Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

Jana baada ya mdau kuzungumzia JAGWA ikabidi niende tube mate nikakuta wimbo wao wa kondakta nimecheka sana kondakta a nataka kuchukua nauli kwa mgambo mgambo hataki anasema yeye chombo cha dola.
Upitie tena huu wimbo na utamsikia mwimbaji akisema hivi hii ni sauti ya chaukucha family eh,watoto wadogo waliokomaa kichwa kutoka kulekule kwa kopa,hii ni ishara kuwa nyimbo hii haikuimbwa na jagwa bali ni nyimbo ya chaukucha family na huu wimbo huyu mwimbaji(Igosh) anawapiga dongo jagwa kutokana na ugomvi uliomfanya ahame jagwa muzik(dege la jeshi) na kuhamia chaukucha family
Nalog off
 
Katika watu waliokuwa hatari wanaoweza kulaza Mtaa mzima saa6 ya mchana ni huyo Nanga Boy Simela na wenzake wakina Chichi Baunsa. Dah tumekulia katika mazingira hatarishi sana kwa malezi ya kitaa,tunashukuru sana Mungu kutuepusha na vishawishi na mabaya yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu masela wote wataenda peponi.
Mi ulevi wangu ni jagwa muziki,tokea baba dullah,baba J R.I.P,Igosh na dogo jack simela R.I.P,walipokuwepo nipo na nimeshanusurika kufa kwa ajili ya mnanda.
Nalog off
 
Tulikua tumekaa, maskani Lebanon ferry,
Tumestarehe Sina lile wala hili,
Kumbe kuna msela mmoja mtaani kafanya zari,
Mara mda mdooogo,
Wakaja Polisiii,
Wakaja na gari laooooo,
Kufika wakatukamataaa,
Mahakamani tukafikaaaaa,
Tukasomewa Shitakaaaaaaa.
Huyu ni marehemu baba J na hii ndio album yake ya kwanza ndani ya jagwa na ni volume ya tatu ya kundi la jagwa muziki.
Baba J aliimba kwenye kundi la jagwa volume namba 3,4 na 5 na baada ya hapo alihamia kundi la wanyamwezi family,nyimbo hii kama alijitabiria kuhusu kukamatwa kwake basi akakamatwa(jumba bovu lilimuangukia) na volume namba 6 ikaimbwa na Igosh na nyimbo akamtungia inaitwa jela haina mwenyewe, baba j alifia jela kama sikosei.Mungu amuweke pema
Nalog off
 
Mkuu masela wote wataenda peponi.
Mi ulevi wangu ni jagwa muziki,tokea baba dullah,baba J R.I.P,Igosh na dogo jack simela R.I.P,walipokuwepo nipo na nimeshanusurika kufa kwa ajili ya mnanda.
Nalog off
Enzi za kinanda cha Omary Omary na ile hadithi ya hereni. Mchiriku unapigwa mwananyamala tunavuka bonde lile kupitia pale magomeni gereji karibu na gesti ya Jerusalem tunazama mwananyamala
 
Hisani "Gari kubwa" hii bendi ilishakufa baada ya waimbaji wake baadhi kuhamia morogoro, baadhi waliobaki Dar wakaamua kuanzisha kundi jipya na jina jipya ikaitwa JAGWA MUSIC.
HISANI au GARI KUBWA wapinzani wao wakubwa walikuwa wanaitwa TOPAZ ambayo nayo pia haikudumu muda mrefu ikavunjika baadhi yao wakaanzisha kundi jipya likiitwa SEVEN SURVIVOR yaani waliosalia na kuanzisha kundi jipya walikuwa ni watu saba chini ya kiongozi wao JUMA MPOGO a.k.a GENERAL LUPOZ.
Kipindi cha ambacho bendi hii ya HISANI na TOPAZ zipo kwenye chati OMARY OMARY alikuwa bado hajaanza kusikika, baadae hizi bendi zilivyokufa na kuzaliwa upya yaani JAGWA na 7 SURVIVOR ndipo OMARI OMARI nae akaja na bendi yake ikiitwa ATOMIC na wimbo wake uliotamba sana ni "said dabani" na baadae "mfungwa hachagui gereza" na nyingine nyingi tu.
Kipindi hicho hata Bongo flavour haijulikani.
RIP General Lupozi
 
Huyo anachanganya habari,maneno ya kusikia anageuza ya kwake.Kipaka ametajwa na Omary Omary kwenye nyimbo iitwayo "Kipaka memory",na bendi ni Atomic Music iliyokua chini ya watu kama Omary Mwenyewe,Saidi Ndiga,Mwankoto Ngoma na wengineo.
 
Duh! weye mtu unanikumbusha mbaliiii kuna kitu inaitwa said dabani kuna mdau kasema mchiriku na wizi kama pete na kidole naungana nae.
"Washkaji karibuni
Karibuni maskaniii
Na wala msione kimyaaa
Said dabani hatumuoniii
Said dabani amefarikiii
Kwa ajali ya gariii
Ambayo imetokeaaa
Buguruunii
Said dabani kaacha majonzii
Hata kwa mzazi mwenzie
Pili mama Ali anabaki analia ooooooh
Duh nimekumbuka hapo.
Saidi Dabani ipo kwenye Atomic no. moja,kiukweli kwa wakati huyo mziki huo na wizi vilikua ni pacha.Saidi Dabani mwenyewe alikua mtu wa ndole.
 
dunia hii *4, kuna vilema dunia hii kuna viwete dunia hii kwani hao wote wameumbwa na mola eeh na ridhiki yao iko kwa mola. Ahh chidide toa heshima! . Ukitaka kuinjoi mziki huu lazima uwe high kidogo usiku mnene
Hao uliowaimba ni Seven Survivor chini ya general Juma Mpogo,wakati huo bado wako katika level za "Matajiri watoto"
 
Jana baada ya mdau kuzungumzia JAGWA ikabidi niende tube mate nikakuta wimbo wao wa kondakta nimecheka sana kondakta a nataka kuchukua nauli kwa mgambo mgambo hataki anasema yeye chombo cha dola.
Halafu wengi wanachanganya,hata wanaorusha mitandaoni wengi hawajui.Wimbo wa Kondakta wenyewe ni #Chaukucha,bendi hii ilipata umaarufu baada mvuragano kutokea pale Jangwa.Wale waliojiita wandewa wa Mwananyamala wakaenda kuunda bendi waliyoipa jina Chaukucha ambayo maskani yao ilikua Mwananyamala kwa Kopa.
 
hiyo atomic na huyo marehem Omar omar.Nakumbuka marehem alianzia Topaz ngoma kabla ya kuunda Atomic
Yap,ahsante mdau kwa kuwa na kumbukumbu,wakati huo Omary anaimba kama demu,baadae ndio wanatimka na machizi kama akina Ndigalu wa Melini na akina Mwamkoto kwenda kuanzisha Atomic Ngoma na baadae inakua Atomic Music.
 
Kukaa kidogo kaja mtu,kaja anatuuliza,eti Kipaka kafa saa ngapi?,watu wote tukashangaa,tulikua hatuna habari,kwenda kuuliza kumbe kweli.Sio yeye pekeyakeeee,yeye ametanguliaaa..........
 
Upo sahihi, huo wimbo aliimba OMARY OMARY. Hivi huyo ni MKAMA SHARP ama MKAPA SHARP? Daah, mdau hapo juu katambaa na mistari balaaa! Ahsanteni. Old is gold.
Mkama Shapu,askari mmoja mnoko sana na alikua na ubavu,yaani swala la kuwasongesha watu kumi ni jambo la kawaida.Wahuni wa mjini miaka hiyo walikoma nae!.
 
7 survivor na jagwa ndo zinapatikana mtandaoni za gari kubwa hata hazionekani labda utafute wakongwe wanaweza kuwa nayo,
Bendi nyingi za mnanda hazipo mtandaoni,hata hizo zilizokuwepo nazo nyimbo ni chache tu,nyingi hamna.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom