mchina na Ng'ombe Wanaotoa Maziwa ya Binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mchina na Ng'ombe Wanaotoa Maziwa ya Binadamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wanasayansi wa nchini China wamefanikiwa kuwatengeneza ng'ombe wanaotoa maziwa kama yale yanayotolewa na wanawake wanaonyonyesha.
  Wanasayansi wa nchini China wametamba kuwa wamefanikiwa kuwatengeneza ng'ombe 300 wanaotoa maziwa kama ya BINADAMU.

  Katika ripoti ya wanasayansi hao iliyotolewa kwenye jarida la Public Library of Science One journal, wanasayansi hao walisema kuwa wamefanikiwa kuwatengeneza ng'ombe wanaotoa maziwa yenye protini ya Lysozyme ambayo hupatikana kwenye maziwa ya binadamu pekee ambayo humwezesha mtoto kuweza kujilinda na maradhi mbalimbali.

  Wanasayansi hao waliifanyia marekebisho embryo ya ng'ombe na kisha kuipandikiza mimba kwenye ng'ombe jike ambaye alipozaa alizaa ng'ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa kama ya binadamu.

  "Maziwa haya ni tofauti kabisa na maziwa ya kawaida ya ng'ombe, yana ladha tofauti na maziwa ya ng'ombe", alisema Profesa Ning Li, kiongozi wa utafiti huo katika chuo kikuu cha China Agricultural University.

  "Tuna malengo ya kuuza baadhi ya tafiti za ugunduzi huu ndani ya miaka mitatu ijayo", alisema Profesa Ning Li na kuongeza " Itachukua kama miaka 10 kabla ya watu hawajaanza kununua maziwa ya binadamu madukani".

  Profesa Li aliongeza kuwa maziwa hayo yatakuwa na virutubisho vingi muhimu kwa mwili wa binadamu.

  Hata hivyo utafiti huo umewagawanya watu ambapo baadhi wanaupinga huku wengine wakiuunga mkono.

  "Tuna wasiwasi mkubwa na utafiti huu wa kuwafanyia marekebisho ng'ombe na kuwapandikiza vinasaba vya binadamu", alisema Helen Wallace, mkurugenzi wa GeneWatch UK.

  "Kuna maswali mengi kama maziwa haya yatakuwa salama kwa binadamu, inabidi yafanyiwe majaribio makubwa kama majaribio yanayofanywa kwa madawa katika kuchunguza kama yatakuwa hayana madhara kwa binadamu", aliongeza bi Helen Wallace.

  Hata hivyo Profesa Keith Campbell, mtaalamu wa baiolojia katika chuo kikuu cha University of Nottingham nchini Uingereza amepingana na bi Helen na kusema kuwa kama taratibu zote za kitaaluma kuhusiana na vinasaba zitatumika maziwa hayo hayatakuwa na madhara yoyote kwa binadamu.

  5574814.jpg
   
 2. K

  King kingo JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hao ndio wachina zaidi ya uwajuavyo hahahah....
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  chuo chenyewe feki
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Busara itaendelea kuwa kwa binadamu kuwanyonyesha watoto wao wenyewe.
   
Loading...