Mchina mbaroni kwa kuchimba madini kwenye pori la akiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchina mbaroni kwa kuchimba madini kwenye pori la akiba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by cement, Sep 10, 2012.

 1. cement

  cement JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 583
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  TANZANIA KWELI NI SHAMBA LA BIBI HILI INGEMKUTA MTZ HALI INGEKUWA MBAYA SANA LAKINI KWA SABABU NI MCHINA HATA FAINI ANAYOPEWA DUH HATARI SANAAAAAA


  Mkurugenzi wa Kampuni ya REDore Mining mwenye asili ya Asia Chaoxian Zhou amehukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini jumla ya Shilingi 1,350,000/= kwa kukutwa na makosa mbalimbali likiwemo lakuchimba madini ndani ya hifadhi ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi kinyume cha sheria .  Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama pori Paul Sarakikya, mtuhumiwa amelipa faini na kuachiwa huru.Makosa megine aliyopatikana nayo ni pamoja na kuingia ndani ya Pori la Akiba Lwafi kinyume na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu cha 15 na kuharibu mimea ndani ya Pori la Akiba kwa kukiuka kifungu cha 18 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori.  Makosa mengine ni pamoja na kuchimba madini ndani ya Pori la Akiba bila kibali kinyume na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori na kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na kifungu cha 95(1) (c) cha Sheria ya madini Na. 14 ya mwaka 2010.  Mshtakiwa alikiri makosa yote mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Richard Kasele na Mwendesha Mashtaka Bwana Prosper Rwegerera na kupatikana na hatia ya kuchimba madini katika eneo la Kanyamakaa lililoko katika Wilaya ya Nkasi kinyume cha sheria ya Kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.  Taarifa hiyo imefafanua kuwa mshitakiwa ameamriwa kuondoa mitambo iliyokutwa ndani ya Pori la Akiba la Lwafi na kufukia mashimo na mitaro yote iliyochimbwa kutokana na shughuli za Kampuni hiyo ndani ya siku saba. Aidha Madini yaliyokuwa yamechimbwa katika eneo hilo ambayo thamani yake bado haijajulikana yametaifishwa na Serikali.  Chaoxian Zhou na mwenzake Wei Lyu ambao wote ni raia wa China walikamtwa Julai 25, 2012 ambapo iligundulika kuwa Wei Lyu hakuwahi kwenda mkoani Katavi wala katika Hifadhi hiyo ya Lwafi na kuchimba madini hivyo aliachiwa huru.
   
 2. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baadhi ya raia wa China na Watanzania wakishirikiana kuchimba madini katika pori la Akiba la Lwafi,wilayani Nkansi kinyume cha sheria,ambapo raia hao wa china walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kulipa faini.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya REDore Mining mwenye asili ya Asia Chaoxian Zhou amehukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini jumla ya Shilingi 1,350,000/= kwa kukutwa na makosa mbalimbali likiwemo lakuchimba madini ndani ya hifadhi ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi kinyume cha sheria .


  Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama pori Paul Sarakikya, mtuhumiwa amelipa faini na kuachiwa huru.Makosa megine aliyopatikana nayo ni pamoja na kuingia ndani ya Pori la Akiba Lwafi kinyume na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu cha 15 na kuharibu mimea ndani ya Pori la Akiba kwa kukiuka kifungu cha 18 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori.


  Makosa mengine ni pamoja na kuchimba madini ndani ya Pori la Akiba bila kibali kinyume na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori na kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na kifungu cha 95(1) (c) cha Sheria ya madini Na. 14 ya mwaka 2010.


  Mshtakiwa alikiri makosa yote mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Richard Kasele na Mwendesha Mashtaka Bwana Prosper Rwegerera na kupatikana na hatia ya kuchimba madini katika eneo la Kanyamakaa lililoko katika Wilaya ya Nkasi kinyume cha sheria ya Kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hii habari imeniharibia kabisha Ndovu zangu nilizokuwa nakunywa! Mgeni amekamatwa anachimba madini halafu anapigwa faini ya maandazi!? This is only in Tanzania.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Kule kwao huyo bwana asingekuwa hai, wangeshatenganisha kichwa na kiwiliwili!!!!
   
Loading...