanapiga nyimbo zao enzi hizo kicheko huyu wa genge la singeli alikuwa mtoto mdogo sana. Wale hisani walikuwa wanapatikana mwananyamala wakati kicheko na dogo mfaume wote watoto wa temeke. Kicheko kazaliwa mikoroshini temeke. Hakuwahi kuimba mnanda. Hisani walikuwa dizain kama ya watu wazima kipindi hicho sasa angalia Age ya kicheko sasa hv ni viwili tofauti. Wakati jamaa wanatamba hata huyu marehemu omary omary, Allah amrehemu alikuwa bado mdogo vile vile. Wakati kicheko na omary omary bado ommy ni mkubwa. Hisani walishakuja maeneo ya tandika bandari enzi hizo parifurika watu ikawa historia, katika harakati za kuburudisha likatokea timbwili si unajua tena masela , ilikuwa balaa show ikafa watu walipotea na raia kama wawili walidedi. Hao waliodedi walikuwa masela waliochukuliana demu maana hiyo piga yake balaaa sijui silaha walizipigilia viunoni! Braza wangu alirudi hom na kandambili moja.
 
Hapana mkuu bado sijazipats
Nyimbo za hisani mtandaoni hakuna. Only cassette. Hata me nilikuwa nayo ila nilipata kumuazima rafiki yangu nae akanogewa akaja akampa mtu basi kadhulumiwa ikapotea. Ningeweza hata ku record nikatupia humu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom